SHERIA imewatia hatiani viongozi 4 kati ya 5 wa kampuni
ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI)
iliyokuwa ikijihusisha na shughuli za kuvuna na kupanda fedha nchini
kinyume cha sheria.
Hayo
yalibainika hii leo wakati wa hukumu ya kesi hiyo iliyodumu kwa miaka
kadhaa huku mtuhumiwa mmoja katika kesi hiyo akiachiw huru baada ya
upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.
Akisoma
hukumu hiyo iliyo andikwa na Hakimu Mwenzake, Stuart Sanga, Hakimu wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Aloyce Katemana
alitafsiri sheria kadhaa zilizowatia hatiani watuhumiwa hao.
Vigogo
hao waliotiwa hatiani ni pamoja na Jackson Sifael Mtares, Dominick
Kigendi, Timotheo Saigaran ole Loitginye, Samwel Sifael Mtares,Samwel
Mtalis huku sheria ikimwachia huru Arbogast Francis Kipilimba baada ya
kushindwa kumtia hatiani.