Tuesday, April 16, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE APRIL 16, 2013

.
.
.
.

Kutoa Taarifa za Siri Katika Mawasiliano ya Elektroniki ni Kosa la Jinai.

Jana na leo, Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa katika vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu, wahusika wa namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo hili ni Kosa la Jinai. Mfano; tamko la Chadema lililotolewa na Ndugu Mabare Marando Mjini Dar es Salaam tarehe 14/04/2013.
Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;
“Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii”. Aidha, “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”

Monday, April 15, 2013

JB AJITOSA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE MWAKA 2015..!!



Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda muafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii,” alisema JB.
Hata hivyo, ‘mheshimiwa’ huyo hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea akisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja kubwa lenye upinzani mzito kila ukifika wakati wa uchaguzi.
“Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi,” alisema JB.

KAJALA APATA MCHUMBA MPYA, NI MFANYAKAZI WA WEMA

petit
Kajala ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mtayarishaji wa muziki maarufu hapa Bongo “P-Funk” na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja, hivi sasa inasemekana ana-roll na mchizi mmoja ambaye ni member wa kampuni ya Endless Fame ya Wema Sepetu. Solid snitch wa bongomovietz.com ambaye amezipata za chinichini na ku-notice nyendo mbili tatu  za bootylicous actress Kajala Masanja kupitia BBM na mshkaji huyu. Directly unaweza kukubali kwamba yes, Jamaa na Kajala ni mtu na mpenzi wake kwa sasa. All is well, its a new life for Kajala and she deserve to love and to be loved. Best wishes kwenye kila anachokifanya hasaa kazi ya yake ya movie.

ANGALIA MKOKO MPYA WA 50 CENT, UMETENGENEZWA KWAAJILI YAKE TU....!!

.
.
.

SHIBUDA AANDAA MAANDAMANO YA NG'OMBE HADI IKULU KWA KIKWETE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbwjqjXHF9HaBsolyXSDp-xs7jy7u86HL0TuBEty_uSHykuZ6QMyLHZbNHRh50YBas5PQi5OkPltEurwLSyl6veaC1nBEda38tZmMGBUt5KuHRyqikKzczdV1uep3ZrfWqg2J5C2QMz9Nh/s1600/sawa.jpgMbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda anatarajia kuongoza maandamano makubwa ya ng’ombe kutoka Lusumo Nyakabanga Mkoani Kagera, hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ili kupinga uonevu na manyanyaso wanayofanyiwa wafugaji. 
 
“Kama watu wanasema ni porojo za Shibuda, basi wasubiri kama hotuba ya Waziri Mkuu haitakuwa na majibu kwa wafugaji, lazima hayo yatatokea kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, hawa nao ni binadamu waambiwe basi kama hawatakiwi Tanzania,” alisisitiza.
 
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi akiwa na uongozi wa wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa ambao wako Dodoma kwa lengo la kuonana na Mawaziri wa Maliasili na Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri Mkuu, ili kufikisha kilio cha wafugaji ambao wanateketezewa mifugo yao na askari wa wanyama pori.
 
Shibuda alisema kuwa “Katika nchi yoyote duniani hakuna mateso yanayofanywa kwa wananchi wake kama ambavyo inafanyika Tanzania kwa upande wa wafugaji, ni heri ya wakimbizi watakuwa na amani kuliko hawa wanaonekana kama takataka.”

JOKATE AMCHEKA UWOYA BAADA YA KUSIKIA KATOKA NA DIAMOND

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ameangua kicheko baada ya kusikia mwigizaji Irene Uwoya kunaswa hotelini na Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Jokate aliangua kicheko hicho juzikati jijini, Dar wakati alipozungumza na paparazi wetu na alipogusiwa kuhusu suala la Uwoya kunaswa na Diamond, alicheka sana huku akimshangaa.
“Hahaha sasa ndiyo nini tena, yeye si aliwahi kunisema mimi nakwapua mabwana? Sasa leo imetokea kwake tena!” alisema Jokate.

 
Irene Uwoya.

"SHILOLE NI MNAFIKI…MIMI SIKUMBAKA BALI ALINIPA PENZI KWA HIARI YAKE"

MZAZI mwenziye na staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Makala Elias amembomoa staa huyo na kumwambia aache kuungopea umma kuwa alibakwa wakati waliishi naye kinyumba.

Akiongea  na  mwandishi wetu, Makala aliweka wazi kuwa anasikitika anapomsikia Shilole akisema kwamba alipata ujauzito baada ya kubakwa wakati walioana na kuachana miaka ya nyuma kabla staa huyo hajawa maarufu.
“Namsihi Shilole aache kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na kuwafanya Watanzania wamuone mtoto aliyenaye alimpata kwa njia ya kubakwa wakati alikuwa ameolewa na mimi,’’ alisema Makala ambapo Shilole alikataa kuzungumzia juu ya ishu hiyo akidai ameshazungumza mara nyingi.

BINTI ATUMIA FACEBOOK KUELEZA HISIA ZAKE ZA MAPENZI KWA DIAMOND........!!!

 Katika  hali  ya  kushangaza, binti  mmoja  maarufu  kwa  jina  la  Hilda  amejitokeza   hadharani  kupitia  facebook  yake  na  kudai  kuwa  yupo  tayari  kugawa  penzi  kwa  diamond  hata  bure  ili  naye  ajionee  kinacho wafanya  wanawake  wenzie  wamgombanie...

Huu  ni  ujumbe  wake
"Hey tsup..!! Diamond  nipe  penzi  lako  nionje  kinachofanya  kila  mwanamke  akung'ang'anie  na  kukutaka..
nataka  kujua  ni  ufundi  ama  una  mashine  kubwa  au spe*m zako  zina almasi???.. c'moon plutnumz  give me a chanche to one nite

Wema,Wolper,Uwoya,Aunt Ezekiel ...haiwezekani....Mwanaume unacho cha ziada siyo bure...

Nahitaji any time na popote.nitakuvulia chupi bila hofu.take my body right now bro..."

ZITTO KABWE AZIDI KUIUMBUA CHADEMA KUTOKANA NA TAMKO LAO


Namba hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012. Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.
Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

MAGAZETI APRIL 15, 2013 UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.
.

HII NDIO KAULI YA MJENGWA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI MAKAO MAKUU KUHUSU KUTEKWA KWA KIBANDA HII HAPA




Ndugu zangu,
Kama alivyowataarifu kaka yangu Nyaroonyo Kichehere, ni kuwa, jana Jumamosi nilikuwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa tano asubuhi ya jana mpaka saa tatu usiku. Ilihusu mahojiano ya Polisi na mimi kuhusiana na sakata la ndugu yetu Absalom Kibanda.

Ukweli sikukamatwa mahali popote, bali niliitwa na Kamishna ( Upelelezi) Advocate Nyombi. Alhamisi nikiwa Iringa, tukakubaliana na kiungwana na Kamishna Nyombi kuwa nifike Makao Makuu hayo ya polisi Jumamosi saa tano. Ikawa hivyo.

Hapo nilipokelewa na Kamishna Nyombi. Baada ya mazungumzo mafupi ndipo akawaita maofisa wengine watano wa Upepelezi kufanya mahojiano nami.

Niliomba niwe na Mwanasheria, nikakubaliwa. Nilimpigia simu kaka yangu Nyaroonyo, naye, kwa vile ni Wakili pia wa Kibanda akanisaidia kuhakikisha napata wakili mwingine. Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, ndugu yangu Nyaroonyo Kichehere alifanya alivyoweza.

Ndani ya dakika 40 hivi alifika chumba nr 704 ghorofa ya saba akiwa na Wakili Jacquiline Rweyongeza na Legal Officer Dickson Mbonde. Nilimshukuru Kaka Nyaroonyo Kichehere. Na nilimuaga kwa kumwambia; “ Nenda ukaifahamishe jamii juu ya hiki kilichonitokea”.

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati kabisa dada yangu Wakili Jacquiline Rweyongeza na kaka Dickson Mbonde kwa kuacha yote ya Jumamosi na kuwa tayari kuwa msaada kwangu.

Sunday, April 14, 2013

HII NDIO NYUMBA MPYA YA DIAMOND ANAYOMALIZIA KUIJENGA...!!

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA

Ndugu waandishi wa habari; 
LEO tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi. 


Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine. 


Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa. 

Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 
14 Aprili, 2013

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika Hosptali ya TMJ.

Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea nidhamu na uzalendo.

Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO YA MAREHEMU
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...