Monday, April 15, 2013

"SHILOLE NI MNAFIKI…MIMI SIKUMBAKA BALI ALINIPA PENZI KWA HIARI YAKE"

MZAZI mwenziye na staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Makala Elias amembomoa staa huyo na kumwambia aache kuungopea umma kuwa alibakwa wakati waliishi naye kinyumba.

Akiongea  na  mwandishi wetu, Makala aliweka wazi kuwa anasikitika anapomsikia Shilole akisema kwamba alipata ujauzito baada ya kubakwa wakati walioana na kuachana miaka ya nyuma kabla staa huyo hajawa maarufu.
“Namsihi Shilole aache kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na kuwafanya Watanzania wamuone mtoto aliyenaye alimpata kwa njia ya kubakwa wakati alikuwa ameolewa na mimi,’’ alisema Makala ambapo Shilole alikataa kuzungumzia juu ya ishu hiyo akidai ameshazungumza mara nyingi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...