Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana
alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza
kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na
lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.
Mawaziri
wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu
na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati
Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya
upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni
mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha
kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji
cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee,
ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika
kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu
Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba
wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia
Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite
kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz