1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja).
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja).
Hata
hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake
zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.