Kocha Mkuu wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Faouzi Benzarti
KOCHA Mkuu wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Faouzi Benzarti, ameingia mitini baada ya kushindwa kutokea katika mkutano wa makocha na waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Benzarti alishindwa kuhudhuria mkutano huo kwa madai walichoka baada ya kuwa angani kwa saa tisa wakitokea Tunisia ambapo waliwasili Dar es Salaam jana alfajiri.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, Benzarti aliwataarifu kwamba asingefika kwenye mkutano huo na kuwaomba radhi kutokana na hilo.
Pamoja na kushindwa kutokea kwa kocha huyo, Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm alisema amezikamata mbinu za Etoile du Sahel na atahakikisha wanashinda mchezo huo wa raundi ya pili wa Kombe la Shirikisho Afrika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.