MSANII mkongwe wa muziki wa bongo fleva ambaye mpaka sasa anashikilia taji la mkali wa mashairi nchini Seleman Msindi'Afande Sele a.k.a Dume la Simba juzikati alizua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofulika ndani ya kiwanja kipyacha Tanzanati Complex baada ya kuangua kilio jukwaani.Baada ya kuona hali hiyo waandaji wa shoo hiyo walipata jukwaani kwa kushirikiana na mabaunsa ambao kwa pamoja walimbembeleza msanii huyo bila mafaniki hali iliyosababisha baadhi ya mashabiki hasa wa kike nao kumsapoti kwa kuangua vilio vilivyovuma ukumbi mzima.
Tuesday, May 14, 2013
ZITTO KABWE APIGWA KIBUTI LIVE MTANDAONI NA DEMU WAKE ( LOVENESS DIVA)
Waswahili husema ..."Mapenzi ni UCHIZI"...
Hili ndo tunalolishuhudia kwa Mh Zitto na Manzi wake MAPEPE ( Loveness Diva ) ambaye ameamua kumtema na kupeleka penzi lake kwa Prezzo wa Kenya..Kwanza ulianza ujumbe wa kumpongeza Prezzo na ahadi ya kumtema RAIS WETU MTARAJIWA....
Baaye kikafuata KIBUTI kwa mh. Mbunge.
WABUNGE WADAIWA KUPEANA MIMBA, STORI YA SAKATA ZIMA HII HAPA
SKENDO nzito inalitafuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikitawala madai kwamba kuna wabunge wawili wanawake, wamejazwa mimba na waheshimiwa wenzao wanaume.
Awali, ulitawala uvumi kuwa mmoja wa wabunge wa upinzani (viti maalum), akitokea Kanda ya Kaskazini, amepewa ujauzito na mheshimiwa mwingine ambaye ni kiongozi anayeshika nafasi za juu kwenye moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini (wote majina yao tunayahifadhi kwa sasa).
Kashfa hiyo ya mtunga sheria huyo kupewa mimba na mheshimiwa mwenzake ambaye ni mume wa mtu, ilipata mbeleko na kuifanya ivume zaidi, baada ya Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde (pichani), kulipuka bungeni: “Humuhumu ndani kuna wabunge wanawake wenye mimba zisizotarajiwa.”
Lusinde, alitamka hayo Aprili, mwaka huu, wakati akichangia hotuba ya bajeti, Ofisi ya Waziri Mkuu, kipindi ambacho bunge lilikuwa limechafuka kutokana na wabunge kurushiana ‘mipasho’ wao kwa wao.
Kauli ya Lusinde, pamoja na kupokelewa tofauti na wabunge wengi wanawake, wakidai mheshimiwa mwenzao amewadhalilisha, upande mwingine, katika ‘vikao vya kwenye korido’, matukio ya vicheko na kugonga mikono yalitawala na kunena kwa msisitizo “message delivered”, yaani ujumbe umefika.
Wakati mwandishi wetu akifuatilia sakata lenyewe, mbunge mwingine wa Viti Maalum (CCM) ambaye jina lake tunaliweka kabatini, aliamua kufunguka: “Nashangazwa sana na haya madai, tunawasema wapinzani, wakati hata kwetu (CCM) kuna watu wamepeana mimba.”
Awali, ulitawala uvumi kuwa mmoja wa wabunge wa upinzani (viti maalum), akitokea Kanda ya Kaskazini, amepewa ujauzito na mheshimiwa mwingine ambaye ni kiongozi anayeshika nafasi za juu kwenye moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini (wote majina yao tunayahifadhi kwa sasa).
Kashfa hiyo ya mtunga sheria huyo kupewa mimba na mheshimiwa mwenzake ambaye ni mume wa mtu, ilipata mbeleko na kuifanya ivume zaidi, baada ya Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde (pichani), kulipuka bungeni: “Humuhumu ndani kuna wabunge wanawake wenye mimba zisizotarajiwa.”
Lusinde, alitamka hayo Aprili, mwaka huu, wakati akichangia hotuba ya bajeti, Ofisi ya Waziri Mkuu, kipindi ambacho bunge lilikuwa limechafuka kutokana na wabunge kurushiana ‘mipasho’ wao kwa wao.
Kauli ya Lusinde, pamoja na kupokelewa tofauti na wabunge wengi wanawake, wakidai mheshimiwa mwenzao amewadhalilisha, upande mwingine, katika ‘vikao vya kwenye korido’, matukio ya vicheko na kugonga mikono yalitawala na kunena kwa msisitizo “message delivered”, yaani ujumbe umefika.
Wakati mwandishi wetu akifuatilia sakata lenyewe, mbunge mwingine wa Viti Maalum (CCM) ambaye jina lake tunaliweka kabatini, aliamua kufunguka: “Nashangazwa sana na haya madai, tunawasema wapinzani, wakati hata kwetu (CCM) kuna watu wamepeana mimba.”
JESHI LA POLISI LAWASWEKA RUMANDE POLISI 16 KWA MAGENDO JIJINI DAR ES SALAAM
Mkuu wa jeshi la polisi,Said Mwema
DAR ES SALAAM.
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata askari wake 16 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kushiriki na kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wa magendo wanaovusha bidhaa zao kupitia bandari bu
bu kandokando ya Bahari ya Hindi na maeneo mengine.
Hatua hiyo umekuja baada ya kubaini baadhi ya askari wa vikosi mbalimbali ambao imeelezwa kuwa wametengeneza mtandao huo ulioanzishwa zaidi ya miezi sita kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao hukusanya fedha kinyume cha sheria kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru halali Serikalini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: "Tumeshirikiana na wananchi kwa kufuatilia nyendo za askari hao na kubaini kuwa walitengeneza mtandao huo wa kuvusha mali kupitia bandari bubu zisizo rasmi maeneo ya Kawe hadi Bagamoyo."
Alisema polisi kupitia teknolojia ya kisasa iliwabaini askari hao kwa nyakati mbalimbali wakishirikiana na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakitoa rushwa ili wasikamatwe.
“Mpaka sasa askari wa vyeo mbalimbali waliokamatwa wako 16 na wanaendelea kuhojiwa... majina yao yanahifadhiwa kwa sasa kwani bado kuna wengine wanatafutwa ili kuwabaini na kuusambaratisha mtandao mzima,” alisema.
Alisema mtu yeyote ambaye amefanya kosa ndani ya Jeshi la Polisi atachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani kama raia wengine.
Kamanda Kova alisema operesheni hiyo itawalenga wafanyabiashara, wafanyakazi wa TRA na wa taasisi nyingine watakaobainika kuhusika na mtandao huo.
KASHFA YA WABUNGE WA KIKE KUJICHUBUA YAIBUA MJADALA MZITO...!!
KUMBE! Baadhi ya wabunge wa kike ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatumia vipodozi vinavyochubua ngozi ya juu ya mwili ili wawe na mwonekano mweupe (kama wazungu).
Kauli hiyo ya kushangaza ilitolewa bungni Mei 9, mwaka huu na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy wakati alipokuwa akichangia Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu udhibiti wa dawa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Akizungumza bila kupepesa macho, Mheshimiwa Kessy alisema kuwa baadhi ya waheshimiwa wa kike ndani ya mjengo wanatumia vipodozi ambavyo vina madhara makubwa kwa afya ya mtumiaji.
“Labda niseme tu TFDA wanapaswa kusimamia kuhakikisha vipodozi vyenye madhara haviingii nchini, watu wengi sana wanaathirika na kupata magonjwa ya kansa ya ngozi.
“Humu ndani (bungeni) wapo waheshimiwa ambao wanatumia vipodozi hivyo ambapo wanapokuja kuumwa serikali inapoteza fedha nyingi kwenda kuwatibia nje ya nchi,” alisema Kessy.
WABUNGE WAMEKASIRIKA?
Akizungumza bila kupepesa macho, Mheshimiwa Kessy alisema kuwa baadhi ya waheshimiwa wa kike ndani ya mjengo wanatumia vipodozi ambavyo vina madhara makubwa kwa afya ya mtumiaji.
Grace Kiwelu.
MSIKILIZE KWA KINA“Labda niseme tu TFDA wanapaswa kusimamia kuhakikisha vipodozi vyenye madhara haviingii nchini, watu wengi sana wanaathirika na kupata magonjwa ya kansa ya ngozi.
“Humu ndani (bungeni) wapo waheshimiwa ambao wanatumia vipodozi hivyo ambapo wanapokuja kuumwa serikali inapoteza fedha nyingi kwenda kuwatibia nje ya nchi,” alisema Kessy.
WABUNGE WAMEKASIRIKA?
REGINALD MENGI ATANGAZA DAU LA MILIONI MOJA KWA MTU ATAYEMTUMIA TWEET NZURI
Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurashia.
Not to fast though…… Sio tweet zile za ‘I’m having fun being single, #TeamSingle, tupa kuleee!
Mengi anataka ulikune jicho lake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka 1 anzia Mei ntatoa sh 1m kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini,” ametweet leo.
Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu akiandika tweet afanye kummention ili aione.
AJALI YA COASTER NA LORI YAUA ABIRIA MMOJA AFARIKI DUNIA WENGINE 17 WAKIJERUHIWA WILAYA RUNGWE MKOANI MBEYA.
MSANII WA BONGO MOVIE ATAFUTA MUME WA KUMZALISHA
Baada ya kuadimika kwa muda mrefu, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aisha Bui ameibuka na kusema kuwa anatafuta mwanaume ambaye atamzalia mtoto na hatimaye waoane ila akadai wa kumuoa kwa sasa hamuoni
Akizungumza na mwandishi wetu, Aisha amefunguka kuwa alikuwa kimya kwa sababu kuna mambo alikuwa akifanya.
Alisema kwa kuwa ameyakamilisha, sasa ana nafasi ya kusaka mtoto iwapo atampata mwanaume sahihi.
Aisha amevitaja vigezo vya mwanaume wa kumzalia kuwa amjengee nyumba ya kuishi yeye na mtoto wake kisha awe na uwezo wa kumlea na kumpatia elimu bora.
Monday, May 13, 2013
WHO yasema coronavirus yaambukiza.
Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inaelekea sana kuwa aina mpya ya virusi vinavouwa, vya coronavirus, vinaweza kuambukizwa baina ya watu walio karibu sana.
Virusi hivyo ni sawa na vile vya homa ya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) na vinamfanya mgonjwa kuwa na shida sana ya kuvuta pumzi.
Nchini Ufaransa mwanamume mwengine hivi sasa ni mahtuti baada ya kuambukizwa na mgonjwa wa mwanzo nchini humo, ambaye walilazwa chumba kimoja hospitali.
Hadi sasa watu 34 wanajulikana kupata ugonjwa huo duniani tangu mwaka wa 2012, 18 kati yao walikufa Saudi Arabia.
WHO inasema ni muhimu kujulisha watu kuhusu virusi hivyo kwa sababu kuna wasi-wasi mkubwa kuwa vinaweza kusambaa.
Chanzo ni BBC Swahili.
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUTANGZWA WIKI HII
Matokeo mapya ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 yanatarajia kutangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi siku yeyote wiki hii.
Kutangazwa upya kwa matokeo hayo kunafuatia uamuzi uliochukuliwa na serikali hivi karibuni kufuta wa matokeo hayo ili yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.
Habari ambazo NIPASHE imezipata jana na kuthibitishwa na
viongozi wandamizi wa wizara hiyo, kazi ya kufanya marekebisho ya matokeo hayo imeshakamilika na yatatangazwa wiki hii.
“Kazi ya kuandaa matokeo imekwishakamilika sababu ni kazi inayofanywa na watu watatu kwa kutumia kompyuta,” alisema ofisa mmoja ambaye alisema taarifa rasmi zitatolewa na Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
AFANDE SELE AMSHUKURU MH. ZITTO KABWE KWA KUGHARAMIA VIDEO YAKE, HIKI NDO ALICHOKISEMA
Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO. Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.
Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"
Subscribe to:
Posts (Atom)