Mchekeshaji na muigizaji wa Tanzania
Tumaini Martin ‘Matumaini’ amevunja ukimya kuelezea maendeleo ya afya
yake akidai kusumbuliwa na maumivu makali ya miguu kwasasa.
Akiongea na
BK Cop leo Matumaini amesema kuwa anaendelea kutumia dozi ingawa hali
ya afya yake bado si shwari kutokana na kugulia maumivu makali ya
Msanii huyo ameeleza kuwa kwa siku moja
huwa anameza vidonge zaidi ya 39 lakini hapati lishe nzuri kwababu ya
kutokuwa na pesa na kujinunulia chakula.
Aidha
amedai kuwa wakati alipokuwa msumbiji alipata misaada ya kifedha kutoka
kwa wasanii mbalimbali lakini hasaidiwi tena tangu alipofika Tanzania.
‘Niliomba
msaada kwenye magazeti ambapo niliacha namba zangu za tigo pesa lakini
meseji nyingi nazopokea ni za pole; hata hivyo kuna watu wanadai
wametuma kwa namba ya Michael Sangu (Mkt Chama cha waigizaji) ambayo
alitoa gazetini lakini mimi sikuwahi kuonana tena na Michael tangu
aliponililipia matibabu wakati natoka hospitali’. Alisema Matumaini
Mnamo
Februari 9 mwaka huu Matumaini aliruhusiwa kutoka hospitali ya Amana
jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa siku tatu tatizo kubwa
likiwa ni miguu na alitakiwa kurudi tena hospitali baada ya kumaliza
dozi aliyoandikiwa na daktari.
Awali
Matumaini alikwenda kuishi nchini msumbiji na kuripotiwa kusumbuliwa na
maradhi, lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambako Naibu Waziri wa
Habari vijana na utamaduni na michezo Bw Amos Makalla akishirikiana na
baadhi ya wasanii alichukua jukumu la kutoa nauli ya kumrudisha nchini.
SOURCE::MPEKUZI::













Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa
mahututi MOI.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya
Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya
kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea
amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa
tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni
yake ya tano.








Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo
za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa
Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.
Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey
Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba
huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.




