Thursday, March 07, 2013
WAUGUZI MOROGORO WAPOKEZANA KUWASHIKIA DRIPU WAGONJWA BAADA YA KUKOSA VITANDA
BAADHI
ya wananchi wa mkoani MOROGORO wameshangaza na kitendo cha waunguzi
wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,kupokezana kuwashika madripu ya
dawa wagonjwa waliolaza chini ya wodi za hospital hiyo ya rufaa nya
mkoa wa Morogoro baada ya kukosa vitanda.
.
Skendo zinazidi kuiandama hospital
hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa hospital ya rufaa hivi karibuni
ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top redio ya mkoani hapa Edward
Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimwizwa kwenye hospital hiyo
imeilalamikia hospital hiyo kwakumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi
ya masaa matano na kuladhimika kuondoka kwenye hospital hiyo ya serikali
na kwenda kutibiwa hospital za watu binafsi.
Mtandao huu umeibua Skendo
nyingine ndani ya hospital hiyo baada ya kushuhudia waunguzi wa hospital
hiyo wakipokeza kuwashikia madripu ya dawa wagonjwa waliolazwa chini
ya sakafu baada ya hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
Juzikati
hospital hiyo ilivamiwa na majeruhi zaidi ya 60 waliopoteza fahamu
baada ya kiwanda cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na
shoti ya umeme na kukimbizwa kwenye hospital hiyo,hivyo uongozi wa
hospital hiyo baada ya kuelemewa na wingi wa majeruhi hao ulilazimia
kutoa magodoro stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kufuatia
hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.
" Hii ni aibu kubwa kwa hospitali ya
rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba
wagonjwa wamekuja kwa mkupo. hospital inapopewa hadhi ya rufaa inamaana
inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi
zaidi ya mia watakaofika kwa mkupuo kwenye hospital hiyo"alisema Bi Asha
Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao.
Vile vile mwandishi wa matandao
huu mbali ya kushudia wauguzi hao wakipokezana kuwashikia madripu
wagonjwa hao pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kupita juu ya
wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo
Ili kupata ufafanuzi wa jambo
hilo Mtandao huu ulimsaka Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo kwa zaidi ya
siku tano na kufanikiwa kumpata leo asubuhi ambapo alipotakiwa kueleza
hali hiyo Mganga huyo mfawidhi Bi Rita Lyamuya alikuwa na haya ya
kusema
" Nikweli siku ile ya tukio la
kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya
majeruhi .kiukweli kwa ishu kama ile tulikosa namna ya kukabiliana
nayo kwani walikuja kwa mkupua zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya
tuliwapokea na baadhi kuwalaza chini na kuwapatia hudumu ya kwanza huku
tukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza"alisema Dr Rita
dustanshekidele blog
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA UKOSEFU WA VYOO
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WAKIWA DARASANI HUKU DAWATI MOJA WAKIWA WAMEKALIA WANAFUNZI WATANO |
HII NDIYO HALI HALISI YA VYOO HIVYO KWAKWELI NI HATARI KABISA VIPI WAHUSIKA MPOOO NA MNALIONA HILI? |
HIVI NI VYOO VYA WAALIMU WA SHULE HIYO |
WANAFUNZI SASA HUJISAIDIA KATIKA VICHAKA HIVI KWAKWELI HATARI SANA KUKUTANA NA NYOKA NA WADUDU WENYE SUMU KALI |
PICHA NA KAMANGA MBEYA |
CHADEMA WAZUA GHASIA MAZISHI YA MOLLEL
Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya
aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung’oa
bendera za chama hicho na kuamsha hasira za
waombolezaji wafuasi wa chama tawala.
Mollel
alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden
Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM
walionekana wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema.
Mashuhuda
walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi
wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo
msibani na hivyo kuanza kuzing’oa.
Matatizo ya mitambo ya uchaguzi Kenya
Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais nchini
Kenya, ilisimamishwa usiku kucha kwa sababu ya hitilafu za mitambo ya
tume huru ya uchaguzi na mipaka iliyokuwa inatumika kwa mara ya kwanza
katika uchaguzi wa Kenya.
Maafisa wa tume hiyo, wamelazimika kusafiri kwa
barabara kutoka umbali wa maelfu ya kilomita ili kwenda katika kituo cha
kutangazia matokeo ya kura za urais mjini Nairobi kuwasilisha fumo zao
za matokeo.Maafisa wa uchaguzi wametoa wito wa utulivu na amani kwa wakenya wakati tume ikiendelea kutatua tatizo la kura.
Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,ambaye anatakikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, miaka mitano iliyopita, angalia yuko mbele katika matokeo ya uchaguzi wa urais.
Kufikia sasa asilimia 42 ya kura za urais nchini Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa rasmi kwa tume ya uchaguzi IEBC kupitia mitambo ya electroniki.
Hata hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha kura kutokana na hitilafu ya mitambo.
Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia uongozi huku kura za urais zikiwa bado zinahesabiwa.
Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007/2008 kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenyatta aliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya matokeo ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake waziri mkuu Raila Odinga katika siku ya pili ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi ya masaa 36 baada ya shughili ya upigaji kura kukamilika.
Hadi sasa Uhuru ana kura milioni mbili nukta nane wakati Raila Odinga akiwa na kura milioni mbilii nukta mbili
Raila Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka 2007 wakati matokeo yalizua ghasia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja huku maelfu wakiachwa bila makao
Wakati mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura kwa amani siku ya Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura ndio itakuwa ishara ya uthabiti wa nchi hiyo.
Ni asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa huku kukiwa na vituo zaidi ya elfu thelathini ambako kura zilipigiwa.
Ni zaidi ya kura milioni tano zilizohesabiwa kutoka kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.
UN, ''Mauaji ya Albino yaongezeka Tanzania''
Kamishna Mkuu wa haki za
binadamu katika Umoja wa Mataifa,Navi Pillay, amelaani mashambulizi
mabaya yaliyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino nchini
Tanzania ikiwemo mauaji ya mtoto mvulana.
Serikali inapaswa kukomesha mauaji hayo pamoja na unyanyapaa dhidi yao , alisema Bi Pillay.Taarifa zinazohusiana
Watu watano pekee wameshtakiwa mahakamani nchini Tanzania, tangu mwaka 2000 kwa mauaji ya maalbino.
Takriban wengine 72 waliuawa katika kipindi hicho.
Mnamo mwaka 2009, rais Jakaya Kiwete, alisema kuwa mauaji hayo yaliiletea Tanzania aibu kubwa na kulazimu nchi hiyo kufanya kampeini ya kitaifa ili kukomesha dhulma hizo dhidi ya maalbino.
Mnamo mwaka 2010, Salum Khalfani alikuwa mtu wa kwanza mwenye ulemavu huo kuchaguliwa kama mbunge nchini Tanzania.
Bi Pillay alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama mtu yeyote ule bila hofu ya kuuawa au kubaguliwa.
Katika taarifa yake, Bi Pillay alisema kuwa mashambulizi manne ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi, yaliripotiwa katika siku kumi na sita kati ya mwezi Januari na Februari.
Ni pamoja na mauaji ya mtoto mwenye miaka saba, Lugolola Bunzari. Watu walimvamia walikata paja la uso, mkono wake wa kulia , bega la kushoto.
Babu ya kijana huyo, mwenye umri wa miaka 95, pia aliuawa kwenye shambulizi hilo, alipojaribu kumuokoa mjuu wake.
Bi Pillay alisema mashambulizi kama haya ni mabaya na watu wana haki ya kuishi kama watu wengine bila hofu ya kuuawa au kujeruhiwa vibaya.
NSSF YABISHA HODI KIGOMA VIJIJINI
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwasili katika Kijiji
cha Matyazo wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa
Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Hamis Betese akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini.
Baadhi ya wanakijiji cha Matyazo pamoja na vijiji vya jirani wakiwa katika uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma za kitamaduni cha Changamoto kikitoa burudani.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kujiandikisha kwa hiari kwa wanachama wa NSSF, wakulima
wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. Zaidi ya Wanachama 500
wameandishwa Uanachama wa Hiari wa NSSF katika Kata ya Kalinzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Ramadhani Maneno akizungumza wakati wa Uzinduzi huo.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akizungumz wakati wa
uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa
Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini.
Wanakijiji wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Matyazo, Rusaba na Makabogo wakiwa katika hafla hiyo.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Mseli Abdalah akiongoza hafla hiyo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akizungumza wakati wa uzinduzi.
Kikundi cha Ngoma cha Changamoto kikitoa burudani.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya
Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Mary
Wilfred wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya
Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Meckrinda Enock wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akipokea zawadi ya Kahawa kutoka
kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akipokea zawadi ya Kahawa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari MahwisaMwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja Kiongozi, Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akifurahia zawadi ya Kahawa mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.
Wednesday, March 06, 2013
Cardinal impostor caught sneaking into Vatican conclave
SINSATIONAL: Bogus “Bishop” Ralph Napierski slips a fast one by Sergio Cardinal Sebastiani yesterday.AFP/Getty Images
A bogus bishop nearly sneaked into the closed-door Vatican meeting of
the world’s cardinals yesterday as they prepared to choose the next
pope.
“Bishop Ralph Napierski” got past a checkpoint of Swiss
Guards and was photographed shaking hands with Sergio Cardinal
Sebastiani in the cobblestone square to the left of St. Peter’s
Basilica.
But Napierski never made it inside the Pope Paul VI
Audience Hall, where more than 140 cardinals from around the world were
having their first formal meeting since the resignation of Pope Emeritus
Benedict XVI.
Well, his cassock was several
inches too short. His crucifix looked odd. His purple sash was obviously
a scarf. And instead of wearing a zucchetto — the familiar
ecclesiastical skullcap of bishops — he had a black, brimmed fedora.
Before
he was hustled out of the area near St. Peter’s Square by Swiss Guards,
Napierski told reporters that he was “Basilius” of the Italian Orthodox
Church — which doesn’t exist.
He added that he was a founder of
the Corpus Dei order — another imaginary group — and he complained that
Catholic bishops had “made a mistake by moving priests” who were accused
of sexual abuse from parish to parish.
Napierski, believed to be
an Italian living in Germany, has a bizarre Web site in which he said he
was “a slave and apostle like St. Paul” and came from “a tribe of the
Roman Catholic Church” that is fighting “heresy and false movements”
inside the church.
Vatican spokesman Rev. Federico Lombardi said he had no information about the incident.
Vatican
officials said 107 of the 115 cardinals eligible to vote for pope
attended yesterday’s meeting, but no date for the papal conclave will be
set until all are in attendance.
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam lawashikilia watu wanne kwa tuhuma za uchochezi wa kidini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni ACP Charles Kenyela.
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujishughulisha na uchochezi wa kidini.
Watu
hao wamekamatwa hivi karibuni katika msako maalum unaoendeshwa na Jeshi
la Polisi Kanda Maalum katika hali ya kukabiliana na uchochezi wa
kidini ambao lengo lake ni kuleta chuki pamoja na ubaguzi wa kidini
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleimani Kova amewataja watu hao
kuwa ni Kombo Hassan Zuberi mkazi wa Mburahati Barafu (32), Basote
Hassan Tandala Rayan mkazi wa Gongo la mboto (24), Mohamed Hassan Sharif
mkazi wa Tabata Bima(33) na Salum Athman Mahambi mkazi wa Tunduma(46).
Aidha
Kamanda Kova ametoa onyo kali kwamba Jeshi la Polisi halitasita
kuwachukulia hatua wale wote wanaoleta uchochezi kupitia shughuli za
kidini au kisiasa.
TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUMUENZI STEVEN CHARLES KANUMBA
WASANII wa filamu Tanzania wapo katika harakati za mwisho wa mchakato wao katika maandalizi ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni moja ya jambo walilokusudia kuhakikisha wanamuenzi na kuthamini mchango aliouacha kwenye tasnia ya filamu
Akizungumzia maandalizi hayo jijini Dar es Salaam rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba alisema kuwa baadhi ya maandalizi yameanza kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba, huku wakishirikiana na familia ya marehemu ili kuweka mipango ya nini kifanyike katika harakati za kutimiza lengo
Alisema kuwa lengo lao lazima litimie kwa sababu walikusudia kufanya kitu kwa ajili ya kumuenzi marehemu kutokana na mchango wake aliouacha kwenye filamu na ili kudhihirisha hilo wanaamua kumenzi katika hali ya kiupekee
"Lazima tufanye kitu cha tofauti katika kumuenzi marehemu na ili tuonyeshe upendo wetu lazima tuheshimu kile alichokiacha kwa kuendeleza" alisema Mwakifwamba
Aliongozea kuwa muda ukifika na maazimio yakipitishwa ndipo ataweka wazi ni jambo gani lililokusudiwa kufanyika
Marehemu Steven Kanumba amefariki april 7 mwaka 2012 ambapo chanzo cha kifo chake kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa mapenzi, na aliyekuwa mpenzi wake msanii mwenzie wa filamu Lulu
Mwigizaji Matumaini Aomba Msaada wa Matibabu Serekalini
KOMEDIANI
maarufu Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ ameiomba serikali imsaidie
kupata matibabu ili aweze kupona maradhi ya figo na ini yanayomkabili.
Akizungumza na Tollywood Newz
jijini Dar es Salaam alisema: “Hali yangu bado si nzuri ingawa natumia
dawa lakini sijapata tiba sawasawa. Sina fedha na familia yangu kwa sasa
imeishiwa kwa sababu magonjwa yanayonisumbua ni makubwa na yanahitaji
fedha nyingi.
“Naiomba serikali kupitia Wizara
ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo isikie kilio changu. Hali yangu
si nzuri, nahitaji msaada ili kuokoa maisha yangu. Nina imani nikipata
tiba kamili nitapona na kurejea tena jukwaani.”
DIAMOND HUWA ANAPENDELEA KUFANYA HIVI AKIWA NYUMBANI
With My Homeboy Abou.....!! |
RAIA WA UGANDA WAFUNGA NDOA YA JINSIA MOJA
Lawrence na jimmy raia wa uganda ila wanaishi Sweden wamefunga ndoa ya jinsia moja daaaah!! aibu tupu je ungekuwepo we ungefanya nini hapo... watu wanasheherekea kabisaaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)