SHUKURU KAWAMBWA |
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema kuendeleza mjadala huo ni kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete alishamaliza kazi yake.
Rweyemamu alisema Rais ndiye mwenye
mamlaka ya kuteua mawaziri ambao wana wajibu wa kumsaidia katika
utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si sahihi wateule hao kuitwa
'mizigo' kwani yeye (Rais) ameona wanafaa.
"Rais anapoteua watu anaangalia wanaofaa kumsaidia na si vinginevyo. Kwani lengo lake ni kuona nchi ina 'move forward' (inasonga mbele) kimaendeleo," alisema Rweyemamu. Alisema watu wanapaswa kukumbuka kuwa mtu anapoteuliwa kwenye uwaziri kuna suala la uwajibikaji: "Anatakiwa kutekeleza uwajibikaji wa pamoja. Sasa kumshambulia mtu binafsi na kumwita mzigo siyo sahihi."
Rweyemamu alisema mjadala huo kwa sasa umepitwa na wakati na kuwataka wananchi na wachambuzi kuwaacha mawaziri hao kuchapa kazi.
"Ni vizuri wananchi wakawapa nafasi mawaziri hawa ya kufanya kazi na baadaye kuwapima na kuwachambua kutokana na utendaji wao," alisema.
Chimbuko la majadala
Mjadala kuhusu suala hilo unatokana na Rais Kikwete kuwarejesha katika Baraza la Mawaziri baadhi ya mawaziri ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu katika utendaji wao.