Saturday, May 11, 2013
SHEIK PONDA NA USTAADH MUKADAM WATOA TAMKO KALI LEO
Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho.
Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo mkubwa mmoja alie mahututi Afrika kusini(wanadai eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!
KAULI ZA SHEIKH PONDA.
Alitamka kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote!
Karudia tuhuma za kuwa NECTA kuna udini na Waislamu wanafelishwa! Kasema serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia kuhusu bomu la Arusha kasema, wamekamatwa waarabu ,mbona hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na uislamu!
Ponda kasema wakristo hajawahi kuuawa na serikali,ila waislamu 2 ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa.Anadai hata Pemba Waislamu waliuawa na serikali ikitumwa na Kanisa! Amehoji,mbona hatujawahi kusikia mchungaj au padri kauawa?kasema pemba kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini) wakati wanakimbilia Mombasa naTanga.!
Pia kasema,nchi hii hakuna udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pakusemea
Credit: JAMIIFORAM
Friday, May 10, 2013
WANAFUNZI WALA KICHAPO KIKALI MARA BAADA YA KUNASWA WAKIJIUZA NJE YA NYUMBA YA KIGOGO WA SERIKALI HUKO SINZA...!!
WAREMBO watatu wanaodaiwa kuwa ni madenti wa chuo kikuu kimoja jijini Dar, waliojitambulisha kwa jina mojamoja, Rachel, Neema na Suzan, wamekumbana na balaa zito baada ya kupokea kibano cha kutosha, Ijumaa lina mkanda kamili.
Tukio hilo lililonaswa laivu na gazeti hili lilitokea maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, usiku wa saa 8:00, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo madenti hao walipokea kibano ‘hevi’ kutoka kwa Polisi Jamii.
Kipondo: Madenti hao baada ya kusurubiwa na Polisi Jamii.
KERO
“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.
“Unajua walikuwa kero sana. Yaani asubuhi kukicha utakuta mipira ya kiume imetapakaa kila sehemu. Mbaya zaidi utakuta watoto wakicheza mchana wanaokota hiyo mipira ya kiume na kupuliza kama puto,” alisema shuhuda mmoja aliyeamshwa na makelele ya warembo hao wakati wakila kibano.
Vilio: Warembo hao wakilia baada ya kichapo.
Aliendelea: “Unajua wakikaa hapa ni hatari tupu kwani wanaume wanaokuja kuwafuata wanaweza wakatudhuru kwa sababu hatuwajui.”
SHAFFIH DAUDA MATATANI NA TFF, APEWA SIKU SABA TU ATOE MAJIBU !

Shaffih Dauda
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba
Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA
Kwa kuipitia barua hiyo bofya: HAPA
MAINDA WA BONGO MOVIE AOKOKA KILA MAHALI NA BIBLIA CHEKI PICHA HAPA.
MSANII wa filamu ambaye alikuwa Muislam na baadaye kuamua kuingia kwenye Ukristo na kuokoka, Ruth Suka ‘Mainda’ sasa anaonekana kupambana vilivyo kuhakikisha anaiboresha imani yake kwa kutembea na Biblia kila anakoenda.
Ruth Suka ‘Mainda’ akiwa na Biblia yake mkononi.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Mainda aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa msanii huyo anaonekana kuwa na uchu wa kuijua vilivyo Biblia.
Ruth Suka ‘Mainda’ akisoma Biblia.“Kwa kweli sasa hivi Mainda hakaukiwi na Biblia mkononi, yeye na Biblia kila wakati. Kuna wakati hata akiwa lokesheni, akipata muda kidogo anaitoa na kuanza kuipitia. Hakika amebadilika,” kilisema chanzo hicho huku maneno hayo yakishibishwa na picha alizotupia Mainda kwenye mtandao wake wa Facebook zikimuonesha akiwa ameshikilia kitabu hicho kitakatifu.
ALIYEJIBADILISHA JINSIA NA KUWA MWANAMKE ATAKA BARAZA LA MTIHANI LISHURUTISHWE KUBADILI VYETI VYAKE NA KUWA NI MWANAMKE
| BAADA YA KUJIBADILISHA |
Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.
Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti vyake.
DIAMOND PLATZNUM AMKANA MDOGO WAKE WA DAMU!!
Katika pita pita zetu tukutana na kijana aitwaye Saleh Abdul anayedai kuwa ni mdogo wake na Diamond Platnumz. Saleh anadai yeye na Diamond wanachangia baba lakini jitihada zake za kuwa karibu na kaka yake zimekuwa zikigonga mwamba kwakuwa hitmaker huyo anadai kumkana.
“Mimi ni mtu ambaye nina kipaji cha kuimba lakini najikuta kwamba naambulia patupu yaani kukosa msaada wowote, nikimwendea kaka yangu Diamond anashindwa kunielewa, hataki kunisaidia, halafu wakati mwingine ananikana kabisa kwamba mimi sio mdogo wake,” amesema Saleh kwa uchungu
source bongo5
source bongo5
MAMA KANUMBA: CHONDECHONDE, KABURI LA MWANANGU LISIGEUZWE MTAJI
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
BAADA ya siku za hivi karibuni kubainika kuwa baadhi ya vijana wanaolinda makaburi ya Kinondoni wamegeuza mtaji kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, mama mzazi Flora Mtegoa amewaomba wahusika kuacha mchezo huo mara moja.
Akizungumza kwa huzuni mama Kanumba alisema alihuzunishwa sana na kitendo hicho cha kaburi la mwanaye kugeuzwa mtaji na kumtaka mtu yeyote atakayetozwa pesa aripoti polisi mara moja.
“Inaniuma sana na naiomba serikali na watu wengine wanisaidie jamani kwa sababu wanaofanya biashara hiyo ya kulipisha watu kwa ajili ya kuliona kaburi wanakosea,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni ilibainika kuwa baadhi ya vijana wanaotunza makaburi ya Kinondoni wanatoza shilingi 5,000 kwa watu wanaotoka mikoani kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba na kupiga picha.
Na GP
Prezzo kuhusu penzi la Diva: Bado mahari tu ipo njiani kutoka Mwanza
Apparently watangazaji wa kike wa Clouds FM humchanganya sana Rapcellency, Prezzo. Kama unakumbuka aliwahi kudai kuwa hasemi wala haongei kwa uzuri wa Dj Fetty.

Na sasa word on the street ni kwamba jicho la rapper huyo mwenye asili ya Kenya na Tanzania limetua kwa mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho, Loveness Diva. Wiki iliyopita, Diva alimwalika Prezzo kwenye show yake na huenda ukaribu huo uliongezeka zaidi siku hiyo.
Kwa mujibu wa You Heard ya Clouds FM, Diva na Prezzo ni item.
“Diva siwezi kumwachia bwana, nimwachie nichekwe,” alisema Prezzo.
“Bado mahari tu mshkaji wangu inatoka kutoka Mwanza. Only time can tell, nikikuambia sasa hivi ukweli wangu ntamaliza uhondo. Inaitwa yaani love at first sight, Diva mwenyewe umeshamwona, she is classy yaani she is beautiful,” alisisitiza Prezzo ambaye jina lake ni Jackson Makini.
Hata hivyo Diva amekanusha kwa kudai kuwa yeye na Prezzo ni marafiki tu.
KOCHA WA EVERTON DAVID MOYES ATANGAZWA KURITHI MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON MAN U
Kocha wa Klbau ya Everton, David Moyes, leo mchana ametangazwa rasmi kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson, aliyetangaza kujiuzulu jana, ambapo sasa kocha huyo atakua na kibarua cha mkataba wa miaka 6, ya kuinoa timu hiyo ya Mashetani wekundu.
Moyes, amesaini kataba wa miaka sita leo mchana na kutangazwa rasmi kukabidhiwa mikoba hiyo, ya Ferguson, aliyeitumikia Klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 27 na kuipa mataji 20.
Akizungumza wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo, Moyes, alisema kuwa anatarajia kujiunga na wekundu hao mara tu utakapomalizika rasmi msimu huu wa Ligi ya England.
Wakati hayo yakijiri, Kuna habari zilizochini ya Kapeti hadi sasa kuwa huenda, katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya England, Timu hito ya Man U, ikamkosa mshambuliaji wake, Wyne Rooney anayetarajia kutimka katika Kikosi hicho na badala yake sasa anayetarajia kujiunga kwa mara ya pili na kikosi hicho ni aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, ambaye kwa sasa anakipiga na Klabu ya Real Madri, Christiano Ronaldo.
Thursday, May 09, 2013
UWOYA AJISAFISHA KUPITIA JINA LA RAISI, SOMA ALICHOKISEMA HAPA
Irene Uwoya.
STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata. Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.
“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu ningeitwa na rais wa Burundi kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo maana aliniita mwaka 2011 kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu tusingekubalika hadi na viongozi wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,” alisema Uwoya akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kuhusu madai ya wasanii kuwa na tabia chafu.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri
BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA
Mwimbaji wa Muziki wa Injili Bahati Lusako Bukuku.
MWIMBAJI wa Muziki wa Injili mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
CHANZO CHA HABARI NI MTANDAO WA GLOBAL PUBLISHERS
KIOJA CHA MWAKA 2013...MWANAUME KWA MWANAUME WAFUMWA LAIVU GEST..Angalia PICHA
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
Breaking Newzzzzzzzz......!!! SHEIKH PONDA AHUKUMIWA MWAKA MMOJA
Hukumu ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda imetolewa leo katika mahakama ya kisutu jijini dar es salaam ampapo kahukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.
Subscribe to:
Comments (Atom)










