Saturday, October 18, 2014

UN YATETEA JUHUDI ZA KUAANGAMIZA EBOLA

David Nabarro katikati
Mratibu wa shughuli za Umoja wa mataifa kuhusu ugonjwa wa ebola Davis Nabarro ametetea juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo magharibi mwa afrika.
Bwana Nabbaro alikuwa akijibu shutma kutoka kwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF lililosema kuwa ahadi za misaada hazijakuwa na mafaniko yoyote katika vita dhidi ya ugonjwa wa ebola.
Ameiambia BBC kuwa mipango iko njiani ya kutoa vitanda 4000 kwa wagonjwa wa ebola ifikiapo mwezi ujao.
Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya ndani ya shirika la afya duniani inayosema kuwa WHO imeshindwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM KUWAACHIA WANAFUNZI




Wanafunzi wa Chibok waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram

Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Mkuu wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais wa Chad Idris Derby.
Alisema kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, October 17, 2014

CHADEMA WAANZA SAFARI YA KUPINGA KATIBA NCHI NZIMA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akizungumza kwenye mkutano na waandishi Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed. 

Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendesha kampeni ya kupinga Katiba Inayopendekezwa kwa viongozi wake wakuu pamoja na wale wa mabaraza yake kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
Hatua hiyo imekuja siku tatu, tangu Rais Kikwete autangazie umma wa Watanzania alipokuwa akihutubia kilele cha Mbio za Mwenge mkoani Tabora kwamba Katiba Inayopendekezwa inafaa hivyo kuwataka Watanzania waipigie kura wakati wa mchakato wa kura ya maoni.
Ziara ya Chadema itaanzia katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako itachukua siku 20 ikiongozwa na Baraza la Wanawake (Bawacha), linaloongozwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na baada ya kumaliza, itaanza ziara nyingine ya siku 20 itakayofanywa na Baraza la Vijana (Bavicha).
Dk Slaa alisema CCM wameanza kazi ya kuwataka wananchi kupiga kura ya ‘ndiyo’ na Chadema wanaanza mikutano ya kuwashawishi wananchi kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana’.
Alisema kuanzia Novemba 5 mwaka huu, viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho nao wataanza ziara katika mikoa mbalimbali nchini.
“Bawacha ndiyo itakuwa timu ya kwanza. Itakwenda Mwanza mjini, Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Busanda, Bukombe, Biharamulo, Muleba, Karagwe, Bukoba Mjini, Chato, Shinyanga Mjini na Maswa Mashariki,” alisema Dk Slaa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA: MSIKURUPUKE KUPITISHA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Picha na Maktaba 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka Watanzania kutokurupuka kuipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa imeyaacha kando maoni yao mengi na akawataka waisome kwa makini kabla ya kuikubali au kuikataa.
Akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Harrieth, Jaji Warioba aliulizwa na kujibu maswali; anaionaje Katiba Inayopendekezwa na iwapo CCM imemgeuka kwa nini asihame chama?
Akijibu maswali hayo, Jaji Warioba alisema Katiba hiyo haina maoni yote ya wananchi kama Bunge Maalumu lilivyojinadi, bali yamewekwa machache ambayo hata hivyo yamo hata katika Katiba ya sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DIDA, JAJA, WABEBA JUKUMU ZITO YANGA


kipa Deogratius Munishi 'Dida' 

Pambano la watani wa jadi, Yanga na Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam litakuwa mtihani mkubwa kwa nyota watatu wa Yanga kwa sababu tofauti.

Watatu hao ni mshambuliaji, Genilson Santos ‘Jaja’ , kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na kiungo Andrey Coutinho.

Jaja, aliyeibuka shujaa ghafla alipoitungua Azam kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, kisha akapoteza makali tangu Ligi Kuu ianze,  ana deni kubwa kwa mashabiki wenye matumaini kwake kuwa atafungua akaunti ya mabao dhidi ya Simba.

Makali yake ya Septemba 14 alipoisulubu Azam yaliyomkatia tiketi ya kuwa kipenzi cha mashabiki na  yanaweza kuongezeka au kufutika.

Mbrazili huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga, ingawa pia anaweza kuwa na wakati mgumu kesho kuthibitisha uwezo wake, kutetea nafasi yake kwenye kikosi  cha kwanza, akishindwa kuisaidia Yanga kuchomoza na ushindi, itakuwa tiketi yake ya kusahaulika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

DSC04323
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Tuesday, October 14, 2014

WAZIRI LAZARO NYALANDU AZUNGUMZIA TETESI ZA KUTANUA NA AUNT EZEKIEL NCHINI MAREKANI

 
Baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(Pichani juu) na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari nchini Marekani hatimaye waziri huyo 
Aunt Ezekiel
alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji kazi wake.

Nyalandu alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.

Alikana kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima yake mbele ya jamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAMA KANUMBA NA LULU NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO "MAPENZI YA MUNGU"

Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAASKOFU KATOLIKI WAUZUNGUMZIA USHOGA


Mkutano wa maaskofu Vatican
 
Makasisi wanaoshiriki katika mkutano wa maaskofu wanaangazia masuala ya mafunzo ya kanisa katoliki kwa familia ,wametoa mwito kwa kanisa hilo duniani kuwachukulia watu wenye mapenzi ya jinsia moja kwa usawa
Kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Ripoti hiyo haitoi changamoto yoyote kwa msimamo wa muda mrefu wa kanisa hilo juu ya kupinga ndoa za jinsia moja,lakini baadhi ya vikundi vya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanachukulia kauli hiyo kuwa ya mafanikio makubwa kwa jamii zao.
Na moja ya makundi yenye kushikilia msimamo mkali kikanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuuita ya kisaliti. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WASICHANA WA CHIBOK NIGERIA BADO WANASHIKILIWA NA BOKO HARAM

Aliyekua kiongozi wa Boko Haram, Aboubakr Shekahu
Walikamatwa na kikundi cha kigaidi cha kiislam boko Haram kutoka shuleni kwao huko chibok. Ingawa kunaahadi nyingi kutoka serikali ya Nigeria kwamba wataokolewa na pia watapewa msaada kutoka dunia nzima lakini mpaka sasa bado hawajaonekana, ripoti ya mwandishi wa BBC Will Ross kutoka Lagos inasomwa na Regina Mziwanda
Miezi sita sasa na wasichana 219 bado wametekwa, ni ushaidi kidogo sana unaojulikana kwa kile kilichotokea kuhusu wao tangu walipoondolewa katika shule yao ya bweni huko chibok na boko haram, serikali ya Nigeria imepata wakati mgumu sio tu kuwaokoa lakini pia kwa kuonesha mwitikio mdogo wa umma..
Wazazi wa chibok wameiambia bbc kuwa wameachwa na maneno tu na ahadi zinazovunjwa kwamba watoto wao wa kike watarudi nyumbani hivi karibuni, baba mmoja amesema wanasiasa wamejikita kwenywe uchaguzi wa mwakani ujao zaidi yakuwaokoa watoto wao waliopotea.
Tangu mwezi April vijana wengi wa kike na wa kiume wametekwa nyara na kikundi cha kiislam cha Boko haram ambao wanaongoza mijini na vijijini karibu na mpaka wa Cameroon.
Serikali ya Nigeria imesema jeshi kwa sasa limepata mafanikio dhidi ya vita na boko haram lakini wamezidiwa nguvu kaskazini mashariki ambapo raia hawako salama na maelfu ya watu wamehama makazi yao katika wiki za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA WAWEKA KAMBI KUNDUCHI

Kuelekea kwenye mpambano wa watani wa jadi YANGA Vs SIMBA siku ya jumamosi Oktoba 18, kikosi cha timu ya Young Africans kimeingia kambini leo mchana katika hoteli ya Landmark iliyopo eneo la Kunduchi kujiandaa na mchezo huo ambao umeteka hisia za wapenzi wa soka nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kocha mkuu Marcio Maximo ameingia kambini na kikosi cha wachezaji 28 kujiandaa na mchezo huo ambapo kikosi chake kitakua kikifanya mazoezi katika Uwanja wa Boko – Veterani kila siku kujweka fit kwa kuzisaka pointi tatu muhimu siku ya jumamosi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, October 13, 2014

NDENJELA AZINDUA MABASI MAPYA YA KISASA NDENJELA JET

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua mabasi ya kisasa ya kampuni ya Mwaji Group  jijini Mbeya.
Ndani ya mabasi ya Ndenjela jet.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi wakifurahia maelezo mafupi toka kwa Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LWAKATARE. DDP KUCHUANA UPYA LEO





Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare. PICHA|MAKTABA 


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare leo anatarajiwa kuchuana upya na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakati Mahakama ya Rufani itakaposikiliza maombi ya marejeo ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyomfutia mashtaka ya ugaidi.

Maombi hayo Namba 5 ya mwaka 2014, yalifunguliwa na DPP akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili yeye na mwenzake, Joseph Ludovick.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba Mahakama ya Rufani iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi na kisha ifute uamuzi huo wa Mahakama Kuu na amri zote ilizozitoa.

Pamoja na mambo mengine, DPP anadai kuwa haikuwa sahihi Mahakama Kuu kuamua kuwa mashtaka hayo hayakuwa halali, kwani hapakuwa na taarifa zilizowasilishwa dhidi ya washtakiwa ambazo Mahakama Kuu ingezizingatia katika kuamua uhalali wake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...