Friday, December 05, 2014

MUGABE ASEMA HANG'OKI MADARAKANI..!!!

Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani. 
 
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Hasira ya Mugabe ilionekana kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI: TULIPANGA KUMWOKOA SOMERS

Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013, ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa, yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33, alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa, ukiwemo mtandao wa BBC. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Thursday, December 04, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS DESEMBA 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

2014 NI MWAKA WA JOTO KALI DUNIANI

Viwanda vikitoa moshi angani na kuchafua mazingira
Mwaka huu unaoishia unasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha joto duniani na kwa Uingereza tangu kumbukumbu zianze kutunzwa.
Makadirio ya awali yanaonyesha kuwa katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2014, wastani wa kiwango cha hali ya joto duniani kilikuwa 0.57C juu ya wastani uliokuwepo muda mrefu.
Dhoruba nchini Uingereza iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi
Na miezi kumi na mmoja ya kwanza nchini Uingereza imezalisha wastani wa joto la 1.6C likiwa juu ya wastani uliokuwepo kwa muda mrefu.Utafiti mwingine uliofanywa na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza umeonyesha kuwa ongezeko la viwango vya joto vilivyoshuhudiwa, visingetokea bila ya ongezeko la gesi zinazoharibu mazingira kutokana na shughuli za binadamu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

IS WAFUNGUA KAMBI ZA MAFUNZO LIBYA

 Wapiganaji wa Islamic State katika jimbo la Anbar,Syria Marchi 2014 
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wafungua kambi za mafunzo Libya
Wapiganaji wa kundi la Islamic State wameanzisha kambi za mafunzo mashariki mwa Libya, amesema mkuu wa kamandi ya Marekani ya masuala ya Afrika.
Wapiganaji wa Kikurd wakiwa katika mafunzo ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State Septemba 2014 nchini Iraq.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

AFCON 2015 MAKUNDI YA TIMU 16 YATAJWA

Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, AFCON 
 
Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:

Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea

Wenyeji Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CHELSEA HAISHIKIKI LIGI KUU ENGLAND

Ivanovic akishangilia na Drogba baada ya Drogba kuifungia timu yake ya Chelsea bao la pili katika mechi hiyo 

Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya England kushuka viwanjani.
Chelsea, wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata kuzipa nafasi timu nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na timu hizo.

Sergio Aguero, mchezaji wa Manchester City akishangilia moja ya magoli yake katika ligi kuu ya England
Chelsea imeendelea kuwa na tofauti ya pointi sita na Man City inayoifuatia baada ya kuirarua Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City yenye pointi 30 ikiisasambua Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia timu yake ya Manchester City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na Zabaleta kila mmoja akifunga bao moja. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, December 03, 2014

KAFULILA ALIVYOIBUA UFISADI WA AKAUNTI YA ESROW


Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna alivyoibua sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow na kudokeza kuwa kitendo cha baadhi ya watuhumiwa kugoma kujiuzulu, kinaonyesha kuna watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia suala hilo kila mara bungeni hadi uamuzi wa kulijadili ulipofikiwa, amesema ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho wake.

Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa mahakamani.

Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti za escrow, fedha hizo zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa kwa mmiliki mpya wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), jambo lililosababisha kuibuka kwa kashfa hiyo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


DSC06413
DSC06413
DSC06414
DSC06415
DSC06416 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA: ESCROW NI MATOKEO YA KATIBA ISIYO NA MAJIBU

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. PICHA|MAKTABA 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wizi wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, mvutano kati ya mihimili ya dola na viongozi kukosa maadili ni matokeo ya nchi kuwa na Katiba isiyo na majibu ya masuala hayo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Jaji Warioba alisema Bunge la Katiba lilifanya makosa kutoviweka vifungu vinavyozungumzia mambo hayo katika Katiba Inayopendekezwa ambavyo awali vilipendekezwa na Tume yake katika rasimu ya pili.

“Katika mchakato wa Katiba Mpya tulisema kuwe na mgawanyo wa madaraka na kila mtu ajue madaraka yake ni nini na kutenganisha Serikali na Bunge. Kama Serikali na Bunge vingetenganishwa bungeni usingeibuka mvutano kuhusu waliochota fedha za escrow. Bunge lingekuwa huru katika utendaji wake wa kazi,” alisema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SPIKA ASEMA WALIOKEKETWA HAWAFAI

Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga awashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa.

Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.
Kulingana na gazeti la daily Monitor,Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa sherehe ya kitamaduni ambayo inapinga ukeketaji ilioandaliwa na mfuko wa umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MLIPUKO MKUBWA MOGADISHU

Mlipuko wakumba mji wa Mogadishu nchini Somali.
 
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia karibu na uwanja wa ndege.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DROO YA KOMBE LA AFRIKA KUFANYIKA LEO

Droo ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kufanyika leo usiku mjini Malabo nchini Equitorial Guinea.
 
Mabingwa wa zamani Zambia na waandalizi wa kombe la bara Afrika Equitorial Guinea ni miongoni mwa timu zitakazoorodheshwa katika droo ya kombe hilo la mwaka 2015 Jumatano usiku.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF tayari limezigawanya timu hizo 16 katika makundi vyungu vinne vya kinyang'anyiro hicho cha january 17 hadi februari 8.
Hatua hio ilifanyika kulingana na utendaji wa timu hizo katika awamu tatu ya michuano hiyo na mechi za kufuzu katika kipindi hicho hicho.
Miongoni mwa vitu ambavyo vilitiliwa mkazo ni matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.
Droo hiyo ambayo itabuni makundi manne yanayoshirikisha timu moja moja kutoka kila chungu itafanyika mjini malabo jumatano usiku. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Ghana na Ivory Coast ni timu nyengine kubwa huku washindi wa pili wa mwaka 3013 Burkina Faso wameorodheshwa katika kundi la Pili.
2015 Nations Cup :Timu zilivyowekwa.
Pot 1: Equatorial Guinea, Ghana, Ivory Coast, Zambia
Pot 2: Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria
Pot 3: Cape Verde, South Africa, Cameroon, Gabon
Pot 4: Guinea, Senegal, DR Congo, Congo

Monday, December 01, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA ASSAD KUWA CAG MPYA


Profesa Mussa Juma Assad 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz 

BOKO HARAM WAVAMIA MIJI MIWILI NIGERIA

Nia kuu ya Boko Haram ni kuwa na dola ya kiisilamu inayofuata sheria za kiisilamu.
 
Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi katika miji miwili eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
La kwanza lilikuwa la kujitoa mhanga pamoja na shambulizi lengine katika kituo cha polisi cha Damaturu.
Wenyeji wa mji wa Maiduguri walielezea kusikia milipuko miwili kwenye soko moja.
Mashambulizi mengine ya kujitoa mhanga eneo hilo wiki iliyopita yaliwaua zaidi ya watu 70.
Mapema leo Jumatatu watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliteketeza kituo cha polisi katika mji wa Damataru kilicho umbali wa kilomita 100 Magharibi mwa mji wa Maiduguri.
Inaarifiwa watu 5 wameuawa katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotokea katika soko lililokuwa na watu wengi.
Mjini Damaturu , milipuko na milio ya risasi ilisikika huku wanamgambo hao walipokuwa wanashambulia mjini huo.
Boko Haram imeahidi kubuni dola ya kiisilamu katika maeneo ambayo kundi hilo linadhibiti.
Milipuko hio ilitokea Jumatatu katika soko la Maiduguri , mji mkuu wa jimbo la Borno ambayo ilisababishwa na wasichana wawili waliojilipua.
Takriban watu 32 walijeruhiwa katika milipuko hio. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...