Monday, May 27, 2013
ANGALIA PICHA ZA LULU ANAVYOZIDI KUWA NA MVUTO
Muigizaji wa kike aliyekulia kwenye tasnia ya bongo movie,
kwa kuwa alianza tangu akiwa mdogo na hadi sasa kipaji chake kinazidi kung’aa.
Haishii kung’arisha kipaji chake tu bali anazidi kuwa na muonekano wenye mvuto
pia.
Lulu anaonekana hana stress tena kama ilivyokuwa siku kadhaa
zilizopita alipokuwa chini ya ulinzi mkali akituhumiwa kusababisha kifo cha
muigizaji mwenzake Steven Kanumba.
Huu ndio muonekano wa Lulu sasa hivi:
Sunday, May 26, 2013
MULUGO NA WANAFUNZI WANAOMILIKI SIMU
NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema atafanya
ziara katika shule zote za msingi na sekondari ili kuwabaini wanafunzi
wanaotumia simu za mkononi shuleni.
Mulugo alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizindua mpango mkakati wa elimu ya haki za binadamu na kuongeza ataanzia Mkoa wa Dodoma na atakaowabaini atawanyang’anya na kuzichoma moto.
Alisema suala la utandawazi limechangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuharibika na kuwa na nidhamu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuwadharau walimu na wazazi.
Mulugo alisema kitendo cha wanafunzi kwenda na simu shuleni kimesababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili, ambapo pia kimechangiwa na baadhi ya wazazi kujifanya wanawapenda watoto wao: “Hivi sasa limekuwa ni jambo la kawaida kuwakuta wanafunzi wa ngazi zote wakiwa na simu shuleni. Mimi sikubaliani nalo, nimeamua nitafanya

ziara
shule moja baada ya nyingine nikimkagua mwanafunzi mmoja baada ya
mwingine nikianzia na Mkoa wa Dodoma katika kipindi hiki cha Bunge. Ole
wake mwanafunzi nitakayemkuta na simu nitamnyang’anya na kuichoma moto
maana walimu wanawalea sana… halafu na mimi mniimbie ‘tunataka haki
zetu’,” alisema Mulugo.
RAIS NKURUNZIZA WA BURUNDI AJA KUHUBIRI INJILI TANZANIA
Rais Pierre Nkurunziza. |
Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunziza, anatarajiwa kuja nchini Agosti, kuhubiri
Injili katika mkutano mkubwa wa Injili unaoandaliwa na Baraza la
Makanisa ya Kipentekoste nchini (PCT), imefahamika.
Kwa
mujibu wa Askofu Samson Mlawi aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi
mwishoni mwa wiki, tayari Kamati ya Maandalizi imefanya vikao kadhaa
ambavyo pamoja na mambo mengine, kamati ndogo zimeundwa ili kurahisisha
ujio wa Rais huyo.
Alisema,
kwa kutambua umuhimu na uzito wa ujio huo katika shughuli hiyo ya
kiroho, kamati imeweka mtandao wa mawasiliano kuhakikisha waumini wa
madhehebu hayo kutoka mikoa mbalimbali wanahudhuria mkutano huo ambao
bado unatafutiwa uwanja.
Askofu
huyo alisema Rais Nkurunziza pamoja na mambo mengine, anatarajiwa
kuleta ujumbe wa amani na uvumilivu wa kidini hususan katika kipindi
hiki cha mpito baina ya madhehebu ya Kikristo na Waislamu nchini.
“Mimi
na wanakamati wenzangu, tunaamini Mungu atafanya kazi yake kupitia Rais
kuhubiri Habari Njema kwa Watanzania kama ambavyo angehubiri mtu
mwingine yeyote, lakini kutokana na nafasi yake ni matumaini yetu kwamba
ujumbe huo utachukuliwa kwa uzito wa kipekee,” alisema.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa Askofu, mwezi huo huo wa Agosti, Mwinjilisti wa
Kimataifa wa Huduma ya Christ For All Nations (CFaN), Reinhard Bonkke
anatarajiwa kuwasili nchini kwa ujumbe maalumu kwa waumini wa madhehebu
ya Kikristo na Taifa kwa ujumla.
Alisema,
ujio wa wageni hao mashuhuri nchini, utasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza shaka na wasiwasi kwa baadhi ya Wakristo ambao wako njia panda
kuhusu masuala muhimu ya kiimani, ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.
WANASHERIA WAAPA KUWASHITAKI WASANII WA KUNDI LA ZE KOMEDY KWA KUPIGA PICHA ZA UTUPU...!!
Zile
picha za kundi la Ze Komedy la linalorusha kipindi chake kupitia
televisheni ya East Africa TV zinazowaonesha wasanii hao wakiwa na
mabint ufukweni zimechukua sura mpya baada ya wanasheria kuahidi kuzisaidia familia za wazaza wa mabint hao.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema" Nimeziona picha hizo kupitia mtandao wenu kweli imeniuma kama mzazi kwani huo ni unyanyasaji ambao haukubariki hata kidogo naziomba familia za mabint hao kuchukuwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kushtaki ili iwe fundisho kwa wasanii wengine wanaopenda kudhalilisha watu wengine kwa masrahi yao binafsi" Alisema Fortunatus Kasomfi ambae ni mtanzania anaeishi nchini Afrika Kusini
Aidha nae Hawamu Juma ambae ni mkazi wa Arusha maeneo ya Unga Limited ambae ni Mwanasheria maarufu Mkoani humo alioneshwa kusikitishwa sana na tukio na kuwashauri wazazi wa wasichana hao kumtafuta kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka wasanii hao

"
Napenda kuwashauri wazazi wa wabinti hao kama wanahitaji msaada wa
kisheria wanitafute kupitia simu namba 0713-146416 nitawapa mawazo ya
kitaalam ya kisheria ili wasanii hao wafikishwe mahakamani" Alisema Mwanasheria huyo.
MAPACHA WATANO WALIOZALIWA WAKATI MMOJA WAFARIKI DUNIA
Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano kitandani baada ya kujifungua
...............................................................................
Na Nathan Mtega,Songea
WATOTO
watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la
Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma wamefariki
dunia baada ya kuishi hai kwa muda wa masaa kumi.
Akizungumza
kwa njia ya simu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza alisema kuwa watoto hao watano ambao
walizaliwa kwa njia ya upasuaji wakiwa na umri wa miezi nane tofauti na
inavyotakiwa umri wa mtoto kuzaliwa kuwa ni miezi tisa.
DIAMOND ATOA SIRI YA MUZIKI WAKE....!!!
Mengi
yamekuwa yakisemwa juu ya msanii ambae inaaminika ndiye mfalme wa
muziki wa bongo fleva Wapo wanaosema anatumia nguvu za giza ikiwemo
ushirikina na wapo wanaosema yuko powered na Imani ya Free mason ingawa
TEENTZ tunaamini juhudi na kujituma ndiyo njia pekee ya mafanikio kwa
chochote TEENTZ ilipiga story na Diamond na kueleza moja ya sababu kubwa
why yuko juu na na kila siku ananendelea kuwa juu tofauti na baadhi ya
wanamzki wengine
1-"Mungu ndio kila kitu kwa maisha ya binadamu,so napenda kumtanguliza Mungu kwa kila nikifanyacho"
2-"Sipendi
starehe,kutumia pesa vibaya,naiheshimu sana pesa yangu,matumizi yake
makubwa ni chakula,pengine mafuta kwa ajili ya gari matumizi mengine ya
mhimu kwa binadamu na zaidi naitumia pesa yangu kufanya kitu
kitakachoendelea kumantain muziki wangu"
3"-Sibani
pesa kwenye swala la kujijenga kimziki,niko tayali nitumie milioni
kadhaa kufanya kitu kitakachojenga status yangu vizuri,mfano
kugharamikia mavazi ya shows n.k"
VIKONGWE WATATU WACHINJWA KAMA KUKU NA KUCHOMWA MOTO
Matukio kama haya ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwauwa wenzao kwa kuwachoma moto yamekithiri katika jamii na ndiyo yaliyosababisha ajuza watatu kuuwawa kikatili usiku wa kuamkia leo huko Bunda, Mara |
MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto ajuza watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Pia
watu hao mbali na kuwaua kikatili vibibi hivyo kwa tuhuma kwamba
walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza
nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa
wakiwafuga na kuatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa
mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa,
tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira
kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua
kijana huyo hivi karibuni.
Saturday, May 25, 2013
LADY JAY DEE NAYE AMSHANGAA MWANA FA. KUTOKANA NAYE KUANDAA SHOW TAREHE MOJA NA KUAMUA KUMCHUKUA LINNAH.
Kutokana na JIDE kuwa na show yake kubwa
mnamo tarehe 31 mwezi huu pale nyumbani lounge ,Sasa rafikiye wa karibu
sana MwanaFA inaonyesha naye ameanda show yake siku hiyohiyo ya Tarehe
31,Zaidi ya yote mwana FA akawachukua wasanii walio jitoa katika show
ya JIDE kama Linnah sa kutokana na sitofahamu hiyo mtandao huu wa
thechoicetz uliweza kumtafuta JIDE kupitia twitter na kumuu liza juu ya
hili swala naye aliweza kutoa yake anayo yafikiria,pia mtandao huu wa
thechoicetz ulimtafuta MwanaFA lakini mwanaFA hakuweza kutujibu swali
tulilo muuliza hadi muda huu
Hivi ndivyo jide ALIVYO TUJIBU
"MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO "...!!
Tukio
hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la
Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter
lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

Baada ya Mahakama Kumruhusu Dr. Slaa Kuoa, Ridhiwani Kikwete Amponda Facebook
Picha za mwanasheria aliyebambwa akifanya ukahaba. Ashitaki mawakili kwa kusambaza picha zake za uchi
Mwanasheria
mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na
mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa
wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza
picha zake za utupu.
Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama ‘John Doe’ walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.

Subscribe to:
Posts (Atom)