Sunday, July 21, 2013
MAKUBWA ETI.... "HAKUNA MFANYABIASHARA MKUBWA NCHINI ALIYEFANIKIWA BILA KUTOA RUSHWA SERIKALINI".... REGINALD MENGI
MWENYEKITI wa kampuni za IPP, Reginald Mengi ametoboa siri kuwa hakuna mfanyabiashara wa Tanzania aliyefanikiwa katika biashara kubwa kwa kusaidiwa na serikali bila ya kutoa rushwa.
Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), alisema yeye aligoma kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali jambo lililosababisha kupoteza fursa nyingi ambazo zingemfanya awe na maendeleo zaidi ya aliyonayo hivi sasa.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada katika uzinduzi wa ripoti ya uchumi na maendeleo barani Afrika kwa mwaka 2013, ...tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku upate hacari... uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Diplomasia. Alisema kutokanana na kukithiri huko kwa rushwa, maendeleo ya kibiashara na kijamii hapa nchini hayawezi kufikiwa kama jitihada za kupambana na rushwa zitapuuzwa.
Saturday, July 20, 2013
AJALI MBAYA: KICHWA CHA MWANAMKE CHANASA KWENYE KIOO...!!!
Wakimtoa Dereva kwanza |
Wakianza kumuokoa yeye |
Hatimaye ameokolewa |
Juhudi za ziada zilifanywa na askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa kukitanua kioo hicho kwa ustaadi mkubwa huku wakihakikisha hawamkati zaidi mwanamke huyo.
KIKOSI CHA WAASI NCHINI KONGO M23 CHAWEKA PICHA YA PASSPORT YA ASKARI WA JWTZ WALIYEMKAMATA ASUBUHI YA LEO AKISHIRIKIANA NA FDLR
Waasi wa M23 wa DR Congo, wanadai kuwa wamemkamata askari wa Tanzania anayeitwa Christopher George Yohana, wakati akishirikiana na waasi wa Rwanda (FDLR) wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya maelfu ya Watusi mwaka 1994.
Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com, M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo ya Passport Juu hapo:“Leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”
WASTARA JUMA .... "WANAUME WALIO MSAIDIA SAJUKI WAMENIGEUKIA NA KUNITAKA KIMAPENZI"
Wastara Juma amefunguka kuwa wanaume wengi waliokuwa wakimsaidia wakati mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa mgonjwa wanamgeuka na sasa wanamtaka kimapenzi.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Take-One katika Runinga ya Clouds chini ya Zamaradi Mketema, Wastara alisema baadhi ya watu ambao walikuwa karibu naye wakati Sajuki anaumwa sasa hivi wamegeuka na kumtaka kimapenzi, jambo ambalo linamuumiza na kumshangaza mno.
Bishosti huyo alisema kuwa tofauti na wanaume hao ambao walikuwa wakimpa sapoti kipindi hicho, bado wapo wengine kibao kutoka nje na ndani ya nchi ambao wanatuma maombi kwake lakini anawaona wote ni matapeli na wanamtamani tu hivyo hayupo tayari kuingia kwenye uhusiano wa aina hiyo.
ANGALIA PICHA ZAIDI ZA MAPOKEZI YA MIILI YA MASHUJAA WA TANZANIA WALIOUAWA DARFUR ILIVYOPOKELEWA LEO JIJINI DAR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na
viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani,
waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa
ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo
jioni.
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur
nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla.
Miili
hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa
kumi.
"HAKUNA UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA" NAPE NNAUYE
Nape Nnauye |
MKURUGENZI WA Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye
amesema suala la uchaguzi wa Meya wa Mji wa Arusha limefikia tamati na
kamwe uchaguzi huo hautafanyika tena. Nnauye alisema hayo alipozungumza
na MTANZANIA jana, huku akiwataka wananchi wa Jiji la Arusha kupuuza
kauli za vitisho zinazotishia kumwondoa madarakani Meya wa Jiji,
Gaudence Lyimo.
Kauli ya Nnauye inafuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Arusha Isaya Doita, aliyesema kuwa ushindi wa udiwani wa chama chao katika kata nne za mji huo ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe.
Doita akiamini kuwa Lyimo alichaguliwa kwa mizengwe, alisema ana imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.
Hata hivyo, siku chache baadaye Katibu wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema suala la nafasi ya umeya siyo tena ajenda ya chama hicho.
Akizungumzia suala hilo jana, Nnauye alisema CCM imezoea kusikia kauli mbalimbali za vitisho zinazotolewa Chadema na kuwataka wananchi wa Arusha kuzipuuza kauli hizo.
“Ni kazi yao vitisho nia yao ni kutaka watu wasifanye shughuli zao, lakini suala la meya yupo pale na ataendelea kuwapo kwani uchaguzi ulishafanyika na hautafanyika tena.
“Kazi iliyobaki sasa kwa wananchi wa Arusha ni kujenga mji wao kwa kufanya kazi, watu wafanye kazi zao wala hakuna sababu ya kuhofia kauli za vitisho.
“Ni upuuzi kuanza kuzungumzia kila siku suala la Arusha, waliopewa dhamana wawajibike kilichobaki ni kufanya kazi, waache kusikiliza upuuzi,” alisema Nnauye.
CHANZO MTANZANIA
Kauli ya Nnauye inafuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema Arusha Isaya Doita, aliyesema kuwa ushindi wa udiwani wa chama chao katika kata nne za mji huo ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe.
Doita akiamini kuwa Lyimo alichaguliwa kwa mizengwe, alisema ana imani muda si mrefu Jiji la Arusha litapata meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.
Hata hivyo, siku chache baadaye Katibu wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema suala la nafasi ya umeya siyo tena ajenda ya chama hicho.
Akizungumzia suala hilo jana, Nnauye alisema CCM imezoea kusikia kauli mbalimbali za vitisho zinazotolewa Chadema na kuwataka wananchi wa Arusha kuzipuuza kauli hizo.
“Ni kazi yao vitisho nia yao ni kutaka watu wasifanye shughuli zao, lakini suala la meya yupo pale na ataendelea kuwapo kwani uchaguzi ulishafanyika na hautafanyika tena.
“Kazi iliyobaki sasa kwa wananchi wa Arusha ni kujenga mji wao kwa kufanya kazi, watu wafanye kazi zao wala hakuna sababu ya kuhofia kauli za vitisho.
“Ni upuuzi kuanza kuzungumzia kila siku suala la Arusha, waliopewa dhamana wawajibike kilichobaki ni kufanya kazi, waache kusikiliza upuuzi,” alisema Nnauye.
CHANZO MTANZANIA
KOCHA MZUNGU TAIFA STARS AFARIKI DUNIA JANA
Tumempoteza: Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89 jana.
Na Mahmoud Zubeiry na Chris Wheeler,
KOCHA
wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na giwji wa
zamani wa klabu ya Manchester City, Mjerumani Bert Trautmann amefariki
dunia leo akiwa na umri wa miaka 89.
Baada
ya BIN ZUBEIRY kusoma taarifa za kifo cha kocha huyo Daily Mail,
ilimpigia Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Leodegar Chilla Tenga
ambaye alifundishwa na Mjerumani huyo na akasikitisha.
Tenga, ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema kwamba Trautmann, ambaye alikuwa anasumbuliwa alikuwa mwalimu mzuri na wachezaji walimpenda sana.
Alisema
kocha huyo aliyefariki asubuhi ya leo nyumbani kwake, La Losa, karibu
na Valencia aliifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 1975 na 1976.
“Alikuwa
kocha mzuri, kwa sababu ni kocha aliyetokea kuwa mchezaji wa kulipwa,
alikuwa anaelewa saikolojia ya wachezaji, na alikuwa mwalimu ambaye
ukienda kambini unaona raha kuwa kambini.
MAAJABU:MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI TENA KWA MAUMIVU MAKALI
Hayo ndio yaliyojiri Alhamisi ya jana tarehe 18 July 2013 Huku katika Jimbo la Irolini Kwara, Nigeria. Hata hivyo mbuzi huyo alizaliwa na vichwa viwili alifariki saa chache baadae
Friday, July 19, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA PROFESA LIPUMBA KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha
Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu
jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo
hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais
Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika mazungumzo yao yaliyofanyika
Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Kikwete, akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao jana. Picha na Fredy Maro
MNYIKA AANIKA NAMBA ZA MAWAZIRI KWA UMMA...!!!
Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.
Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.
Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.
WEMA SEPETU KUOZEA JELA, ALICHOKIFANYA SAFARI HII....!!!
KUNA kila dalili kwamba mrembo anayetamba kwenye filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au Madam jela inamwita na anatakiwa kufanya maombi ili kukwepa kifungo maishani mwake.
Hali hiyo inafuatia staa huyo kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena Jumatano iliyopita, pale alipopanda katika Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar kwa kosa la kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni meneja wa hoteli moja iliyopo Kawe Beach jijini Dar, Godluck Kayumbu.
Kabla ya kupandishwa kwa ‘pilato’, staa huyo anayemiliki Kampuni ya Endless Fame alikuwa akisakwa na askari kwa siku kadhaa na kufanikiwa kuwapiga chenga za hapa na pale.
ANASWA AKIFUTURU
Hata hivyo, mbio zake ziliishia ukingoni Julai 16, mwaka huu, alipokamatwa saa mbili usiku akiwa anafuturu na wageni wake nyumbani kwake, Kijitonyama Dar.
MTITI KIDOGO
Askari saba walifika nyumbani kwake wakiwa ndani ya Land Rover ‘difenda’ kwa ajili ya kumkamata, hata hivyo walipata upinzani kidogo kutoka kwa mlinzi wa staa huyo ambaye alikuwa akizuia bosi wake asikamatwe ambapo ilibidi askari hao wakaze msuli na kutuliza mtiti uliokuwa ukitaka kutokea.
MZEE WA MIAKA 63 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA MSICHANA WA MIAKA 16 NDANI YA MSIKITI...!!!
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemhukumu Ahamad Fadhil (63), kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 ndani ya Msikiti wa ni Mwembe Mmoja, mjini hapa.
Hukumu hiyo ilitolewa na jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Obadiah Bwegoge, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.
Hakimu Bwegoge alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia ya kikatili kama yake.
Alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi watano ambao bila kuacha shaka, walithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Alisema shahidi wa kwanza upande wa Jamhuri ambaye ni mlalamikaji, alidai kuwa siku ya tukio, saa nane 8:00 mchana, alikwenda msikitini hapo kuomba msaada kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
SERIKALI YASISITIZA KUWA "KODI YA LINE ZA SIMU" IKO PALE PALE...!!!
Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.
Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.
Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko.
Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.
Subscribe to:
Posts (Atom)