Balozi Ombeni Sefue
********
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema, jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshawasilisha mapendekezo yao ya majina takribani 5, 400, Ikulu.
Kuhusu kutaja baadhi ya majina ambayo asasi hizo zimeyependekeza kwenda Ikulu, Balozi Sefue, alisema ofisi hiyo haina ruhusa ya kufanya hivyo labda asasi zenyewe ziamue kufanya hivyo kupitia vyombo vya habari.
“Jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshaleta majina ya watu 5, 400 zilizoyapendekeza. Mapendekezo yaliyoletwa ni mengi, kwani katika idadi hii, wanaotakiwa ni 2001, hivyo kazi ipo,” alisema na kuongeza:
“Kuhusu majina yaliyopendekezwa, hatuna ruhusa ya kufanya hivyo, labda kwa ridhaa yao wenyewe wanaweza kutangaza kwenye vyombo vya habari. Na sasa kazi tunayoendelea nayo ni uchambuzi wa majina hayo ili tumpelekee Rais, ambaye ndiye atakayejua watakaopaswa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba.”