Friday, May 02, 2014

WATU 19 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Saturday, April 26, 2014

MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

IMG-20140426-WA0034_af1cd.jpg
IMG-20140426-WA0035_686a4.jpg
Umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa mbalimbali (Picha na Awadhi Ibrahim)

G7 YAZIDI KUIBANA URUSI...!!!

Askari wa Ukraine
Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa viwanda duniani G7 wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema wataanza kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya jumatatu na wanatarajia kulenga biashara za binafsi na ambazo zina uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Viongozi hao wa G7 wameelezea kuguswa kwa na jinsi Urusi ilivyoshindwa kuacha kuwasaidia wanaoipinga serikali.
Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.

HAKUNA KATIBA BILA UKAWA...!!!

kingunge c2ea5
Na Hudugu Ng'amilo
MWANASIASA mkongwe na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale – Mwiru, amesema makada wenzake wanaomshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanakitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kumtukana au kumshambulia Jaji Warioba, au wajumbe wengine wa tume hiyo ni sawa na kukitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali.
Kingunge alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akichangia sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya Katiba, ambapo alisema wanaomshambulia Jaji Warioba wanaonyesha utovu wa adabu, kwa kuwa chama kina maadili na adabu katika kushughulikia masuala mbalimbali.
"Mimi sitakubali hata kidogo wajumbe watumie msimamo wa chama kumshambulia Warioba au wajumbe wengine wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, si halali kumshambulia Warioba au mjumbe yeyote yule binafsi.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

WANASIASA WANNE WAZUIWA KUSAFIRI...!!!


Wanasiasa wakuu waliokuwa wamezuiliwa
Wanasiasa wanne wakuu walioachiliwa na serikali ya Sudan Kusini, wamepokonywa hati zao za usafiri walipokuwa wanajiandaa kuondoka nchini humo kusafiri hadi mjini Nairobi Kenya.
Mke wa marehemu John Garanga, Rebecca Garang, ambaye anashikilia cheo cha juu katika chama cha SPLM , ameambia mwandishi wa BBC Robert Kiptoo kuwa serikali haikutoa sababu ya kuwapokonya hati za usafiri wanasiasa hao.
Serikali ya Sudan Kusini iliwaachilia wanasiasa hao waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir Disemba mwaka jana.
Waziri wa sheria alisema kuwa serikali ilifutilia mbali kesi dhidi ya wanasiasa hao wanne wakuu waliotuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi ambayo yamesababisha vurugu za wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Wanne hao akiwemo aliyekuwa kiongozi wa chama cha SPLM, walikanusha madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi, na pia wamekanusha uhusiano wowote na mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini.

UPIZANI AFRIKA KUSINI WAKOSOA SHIRIKA LA SABC

Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha  Economic Freedom Fighters (EFF).
Shirika la serikali la utangazaji nchini Afrika kusini-SABC limeshutumiwa vikali na chama cha upinzani cha Economic Freedon Fighters-EFF kwa kutumia kile chama hicho kinasema ni mbinu zinazofanana na zile za enzi za ubaguzi wa rangi kwenye matangazo yake.
Lawama hizo zinafuatia hatua ya SABC kukataa kupeperusha tangazo la chama hicho cha kisiasa kama sehemu ya kampeni zake kabla ya uchaguzi mkuu wa Mei 7.
Julius Malema, kiongozi wa chama hicho cha EFF ambaye zamani alikuwa kiongozi wa vijana katika chama tawala cha African National Congress (ANC), alisema kukataliwa kwa tangazo la chama chake cha kisiasa kunahujumu mchakato wa uchaguzi ujao.
Chama cha EFF kitashiriki kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
CHANZO:VOA

Friday, April 25, 2014

UAMSHO WAMTAKA LUKUVI ATHIBITISHE KAULI YAKE

Khamis-Yusuf-Khamis-April25-2014 57014 Na Hudugu Ng'amilo.

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), maarufu kama Uamsho imemjia juu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ikimtaka athibitishe kauli yake ya kuwahusisha na Chama cha Wananchi (CUF) pamoja na vitendo vya uhalifu visiwani humo.
Uhalifu ambao Lukuvi anadaiwa kuihusisha Uamsho ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kanisani, ni pamoja na kuuawa kwa padri, kuchoma makanisa na uharibifu wa miundombinu Zanzibar.
Kutokana na hali hiyo, Uamsho wamemwandikia barua Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kumtaka ambane Lukuvi athibitishe tuhuma hizo, vinginevyo watatumia sheria kumchukulia hatua.

Nakala ya barua hiyo, ambayo imeambatanishwa na nakala ya DVD inayoonyesha kauli zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi wa kidini uliofanywa na Lukuvi, imepelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete; Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein; Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Spika wa Baraza la Wawakilishi na wawakilishi wote.
Nakala ya barua hiyo pia imepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Amiri wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Amiri wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar, Ofisi ya Mufti Zanzibar, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Jumaza), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Maimamu wote.
Pia imepelekwa kwa Waziri wa Mipango, Sera na Uratibu wa Bunge, Ofisi ya Spika wa Bunge, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Kamati ya Maridhiano Zanzibar, vyombo vya habari, Waislamu na wapenda amani wote Tanzania. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WANANCHI WANAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA


kigangwala2 7c529
Na Hudugu Ng'amilo.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Twaweza umebainisha kuwa wananchi wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Ripoti ya utafiti huo uliofanyika Februari, mwaka huu kwa njia ya simu za mkononi na watu kuulizwa kuhusu mchakato wa Katiba, inaeleza kuwa kama wananchi wangeipigia kura rasimu hiyo mwezi huo, Katiba hiyo ingepitishwa kwa asilimia 65 Zanzibar na asilimia 62 Tanzania Bara.
Akiwasilisha ripoti hiyo jana, Mtafiti wa Twaweza, Elvis Mushi alisema kati ya watu waliohojiwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 20 wangepiga kura ya hapana, kwa upande wa Zanzibar watu ambao wangesema hapana wangekuwa asilimia 19.
"Watu ambao walisema hawana uhakika na hawajui lolote kwa upande wa Zanzibar ni asilimia 19 na Tanzania Bara asilimia 15," alisema.
"Zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura kutoka Tanzania Bara na Zanzibar walisema wana nia ya kupiga kura ya kuikubali Katiba (rasimu) kama ilivyo sasa."
Muundo wa Serikali
Kuhusu muundo wa Serikali, Mushi alisema: "Asilimia 80 ya Wazanzibari wanaunga mkono muundo wa serikali tatu. Kwa Tanzania Bara wanaounga mkono serikali tatu ni asilimia 43."
Alisema takwimu hizo ni tofauti na zilizotolewa miezi minane iliyopita ilipotolewa Rasimu ya Kwanza ya Katiba, ambayo asilimia 51 ya wananchi wa Tanzania Bara walipendekeza muundo wa serikali tatu. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.

SIKU 67 ZA MIPASHO, MATUSI, BUNGE MAALUM LA KATIBA

bunge 4c2f3
Na Hudugu Ng'amilo.
Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta "Mzee wa Kasi na Viwango" linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.
Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

OBAMA AWASILI KOREA KUSINI

Rais Obama akifanya mashauriano na Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye (kushoto) na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.
Rais Obama amewasili Korea Kusini huku hofu ikizagaa kwamba Korea Kaskazini huenda inajiandaa kufanya jaribio la nne ya zana zake za nukyla.
Inatarajiwa kwamba shughuli mpya katika kinu cha nuklya mjini Pyongyang zitatawala mazungumzo kati ya bwana Obama na rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.
Viongozi hao wawili wanarajiwa kuangazia zaidi jukumu la Uchina katika kuithibiti Korea Kaskazini, jambo ambalo Bwana Obama ametaja kuwa lenye umuhimu mkubwa.
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili Korea Kusini katika sehemu yake ya pili ya ziara katika Bara la Asia. Anatarajiwa kukutana na Rais Park baadaye leo na kuwatembelea wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo.
Ziara yake inafanywa wakati ambapo kuna hofu kuwa Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio la nne la Kinukilia.
Korea Kaskazini inatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao wawili na tayari kuna ripoti kuwa maandalizi ya kufanya jaribio la Kinukilia yanayoendelea kufanywa Korea Kaskazini yatahakikisha kuwa taifa hilo jirani linapewa kipao mbele katika mashauriano.
Picha zilizochukuliwa na mitambo ya Sattelite zinaonyesha kuwa kuna masanduku mengi yanayohamishwa hapa na pale katika eneo linalotarajiwa kufanyiwa zoezi hilo Korea Kaskazini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

KERRY ASHUTUMU URUSI KWA GHASIA UKRAINE

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John Kerry akizungumza na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amelaumu Urusi kwa kuchochea mapigano Mashariki mwa Ukraine.
John Kerry alisema ujasusi wa Marekani una hakika kuwa Urusi imetoa silaha na wapiganaji na pia inaendelea kugharamia na kusimamia wapiganaji wa nchini Ukraine kushiriki ghasia hizo.
Katika lugha ya hasira, Bwana Kerry, alishambulia Urusi akisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua madhubuti za kujaribu kutuliza uhasama ulioko nchini Ukraine kama ilivyokubaliwa mjini Geneva juma lililopita.
Bwana Kerry alisema kuwa Urusi inasimamia ghasia zinazoendeshwa na watu wanaotaka kujitenga kutoka kwa Ukraine Mashariki mwa taifa hilo na kujaribu kusababisha ghasia ili kuhujumu uchaguzi unaotazamiwa kufanywa mwezi ujao.
Kwa hasira, Bwana Kerry alilaumu Urusi kwa ghasia zote zinazoendelea Ukraine wakati huu. Ingawa hakutangaza vikwazo inavyoweza kuongezewa Urusi Bwana Kerry alisema mwanya wa kuimarisha amani katika Ukraine unaendelea kuziba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Thursday, April 24, 2014

KOCHA MPYA WA TAIFA STARS KUWASILI JUMAMOSI APRIL 26.

KOCHA

Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mart Nooij ni raia wa Uholanzi, na ameshawahi kufanya kazi katika nchi ya Mozambique kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Burkina Faso U20, na pia ameifundisha timu ya Santos ya Afrika ya Kusini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea nchini Mhe Chung IL wakiwa mbele ya mchoro wa mfano wa Hospitali ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na msanii Mrisho Mpoto baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL na viongozi wengine  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam, April 24, 2014. (PICHA NA IKULU)
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...