Thursday, June 06, 2013

MTANZANIA KUONGOZA JESHI LA KULINDA AMANI DARFUR.

 
 
Kwa mara nyingine  Bendera ya  Tanzania imeendelea kupepea katika Tasnia ya Ulinzi wa Amani  ya Kimataifa.
 Mapema wiki hii,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bi. Nkosizana Dlamin Zuma wametangaza uteuzi wa Luteni General Paul Ignace Mella  Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) kuwa Mkuu  Mpya wa Jeshi la   Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa huko Darfur ( UNAMID)
 
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki Moon, na nakala yake kutumwa  katika  Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  imeeleza kwamba, Lt. Gen. Mella anachukua  nafasi iliyoachwa na Mkuu wa  zamani wa Jeshi hilo (UNAMID), Lt. Gen Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amemaliza muda wake wa  utumishi  March 31,2013.
 
Wasifu wa Luteni General Paul Ignace Mella unaelezwa  kuwa ni Mwanajeshi wa muda mrefu na  mwenye uzoefu na utumishi uliotukuka katika JWTZ akiwa amewahi kushika nyadhifa  mbali mbali  muhimu za uongozi.
Baadhi ya nyadhifa hizo ni pamoja na  Naibu Kamanda Kikosi cha Tanzania chini ya Umoja wa Mataifa huko Liberia (  1993-95), Kamanda wa Kikosi cha  JWTZ, Afisa Mnadhimu-Makao Makuu  ya Jeshi, Mwambata Jeshi-Ubalozi wa Tanzania Uganda na hadi sasa alikuwa ni  Mkuu wa Usalama na Utambuzi- JWTZ.
 Uteuzi wa Lt. Generali Mella unafuatia mchakato mrefu ulioshindanisha wateuliwa kutoka nchi mbalimbali duniani, na hatimaye  yeyé akaibuka mshindi. 
OFISI YA UBALOZI WA TZ UN

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 06, 2013



6 f55a81 37d70

Wednesday, June 05, 2013

MPYA KUHUSU BINTI WA KITANZANIA ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NA KUHUKUMIWA KUNYONGWA IJUMAA HII

Hii ndio picha ambayo imesambaa kwenye mitandao mingi ya msichana anesemekana ni Fatma aka Brown Berry wa Ilala Dar es Salaam ambae amehukumiwa kunyongwa huko egypt baada ya kukamatwa na unga.
Hii ni screenshot ya video hii hapa chini baada ya kukamatwa kwake na unga, Ingawa habari hizi hatuna uhakika nazo kama ni Mtanzania kama invyodaiwa na wengi au ni mswahili wa Oman kama wengine wanavyodai
Mrembo Fatma aka Brown Berry katika pose

MR NICE APIGWA CHINI NA LABEL ALIYOKUA AKIFANYA NAYO KAZI KENYA, KISA NI MVIVU.

GrandPa Records Ya Kenya Imevunja Mkataba Wake Wa kazi na Msanii Mr Nice kutoka Tanzania Baada ya miezi michache ya kufanya nae kazi. Fahamu Mr Nice alipewa mkataba na GrandPa Records huku akijua kuwa ana mkataba mwingine Tanzania na Producer Lamar. GrandPa Wamesema Mr Nice Ni Msanii Mvivu na Asiye toa ushirikiano kwenye kazi kabisa ndio maana wameamua Kuvunja mkataba wake. Hii Ni Post ya FaceBook Ya GrandPa Records. Bado Taarifa Zina Kuja Kaa Na Mimi Utaiskia Interview Yao Hapa Soon


TO

KESI DHIDI YA RUTO KUHAMISHIWA KENYA AU TANZANIA

 Nairobi, Kenya. Kesi inayomkabili makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huenda ikahamishiwa nchini Tanzani au Kenya.
Hiyo inatokana na uamuzi unaotajwa kufikiwa na majaji wa ICC ambao wametoa mapendekezo wakimtaka Rais wa ICC aangalie umuhimu na kutoa ruhusa ya kesi hiyo kusikiliziwa nchini Kenya au kama ikishindikana basi isikiliziwe nchini Tanzania.
Uamuzi huo unaweza pia kusababisha athari za kuichochea mahakama hiyo kuhamisha pia kesi ya aina hiyo inayomhusu Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia mawakili wake wameomba kesi dhidi yake ihamishiwe nchini Kenya au Tanzania.
Ruto pamoja na mtuhumiwa mwenzake, aliyekuwa mtangazaji wa Redio, Joshua Arap Sang wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu wakidaiwa kuhusika kuchochea vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 zilizosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.
Mapendekezo hayo yametokana na ombi hilo lililotumwa Januari 24 mwaka huu ambalo lilikuwa bado likiendelea kujadiliwa n amamlaka zinazohusika kwenye mahakama hiyo.
Februari mwaka huu, Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Fatou Bensouda aliieleza mahakama hiyo kwamba hana pingamizi iwapo itakubalika kesi hiyo isikiliziwe Tanzania au Kenya.
Hata hivyo mahakama hiyo ilieleza kuwa mapendekezo hayo bado yanaendelea kujadiliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na mahakama hiyo.
Hata hivyo, jana ICC ilitoa taarifa ikisema kesi dhidi ya Ruto anayetuhumiwa kufanya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu itaanza Septemba 10 mwaka huu.
Taarifa hiyo imesema majaji wameamua kupanga tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo mapema zaidi kuliko ilivyopangwa awali.
Rais Kenyatta na naibu wake wanahitajika kupandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka yanayowakabili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, makosa ambayo waliyafanya wakati wa vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Rais wa mwaka 2007/08.

"SITANYAMAZA KUSHAMBULIWA KWANGU.NI LAZIMA JAMII IJUE"...HII NI KAULI YA KIBANDA BAADA YA KURUDU TANZANIA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (wa tatu kulia) akiwasili jana.
 
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda amerejea chini jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na kusisitiza kwamba hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kibanda alisema asingependa kuona jambo hilo linamtokea mwandishi mwingine wa habari.

Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka huu.

Azam yawatupia virago Babi, Uhuru



Abdi Kassim ‘Babi’

Dar es Salaam. Azam FC imetoa mkono wa kwa heri kwa kiungo wake mkongwe Abdi Kassim ‘Babi’ na Uhuru Seleiman aliyekuwa kwa mkopo. Meneja wa timu hiyo, Patrick Kahemela alisema jana kuwa sababu kubwa ya kuachana na wachezaji hao ni mikataba yao kumalizika pamoja na umri kuwatupa mikono.

Wachezaji waliotupia virago ni pamoja na Lewis Cosmas aliyejiunga na Ruvu Shooting na Abdulhalim Humoud aliyepata timu Afrika Kusini ya Jomo Cosmos. Akizungumza na gazeti hili Abdi Kassim alisema “Ni kweli mkataba wangu kuitumikia Azam umeisha ingawa walinitaka nisaini mpya, lakini tukashindwa kuafikiana. “Naamini bado nina nguvu na uwezo wa kucheza soka. Kwa hiyo niko tayari kujiunga na timu yoyote ambayo itaonyesha nia ya kunitaka.” alisema Babi aliyekipiga na klabu za Mlandege ya Zanzibar, Mtibwa Sugar, Yanga, DT Long ya Vietnam pamoja na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.
Anaeleza kuwa yuko tayari kujiunga na Yanga, Mtibwa Sugar ama Coastal Union iwapo zitaonyesha kutaka kumsajili kwa ajili ya msimu ujao. Klabu ya Mtibwa iliwahi kukiri kutaka kumrejesha Babi nyumbani katika dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu.

RONALDO AGOMA KUONGOEZA MKATABA REAL MADIRD

ronaldo 7d195

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo ameziweka kiporo Manchester United na Paris Saint-Germain baada ya kusema hataongeza Mkataba Real Madrid baada ya 2015.Real imegoma kumuuza Mreno huyo msimu huu wakati United na PSG zinabakiwa mstari wa mbele atakapotiwa sokoni.Alex Ferguson alimuuza Ronaldo kwenda Madrid mwaka 2009, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ameeleza mara kadhaa hivi karibuni kwamba hana furaha sana katika Jiji hilo na Hispania.
Rais wa Madrid, Florentino Perez alisema anatarajia kuona Ronaldo akitungikia daluga zake katika klabu hiyo, lakini inaonekana atatafuta klabu nyingine miaka miwili ijayo.
Ikiwa Ronaldo atakuwa mkweli kwa kauli zake, ataondoka bure, kitu ambacho Madrid hawatapenda baada ya kumsajili kwa Pauni Milioni 80.

DIAMOND ANA UTAJIRI WA ZAIDI YA BILIONI 1 ZA BONGO, NA HAYA NDIO MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND


1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.

3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.
4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.
6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.
7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.
8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.
9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.
10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.
 
d8fdca7eccf211e2a7ed22000a1f8f24_7

ANGALIA PICHA ZA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ALBERT MANGWEA ZAANZA KUTOLEWA.

Dah this is it ndugu yetu mpendendwa ndo ametangulia mbele za haki na sasa ule muda wa kutoa heshima za mwisho ndo umewadia. Mungu awape nguvu wale wote waliofikwa na msiba huu.


Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 5, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

1 c5c24


2 c0794

Tuesday, June 04, 2013

Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake

Hivi karibuni Diamond aliamua kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye msichana katika maisha yake aliyemkosea sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.

Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.

“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amesema Jokate.

MAPOKEZI YA MANGWEA JIJI ZIMA LAZIZIMA

 Gari iliyobeba mwili wa Albert Mangwea ikisukumwa na washabiki,wapenzi ndugu jamaa na marafiki mara baada kuanza kuondoka eneo la Eapoti hivi punde wakielekea Muhimbili kwa taratibu nyingine,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi--Amen

ANGALIA PICHA MWILI WA ALBERT MANGWEA ULIVYOWASILI DAR

Gari maalum la Kubeba Mwili wa Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Marehemu Albert Mangwea likiwa tayari  kwa kubeba mwili.
Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Wadau kibao wapo uwanjani hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.
Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya habari uwanjani hapa.

ANGALIA PICHA ZA MWANAMKE AZAA WATOTO WATANO KWA MPIGO NCHINI CZECH.

Mmoja wa watoto wa watano akiwa amejifungua mbele ya uangalizi wa jopo la madaktari siku ya jumapili nchini Czech.
Jopo la madaktari wakimchunguza mwanamke Alexandra Kinova miaka 23.
Alexandra Kinova kipindi cha ujauzito.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...