Rais
Jacob Zuma ametangaza kwamba mazishi ya Nelson
Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu,
katika jimbo la Eastern Cape.
Rais
Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera
zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku
ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya
maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari
msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata
dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinto
na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao
wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili
wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia
Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa
kijijini Qunu kwa mazishi
Uwanja
wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa ya
mazishi itafanyika siku ya Jumapili ya Desemba 10, 2013
Jengo la Union Buildinga ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi
mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako
atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.