Sunday, May 26, 2013

MAPACHA WATANO WALIOZALIWA WAKATI MMOJA WAFARIKI DUNIA

 Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano  kitandani baada ya kujifungua
...............................................................................
Na Nathan Mtega,Songea

 WATOTO watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma wamefariki dunia baada ya kuishi hai kwa muda wa masaa kumi.
 Akizungumza kwa njia  ya simu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza alisema kuwa watoto hao watano ambao walizaliwa kwa njia ya upasuaji wakiwa na umri wa miezi nane tofauti na inavyotakiwa  umri wa mtoto kuzaliwa kuwa ni miezi tisa.
 Alisema kuwa watoto hao mara baada ya kuzaliwa Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi walikuwa wakiendelea vizuri ingawa wote walikuwa na uzito mdogo huku mwenye uzito mkubwa akiwa na gramu 730 na mwenye uzito mdogo akiwa na gramu 430 na kitendo cha kuzaliwa kabla ya muda stahili wa mtoto kuzaliwa kimechangia watoto hao kufariki majira ya saa 3 usiku hospitalin hapo.
 Watoto hao wamezikwa katika makaburi yaliyopo eneo la Lilambo mjini Songea na kushuhudiwa zaidi na baadhi ya wanawake huku baadjhi ya wadau wakiwemo viongozi wa serikali wakijipanga namna ya kuwasaidia watoto hao kwa sababu mama yao ni mwajiriwa mpya wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi katika shule ya sekondari Luhawasi iliyopo mjini Songea.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...