NCHINI
Afrika Kusini, hakuna eneo la kivutio cha kitalii linalotembelewa na
wageni wengi kama Kisiwa cha Robben. Umaarufu wa eneo hili umekuwa
ukiongezeka mwaka mpaka mwaka.
Lakini
hakuna shaka kwamba, kiini cha kutembelewa sana kwa kisiwa hiki ni
kutoka na kuwa kituo maalumu cha kuwafunga wapigania uhuru wa Afrika
Kusini wakati huo, akiwamo Nelson Mandela.
Mandela,
Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika Kusini, ndiye mhimili wa kivutio
cha utalii kwenye jela ya wafungwa wa kisiasa iliyojengwa ndani ya
kisiwa hicho.
Kati
ya wafungwa wengi wa kisiasa waliowahi kufungwa kwenye jela ya Robben,
alikuwamo Govan Mbeki, baba mzazi wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini
aliyempokea madaraka Mandela, Thabo Mbeki. Ni Mandela pekee ndiye
aliyekaa hapo muda mrefu.