Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.
Taswira ya majonzi na kilio ilitanda katika mji
wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo
wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine
kuishia mauti.
Bomu hilo lililipuka mbele ya kituo kikubwa cha biashara, kinachotembelewa na watu wengi.
Walioshuhudia walisema sehemu za miili ya wanadamu zilitapakaa kila mahali sakafuni.
Magari yalichomeka kabisa na vioo katika
madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu kuvunjika vyote. Watu waliokuwa na
hofu walielekea kwenye mahospitali yaliyo karibu ambapo walishuhudia
magari ya wagonjwa yakisongamana kila mahali yakiwaleta wagonjwa na
miili ya waliokufa.
John Tobi Wojioa aliwasili mahali hapo muda mfupi baadaye akimtafuta jamaa wake. Alitaja alichoona kama mafuriko ya damu:
"Kulikuwepo magari ya wagonjwa wa shirika la
FRCS (federal Road Safery Corps) na ya mashirika mengine yaliyokuwa
yakiingia na kuondoka yakibeba miili ya waathirika. Kwenye barabara
alama za damu za nyayo za wanadamu zilionekana kila mahali," alisema
Bwana Wojioa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz