Ndugu waandishi wa habari;
LEO
tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba
nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu,
nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo
mengi mno.
Uchunguzi huu
nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na
Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa
mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo
kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika
uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la
watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango
hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi
na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi
la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote
wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom
Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.
Aidha, Nchemba amedai kumiliki video
ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya
kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu
makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?
Kwamba genge hili la kina Nchemba na
wenzake, walipanga kumteka Kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye
wakaingia kwenye plani B ya kutaka kuihusisha Chadema. Wakamtumia
Ludovick Joseph Rwezahula ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya
Lwakatare, kufanikisha mkakati wao huu wa kishetani.
Ndugu waandishi wa habari;
Huu ni mchezo mchafu na wahatari mno
ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa. Kuanzia sasa nimeamua kwa
dhati kabisa, kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa
letu.
Kwa kuanzia,
kesho Jumatatu, nitaongoza jopo la mawakili sita wa Chadema kumtetea Bw.
Lwakatare. Wenzangu wengine katika kesi hii, ni Profesa Abdallah
Safari, Tundu Lissu, Edson Mbogoro, Peter Kibatara na Nyaronyo Kicheere.
Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja anayewekwa na
familia ya Lwakatare.
Ndugu waandishi wa habari;
Mnaweza kujiuliza, kwa nini Chadema
kimechukua uamuzi huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi
hii ya Lwakatare? Jibu ni kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa
kwa lengo maalum la kuidhoofisha Chadema na kuinusuru CCM ambayo
inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana
na kushamiri kwa makundi.
Hivyo wameamfungulia kesi Lwakatare, kwa
lengo la kutaka kuaminisha umma kuwa Chadema ni chama cha magaidi,
kinapanga ugaidi na hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!
Ndugu waandishi wa habari;
Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha
ombi maalum la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za
mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili
kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.
Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri
ya kuletwa taarifa zao simu
na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi
wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na.
255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu
Lameck Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 008888, 0757 946223,
0714 008888 na 0787 513446 na Ludovick Joseph Rwezahula, ambaye simu
zake ni,0715 927100 na 0753 927 100.
Mwingine ambaye mawasiliano yake
yanahitajika, ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi,
anayetumia simu Na. 0754 003388, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya
Mwananchi, Dennis Msaky anayetumia simu mbili, 0655 331010 na 0764
331010 na Bw. Sinbad Mwagha, ambaye ni afisa wa idara ya usalama wa
taifa, anayetumia simu 0754 006355.
Wengine,
ni Bw. Shaali Ali, afisa mwinge wa usalama wa taifa anayetumia simu Na.
0716990099, Saumu K. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 541 434 na 0789
614 629, simu mbili zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa Dk.
Steven Ulimboka, Bw. Ramadhani Abeid Igondo ikiwamo 0713 760 473, simu
za Bw. Ridhiwani Kikwete ambazo ni 0754 566299, 0784 566 299, simu ya
Dr. Steven Ulimboka, ambayo ni 0713 0713 731 610, pamoja na simu zote
tatu za Willifred Lwakatare, ambazo ni 0786 774697, 0713 237869 na 0758
417169.
Ndugu waandishi wa habari;
Mtu mwingine muhimu nitakayeomba
mahakama itoe amri ya kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari
na mpigapicha wa magazeti ya serikali, Muhidini Issa Michuzi. Mwandani
huyu wa Ikulu, ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya emeili kuipongeza
ofisi binafsi ya rais (OBR) na usalama wa taifa kwa kupata video ya
Lwakatare.
Pongezi za Michuzi kwa TISS ndizo
zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi
anaipongeza TISS kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS
ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu
wa Lwakatare ulipelekwa Youtube, badala ya kwenye vyombo vya sheria.
Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua
hiyo video yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na
kwamba Chadema kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa
taifa katika kazi hiyo chafu. Software za video (editing) walizotumia
zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka usalama na Ikulu.
Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa anayempelekea
kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.
Ndugu waandishi wa habari;
Chadema kinajua kuwa mmoja wa
watuhumiwa hawa, Mwigulu Nchemba anafanya mipango na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake.
Nachukua nafasi hii, kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa
kuwa ni kinyume cha sheria za mamlaka ya mawasiliano (TCRA).
Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa
Mwigulu – zinaonyesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na
Ludovick, yakiwamo yale ya tarehe 4 Machi 2013. Hii ilikuwa siku moja
kabla ya Kibanda kutekwa.
Ndugu waandishi wa habari;
Hawa niliowataja ni watu muhimu sana
katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na
vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na
kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dr.
Steven Ulimboka.
Kwa mfano, simu
ya Mwigullu Nchemba, namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223,
zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu,
Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika
katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi
tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.
Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona
yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa
Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya
Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013,
ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.
Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana
na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na
Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa
ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.
Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna
Mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha
anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye
aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye
aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari na Machi 6 mwaka huu.
Ndugu waandishi wa habari;
Ludovick alifanya mawasiliano ya
mwisho na Joyece Agustine, ambaye anatumia simu Na. 0717 559210,
mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku. Hiyo ndiyo ilikuwa simu
yake ya mwisho usiku huo; katika siku hiyo Ludovick aliwasilisna na
Joyce mara tisa kuanzia saa 12: 54 asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao
wa Jamii Forum, ambako video ya Lwakatare ilitumwa, Ludovick alikamatwa
Machi 15 mwaka huu. Hata hivyo, rekodi katika simu yake Na. 0715 927100
inaoyesha 17 Machi Ludovick alifanya mawasiliano na Joyce Augustino.
Mawasiliano hayo yalifanyika saa 8: 9 usiku, wakati inadaiwa na polisi
alishakamatwa.
Naye mhariri wa Mwananchi, Bw. Msaky
ambaye anatajwa kutaka kutekwa na Ludovick na Lwakatare, amekuwa na
mawasiliano kadhaa na Ludovick – mtu anayepanga kumteka. Ludovick na
Msaky walifanya mawasiliano mfululizo kati 27 Desema 2012, siku moja
kabla ya video ya Lwakatare haijarekodiwa na 7 Machi siku moja baada ya
Kibanda kutekwa.
Msacky alitumia simu zake hizo mbili
(0764 331010 na 0655 331010) kuwasiliana na Ludovick, huku Ludovick
akitumia 0753927100. Mawasiliano ya 31 Desemba yalifanyika Ludovick
akiwa Tegeta, jijini Dar es Salaam. Mawakala hawa wawili wa usalama wa
taifa (Ludovick na Msaky), walikutana 31 Desemba 2012, katika hoteli ya
Tamal, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Ndugu waandishi
wa habari;
Baada ya kupitia taarifa hizi za
mawasiliano ya simu za Mwigulu Nchemba, Ludovick Joseph, Ramadhani
Ighondo na Saumu Malungu tumegundua yafuatayo: Kwamba, Ramadhani
Ighondo, amefanya mawasiliano mara nyingi na Mwigulu, Mwagha na Zoka;
naye Mwagha amefanya mawasiliano na Mwigulu na Saumu; naye Saumu
amefanya mawasiliano na Mwagha, Mwiguluna Shaali Ali, ambaye ni afisa
usalama wa taifa.
Tumegundua
vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya Ludovick na Msaky; Ludovick
na Mwigulu; Msaky na Nchimbi; Msaki na Mwagha, Samu na Mwagha na
Ramadhani Ighondo Abeid, anayetuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka na Mwanga na
Mwigullu.
Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati
ya Ulimboka na Ramadhani; Zoka na Ighondo na Ridhiwani na Ighondo.
Mawasiliano haya yalifanywa mfululizo usiku wa Juni 2012 siku ambayo Dk.
Ulimboka alitekwa.
Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya
watu waliotajwa na gazeti la MwanaHALISI kuwa waliwasiliana na Ighondo
usiku wa Juni 26, mwaka 2012, wamefanya mawasiliano pia na Mwigulu,
Mwagha na Shaali Ali.
Ndugu waandishi wa habari;
Mwagha ni afisa usalama wa taifa
anayefanyakazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika
kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani. Ni Mwagha
anayepanga wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya CCM. Ushenzi
wote anaoongea Mwighulu bungeni, hupewa na Mwagha kwa maelekezo ya Jack
Zoka.
Naye Shaali ndiye aliyekutana na afisa
wetu wa usalama, Ahmed Sabula na mwenzake, Machi 29 mwaka huu katika
hoteli ya See Cliff jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo kati ya
Sabula, kijana wetu wa usalama na afisa usalama wa serikali Bw. Shaali
alitaka Sabula akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama,
kuwasilisha kwake nyaraka za kamati kuu na kueleza mipango ya chama
katika kesi ya Lwakatare.
Kwenye mpango huu, afisa huyo wa usalama
wa taifa ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha Sh.
milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia
kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira.
Aidha, Sabula aliahidiwa kulipwa
shilingi 500,000 (laki tano) kila mwezi; afisa wetu huyu ameripoti tukio
hilo kwa viongozi wake wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi
wa kesi ya Lwakatare; aliambiwa akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi
Sh. 500, lakini akaombwa kuwa mvumilivu kwa kuwa atalazimika kupotea
kwa miezi kama mitano hadi sita.
Ndugu waandishi
wa habari;
Kitendo cha Mwigulu kuwasiliana
Ramadhani Ighondo, Mwigulu kuwasiliana na Ludovick, Saumu kuwasiliana na
Mwigulu, Ighondo kuwasiliana na Ulimboka, Zoka kuwasiliana na Ighondo,
tena katika muda uleule ambao Ighondo amewasiliana na Ulimboka na Saumu
kuwasiliana na Mwagha, ni uthibitisho tosha kwamba usalama wa taifa wako
nyuma ya mipango hii ya michafu ya kupanga utekaji na kisha kutaka
kukichafua Chadema.
Aidha, kitendo cha Ludovick kuwasiliana
Msaky; Ighondo kuwasiliana na Mwagha, Ridhiwani Kikwete kuwasiliana na
Ighondo, tena kila baada ya Ighondo kuwasiliana na Ulimboka na Jack
Zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa genge hili la wahalifu linashirkiana
na baadhi ya watu kutaka kuangamiza taifa.
Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo
wanaowahonga wanachama wa Chadema na watu wengine ili watoe ushahidi
feki dhidi ya Lwakatare, na kwamba ni usalama wa taifa walioandaa ile
video uchwara inayopigiwa chapuo na Mwigulu.
Ndugu waandishi wa habari;
Chama Cha Mapinduzi kinajua kwa hali
ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku Chadema ikiwa
katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa. Wanajua kabisa CCM
imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya CCM, litahujumu kundi
jingine. Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka
kuiangamiza Chadema. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona Chadema
kinakufa. Tutapambana usiku na mchana. Juna na mvua. Hadi tushinde hila
hizi.Tunawaambia wanachama wetu na wale wanaotuunga mkono, Chadema ni
chama kikubwa. Kina mtandao kila mahali, kuanzia Ikulu hadi polisi; na
hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya kupikwa.
Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama
itawafichua wote hawa ni kuirudisha Tanzania katika amani yake. Ni
lazima tufikike mahala watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka
wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu yana thamani kuliko siasa chafu na
ufisadi wanaouendeleza.
Nawashukuru kwa kunisikiliza.
Mabere Marando,
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment