WAKATI kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred
Lwakatare ikitarajiwa kusikilizwa leo Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura
(Lady JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama
ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kesi hizo zinatarajia kuvuta hisia za watanzania kutokana na mvuto na aina ya kesi hizo,Lwakatale atapanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili awali na kubaki na shitaka la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika.

Kwa
upande wa Lady JayDee anatarajia kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza
baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo
kesho mei 27 .
Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.