Monday, March 18, 2013
DEREVA ANUSURIKA KUCHARANGWA MAPANGA KWA KUMCHOMEKEA MWENZAKE IRINGA
Dereva wa daladala ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa ameshika panga mkononi akitoka kumkoromea dereva mwenzake aliyetaka kumsababishia ajali kwa kumchomekea eneo la Mshindo mjini Iringa leo. PICHA NA MAELEZO FRANCIS GODWIN
TUMEKUWA TUKILEA MTOTO MCHAWI KWA MUDA MREFU BILA KUJUA".....NIKITA WA BONGO MOVIE
KELVIN....
STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed
Khalfan ‘Kelvin’ na mkewe mwigizaji, Elizabeth Chijumba ‘Nikita’
wamesema mmoja wa watoto pacha waliowaasili (adopt) mwenye umri wa miaka
sita, ameonesha matendo ya kichawi...
Akizungumza
na mwandishi wetu, Kelvin alisema waliwachukua watoto hao mapacha kwa
bibi yao Mtwara mwaka 2009 kwa lengo la kuwalea kutokana na mazingira
magumu waliyokuwa nayo lakini walipofika Dar, mmoja alianza kuonesha
vitendo tofauti vya kichawi.
“Wakati
tukiendelea kuishi nao, tulimuona mmoja ana vitukovituko mara kwa mara
na tuligundua kuwa mke wangu alikuwa akiumwaumwa kila alipomgombeza
mtoto huyo.
“Kuna siku niliamka usiku kwenda
kwenye chumba walichokuwa wakilala watoto hao, nikamkuta akiwa uchi
akirukaruka kitandani na nilipomshtua alijilaza kitandani na asubuhi
tulipomuuliza, alisema muda ule bibi yake alikuwa akimrudisha kutoka
kuroga Tanga."
Kwa
upande wake, Nikita alipomdadisi mtoto huyo kuhusu vitendo hivyo vya
kichawi, alimwambia kuwa bibi yake anataka kumuua kwa sababu wanamzuia
asirudi kijijini kwao Mtwara akaendelee kufanya kazi za kichawi.
“Kwa kweli nampenda sana lakini sina budi kumrudisha nyumbani kwao, roho inaniuma kwa sababu nilimzoea,”alisema Nikita.
Mwandishi
wetu alipomuuliza mtoto huyo kuhusiana na sakata hilo, alikiri kuwa ni
kweli bibi yake ni mchawi na huwa anamchukua kwenda sehemu mbalimbali
kuroga kwa kutumia usafiri wa ungo na ndiye anayemroga Nikita.
KAMPUNI YA SIMAMIA YASHUSHA MABANGO YA MATANGAZO YA KAMPUNI YA COCACOLA TAWI LA MBEYA KUTONANA NA KUDAIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 102
Kampuni hiyo ya simamia ikiendelea na kazi ya kufuta maandishi ya kampuni ya cocacola kwa kutumia rangi nyeusi |
Mtumishi huyo wa kampuni ya cocacola nae akaungana na sisi katika kupiga picha utoaji wa mabango hayo ya kampuni yao |
Mbali na hapo alienda moja kwa moja katika kampuni ya simamia lakini hakushuka kwenye gari yake akaondoka kwa kasi mambo hayo |
Kazi inaendelea ya kushusha mabango ya matangazo ya biashara ya kampuni ya cocacola mbeya |
Halimashauri ya jiji la Mbeya kupitia
wakala wa ukusanyaji wa ushuru wa
mabango SIMAMIA imeyashusha mabango ya kampuni ya Vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya kutokana na
kudaiwa zaidi ya shilingi milioni 102.
Hata hivyo kampuni hiyo iko hatiani kuburutwa mahakami kwa kushindwa kulipia gharama za
mabango ya matangazo yaliyowekwa
maeneo mbali mbali ya Jiji hilo .
Kampuni hiyo imeshindwa kulipia gharama za kuweka matangazo hayo kwa
kipindi cha mwaka wa fedha 2012 – 2013 ambapo deni limefikia Shilingi Milioni
102 ambazo walitakiwa kuzilipa kutokana na wingi wa mabango hayo.
Akithibitisha kudaiwa kwa kampuni
hiyoMkurugenzi wa Wakala wa
kukusanya ushuru wa mabango ya biashara na Hoteli Jiji la Mbeya Simamia Company Limited, Ndugu Aloyce Mrema amesema kampuni yake
inatekeleza sheria ya jiji ambayo inataka kila bango la tangazo linatakiwa
kulipiwa.
Amesema kutokana na Kampuni ya Cocacola
kushindwa kulipia mabango hayo kampuni ya Simamia imeamua kutoa mabango yote
yaliyondani ya Jiji la Mbeya ambapo alisema hatua itakayofuata ni kuifikisha
mahakamani kampuni hiyo kwa kushindwa kutekeleza agizo la Halmashauri ya Jiji.
Amesema kabla ya kuanza kutoa mabango
hayo wameshapeleka barua za kuwakumbusha
zaidi tatu lakini bado hawakuitikia wito wa kulipa mapema gharama hizo
zilizowataka hadi ifikapo Machi 18, Mwaka huu kutoa majibu au kulipia mabango
hayo.
Mrema amesema utaratibu wa kampuni hiyo
ni kuhakikisha kuwa kila kampuni iliyoweka bango la biashara katikati ya Jiji
la Mbeya inalipa gharama kwa mujibu wa Sheria za Jiji ambapo kwa takayeshindwa
kufanya hivyo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Aidha ametoa wito kwa makampuni makubwa
kuheshimu sheria za nchi na siyo kukiuka kutokana na kuwa na fedha nyingi
ambapo aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya makampuni sita makubwa ya Jiji la Mbeya
yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo.
Hata hivyo ameyataja makampuni hayo kuwa
ni pamoja na makampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom, Airtel,Zantel, Tbl
na Pepsi ambayo yameshapewa barua za kuwakumbusha kulipia mabango hayo yakiwemo
makampuni ya watu binafsi.
Akizungumzia hatua hiyo Ofisa wa Cocacola
aliyejitambulisha kwa jina moja la Zekaria amesema hajui lolote kuhusu
kuondolewa kwa mabango ya kampuni yake na wakala wa Jiji Simamia ambapo amesema
atalifuatilia na kulipeleka kitengo kinachohusika kwa ajili ya kulitolea
taarifa.
Hata hivyo Ofisa huyo alionekana kukwepa
kutokuwa na taarifa juu ya kampuni hiyo kung’oa mabango ili hali baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo walionekana wakipiga picha na kufuatilia hatua zote
zilizokuwa zikifanyika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Haslmashauri ya Jiji la Mbeya Juma Iddi alipoulizwa juu ya utaratibu wa kampuni
hiyo wa kutoa mabango ya biashara ya kampuni ya Cocacola amesema hajui lolote
kwa sababu kampuni ya Simamia
ilishinda tenda ya kukusanya ushuru wa Hoteli na mabango ya biashara
hivyo yeye hana uwezo wa kuingilia.
Na Mbeya yetu
TAARIFA YA RIDHIWANI KIKWETE KUKANUSHA YALIYOANDIKWA DHIDI YAKE KATIKA MITANDAO YA JAMII
Ndugu zangu habari za wikiendi.
Yapo
mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na
pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu,
kwako au kwa mtu mwingine.
Mojawapo
ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala
la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and
privacy lawas).
Tumeshuhudia
kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert
Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa
teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika
simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy
Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama
kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na
hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia
mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba
si wewe uliyefanya hivyo.
Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma.
Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma.
Ni
ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na
kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili
kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia
kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila
uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali
mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile
anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.
Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.
Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3.
Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.
Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3.
Kuzuia
mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata
sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na vyanzo
vumbi na ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo
haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka
Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo.
Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo.
Namuombea
kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake
kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo
ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au
nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana
Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu
mwengine yeyote.
Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.
Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za uajenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.
Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.
Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za uajenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.
Asanteni sana.
Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.
Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.
Sunday, March 17, 2013
LOWASSA, MENGI KUFANYIWA UMAFIA KAMA ABSALOM KIBANDA.
EDWARD LOWASSA.
Reginald Mengi.
AFISA IKULU AHUSISHWA NA MKAKATI HUO, AFYA YA LWAKATARE YAZIDI KUDOROLA
WAKATI
sakata la Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare anayetuhumiwa kupanga mikakati ya
uhalifu na kurekodiwa kwa video likizidi kuibua maswali, vigogo wengine
wanadaiwa kuandaliwa mpango wa kurekodiwa kwenye video ili kuwachafua
na kuwanyamazisha, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Vigogo
hao ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald
Mengi, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Taarifa
za mkakati huo zilisambazwa jana kwenye mtandao maarufu wa Jamii Forum,
huku ukihusisha mawasilino ya ofisa mmoja wa Ikulu ya Rais Kikwete
akieleza kufurahishwa kwake na kuwapongeza waliofanikisha mpango wa
kuandaa video ya Lwakatare ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la
Polisi.
AZAM FC YAMJIBU SHAFFIH DAUDA
UONGOZI
WA SSB na Azam FC umesikitishwa na makala iliyotolewa na Blogu ya
Shaffihdauda eti, klabu zimekuwa zikidhulumiwa na SSB na Azam FC kwa
mechi zao kurushwa Live na Star TV.
Tungependa
ieleweke kuwa Azam FC ingependa kuona mashabiki wake nchini na nje ya
nchi wakiiona mechi live na ndiyo maana tumekuwa tukilipia matangazo
hayo, pia tunadhani hili ni jambo jema la kuungwa mkono na wadau.
Pia
tungependa ifahamike kuwa kwenye kipengele cha mkataba kati ya SSB na
Star TV, kuna kipengele kinachoilazimisha Star TV kutoa sehemu ya pato
lake na kuvilipa vilabu ambapo kwa mechi moja klabu hupata shilingi
milioni moja (1,000,000)
Kwa
mechi zinazochezwa chamazi, klabu hupata mgao wa kiingilio wa chini ya
shilingi laki tatu hivyo nyongeza ya milioni moja kwa mechi kurushwa
live ni pesa ya kutosha angalau kwa kuanzia
Dk. Slaa aivuruga CCM
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) kimesema kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba kuna baadhi ya
watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake, kimesababisha baadhi ya
wananchi kukosa imani na vyombo hivyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkoa Maalum wa CCM Dar es Salaam baada ya kikao
chao kutathimini mambo na matukio mbalimbali yanayolitikisa taifa kwa
sasa.
Katika
taarifa yao iliyosainiwa na Katibu wa Wilaya ya Dar es Salaam (ya
kisiasa - CCM), Daniel Zenda ilisema kuwa Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli
hizo mara kwa mara tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2010, lakini
hajaitwa kuulizwa wala kuchukuliwa hatua.
“Lakini
pia kauli ya Dk. Slaa imesababisha wananchi wakose imani na Idara ya
Usalama na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na
kuwahakikishia usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la
serikali,” ilisema taarifa hiyo.
Rais Kikwete apokea Ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Botswana.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa
Botswana uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe
Pandu Skelemi Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa
Botswana uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe.
Pandu Skelemi Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Botwana
Mhe Pandu Skelemi baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa
nchi hiyo jana Ikulu jijini Dar es salaam.(PICHA NA IKULU).
Papa Francis akataa vitu vya kifahari
Siku
chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki
duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa kuvaa viatu
vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia makasisi
watakaotenda uovu.
Papa Francis 1
Tayari,
Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi asiyetaka makuu, mhafidhina na
mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika kanisa hilo lenye waumini
bilioni 1.2 duniani.
Katika
siku mbili za uongozi wake, Papa Francis amelithibitisha hilo kwa
kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi, vyeusi na kuachana na
vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na mtangulizi wake, Benedict
VXI.
Kutoka Uk 1
Katika uongozi wake, siku zote Papa Benedict, alivaa viatu vyekundu vilivyotengenezwa kwa mkono, jambo ambalo Papa Francis anaonekana kuachana nalo.
Watu
walio karibu naye Papa Francis, wanaeleza kuwa kabla ya kuondoka
Buenos Aires, Argentina kwenda Rome, Kardinali Jorge Mario Bergoglio,
kama alivyojulikana awali, alivaa viatu rahisi vya rangi nyeusi, na
kuwafanya marafiki zake, wakiwamo mapadri kutaka kumnunulia viatu
vingine vipya.
“Siku ile aliyoondoka mjini Buenos Aires kuelekea Rome kwa ajili ya mkutano wa uchaguzi wa Papa (conclave), marafiki zake walimpa zawadi ya viatu. Yeye, siku zote amekuwa akitokea hadharani akiwa amevaa nguo rahisi, viatu vya kawaida,” walieleza mapadri hao kutoka Amerika Kusini walipozungumza na Kituo cha Redio Vatican.
Mbele ya makardinali 106
Juzi
Ijumaa alipokutana na makardinali 106, kiongozi huyo mwenye umri wa
miaka 76, licha ya kuonyesha uso wa furaha na kuwatania aliwaonya
makardinali hao kuhusu wajibu wao kama viongozi wa kanisa maeneo
mbalimbali duniani akiwataka kutosahau kuwa hawarudi kwenye ujana.
Katika ukumbi wa Sala Clementina, ulioko Vatican Papa Francis pia aliwataka makardinali hao wakiwamo waliomchagua kuwategemea zaidi vijana aliosema ndio nguzo kuu muhimu ya ustawi wa Kanisa Katoliki, huku aliwashauri makardinali kusaka njia sahihi ya kueneza Ukristo pande zote za uso wa dunia katika karne ya 21.
Aidha,
alimsifu mtangulizi wake, Papa Benedict kwa uamuzi wa kijasiri wa
kustaafu, akieleza kuwa ni uamuzi wa busara, wenye kuonyesha ukomavu na
kuwataka wasichoke kuiga matendo mema.
Yaliyomo kitabuni mwake
Msimamo kuhusu makasisi
Katika kitabu hicho, Papa Francis anazungumzia maisha ya utauwa (usafi wa moyo), uadilifu na maovu akiweka wazi msimamo wake usio wa mzaha na kuruhusu mijadala baina ya makundi ya imani tofauti, msimamo ambao unaweza kupingwa na baadhi ya Wakatoliki wenye msimamo mkali.Kwa maneno yake, Papa Francis anaonyesha kuwa mtu mwenye akili, anayefikiri haraka, mjuzi wa mambo, anayechanganya uhafidhina wa kijamii na akiwa mwenye msimamo mkali wala kutokukubali upuuzi kwa mambo asiyoyapenda au kuyakubali.
Kiongozi huyo ameahidi kutumia Jumamosi ya Machi 23 kumtembelea mtangulizi wake, Papa Benedict katika jumba analoishi huko Castel Gandolf, kusini mwa Rome na anaeleza kuwa kanisa limepitia nyakati ngumu. “Kumekuwa na vipindi vingi, majaribu mengi. Kumekuwa na vipindi vigumu, lakini, kanisa limesimama imara.”
“Ni dhahiri kuwa katika historia yake, kanisa limebadilika mno, sioni sababu za kwa nini tusikubali mabadiliko na kuwa utamaduni wetu wa sasa,” anaeleza.
Kupitia
kitabu, On Earth and Heaven (Duniani na Mbinguni) alichokiandika akiwa
kardinali, Papa Francis alitoa taswira yake kama mtu mwenye dhamira
safi hasa katika masuala ya kusaidia jamii, muumini thabiti anayeamini
katika majadiliano baina ya makundi ya imani tofauti.
Msimamo kuhusu makasisi
Papa
Francis ameonyesha wazi kuchukizwa na matendo ya makasisi (mapadri)
wasio waadilifu, ambao kwa miaka mingi wamelifedhehesha kanisa na
kwamba yeye hakubaliani na wanaoficha maovu ya baadhi ya mapadri
ukiwamo ulawiti.
“Suala
la useja (mapadri kutokuoa) kwamba ndicho chanzo cha ulawiti linaweza
kusahaulika,” anaeleza katika kitabu hicho. “Endapo padri ni mlawiti,
alikuwa hivyo hata kabla ya ukasisi wake. Lakini, hili linapotokea,
lisiangaliwe kwa mtazamo tofauti, lisifichwe.
Kama kiongozi, hutakiwi kutumia madaraka yako kuangamiza maisha ya mwingine.”
Kama kiongozi, hutakiwi kutumia madaraka yako kuangamiza maisha ya mwingine.”
Kuhusu
hatua gani atachukua, wakati akiwa Kardinali Bergoglio, alijibu kuwa
hawezi kukubaliana na waovu, lakini alipoulizwa kama askofu angechukua
hatua gani dhidi ya mapadri wa aina hiyo, alijibu,” Nitamfukuza kazi,
kisha kumshtaki, jukumu langu ni kuweka usafi wa kanisa mbele.
“Hili
ni suluhisho kwa matukio kama hayo kama jinsi ilivyopendekezwa
Marekani; lakini si kuwahamisha wakosaji kutoka parokia moja kwenda
nyingine.
“Huu ni upuuzi, kwani hata huko wataendeleza tatizo hilo. Jibu sahihi kwa tatizo hili ni kutowavumilia.”
Katika kitabu hicho, Papa Francis anazungumzia maisha ya utauwa (usafi wa moyo), uadilifu na maovu akiweka wazi msimamo wake usio wa mzaha na kuruhusu mijadala baina ya makundi ya imani tofauti, msimamo ambao unaweza kupingwa na baadhi ya Wakatoliki wenye msimamo mkali.Kwa maneno yake, Papa Francis anaonyesha kuwa mtu mwenye akili, anayefikiri haraka, mjuzi wa mambo, anayechanganya uhafidhina wa kijamii na akiwa mwenye msimamo mkali wala kutokukubali upuuzi kwa mambo asiyoyapenda au kuyakubali.
Kiongozi huyo ameahidi kutumia Jumamosi ya Machi 23 kumtembelea mtangulizi wake, Papa Benedict katika jumba analoishi huko Castel Gandolf, kusini mwa Rome na anaeleza kuwa kanisa limepitia nyakati ngumu. “Kumekuwa na vipindi vingi, majaribu mengi. Kumekuwa na vipindi vigumu, lakini, kanisa limesimama imara.”
Hata
hivyo, katika misa yake ya kwanza, Alhamisi, Papa Francis alieleza
kuwa kanisa hilo halina budi kwenda na wakati, kukubali mabadiliko.
“Ni dhahiri kuwa katika historia yake, kanisa limebadilika mno, sioni sababu za kwa nini tusikubali mabadiliko na kuwa utamaduni wetu wa sasa,” anaeleza.
Alieleza kuwa mafundisho ya msimu ya Kikatoliki, msimamo kuhusu mashoga, ndoa za jinsia moja, hayawezi kubadilika.
Pia, anaeleza kuwa utoaji mimba ni tatizo la kisayansi zaidi, lakini ambalo haliwezi kukubaliwa na kanisa.
Kuhusu
utandawazi, Papa Francis alieleza kwamba hakubaliani nao kwa kuwa
mfumo huo hauheshimu tamaduni. “Aina ya utandawazi unaofanya vitu vyote
kuwa sawa ni aina ya unyama,” anaeleza akiongeza kwamba tofauti za
kitamaduni hazina budi kudumishwa.
“Hatimaye, utandawazi unageuka njia ya kuwatumikisha wengine,” alisema.
BALOZI KAMALA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UHOLANZI
Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Uholanzi (TANE), Bw. Musuto
wa Chirangi (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Balozi
Kamala.Mwenyekiti wa TANE, Bw. Kweba Bulemo (aliyesimama Kulia), akisema machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Balozi.
Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe Atua Shinyanga, tayari kuzindua Kanda ya Ziwa Mashariki
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,
akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kakola, mahali
ambapo mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unapatikana, Emmanuel Bombeda
anayetokana na chama hicho, wakati kiongozi huyo mkuu wa CHADEMA
alipokuwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho, baada ya
kuwasili mkoani Shinyanga, kwenye kikao cha Baraza la Uongozi Kanda ya
Ziwa Mashariki (Mara, Shinyanga na Simiyu). Mbowe anatarajiwa kufanya
mkutano wa hadhara Mjini Shinyanga, kufanya uzinduzi wa kanda hiyo.
Saturday, March 16, 2013
HEBU ANGALIA WASANII TUNAOWAITA KIOO CHA JAMII
Kuna msemo
unasema wasanii kioo cha jamii je ni kweli?hili ni kava linalobeba kazi
za wasanii kwa hali kama hii bado tunadhubutu kusema wasanii ni kioo cha
jamii? Mimi naona waitwe waharibifu wa jamii kwa halii hii. Hapa watoto wanajifunza nini kwa kweli?
MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOGIA
Rapper
Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea
siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili
wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa
mfumo wa digitali unawaumiza.
Akiongea
na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa
na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika
kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye
ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza
kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali
itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama
hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.
Subscribe to:
Posts (Atom)