Ni miaka kumi na nne sasa imepita tangu mzee wetu mpendwa baba wa taifa hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aiage dunia.
Mwalimu Nyerere ni Rais wa kwanza na ni
muasisi aliyeliletea taifa hili uhuru wa kweli toka katika makucha ya
mkoloni 9 December, 1961. Mwalimu Nyerere alizaliwa April 22, 1922
katika kijiji kidogo cha mwitongo huko Butihama, kasikazini mwa Tanzania
karibu kabisa na ziwa Victoria .
Alikuwa ni mototo wa chifu Burito
Nyerere wa kabila dogo la wazanaki
Nyerere alifariki dunia kwa
ugonjwa wa kansa ya damu, siku ya Alhamisi Oktoba 14, 1999 saa 4:30
asubuhi [kwa saa za Afrika Mashariki], katika hospitali ya Mtakatifu
Thomas London, Uingereza akiwa amezungukwa na timu ya madaktari bingwa.
Ndipo wananchi wote tulipigwa na butwaa kwa kumpoteza kiongozi mwenye
msimamo thabiti na busara duniani.
Mwalimu bado ni taa inayong’aa
gizani, umuhimu wake nazidi kuonekana kadiri miaka inavyokwenda licha ya
kwanza amekwisha tuacha.
Wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere
alichukia na kukemea vikali mambo yasiyofaa kwa mustakabali wa maendeleo
ya Tanzania , Afrika na Dunia kwa ujumla. Baadhi ya mambo hayo ni:
1. UJINGA
Mwalimu Nyerere alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache na ni mtanzania
wa kwanza kupata nafasi yamasomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Edinburg ,
Uingereza na kuhitimu mwaka 1952 akiwa ni gwiji wa uchumi na historia.
Mwalimu hakupenda ujinga na hivyo alipigana vita kali dhidi ya ujinga,
na alifanikiwa kwa nafasi yake kuwaondoa ujinga watanzania wengi,
wakiwemo viongozi wetu wa sasa ambao walisomeshwa ‘bure’ katika
mazingira mazuri yakuridhisha kwa manufaa ya nchi yetu. Ndiyo maana Rais
Kikwete Februari 3, 2007 alisema “….sisi tuliwekezwa na ni lazima
tuwekeze kwenu ili miaka 30 ijayo Rais atoke miongoni mwenu….”