Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais nchini
Kenya, ilisimamishwa usiku kucha kwa sababu ya hitilafu za mitambo ya
tume huru ya uchaguzi na mipaka iliyokuwa inatumika kwa mara ya kwanza
katika uchaguzi wa Kenya.
Maafisa wa tume hiyo, wamelazimika kusafiri kwa
barabara kutoka umbali wa maelfu ya kilomita ili kwenda katika kituo cha
kutangazia matokeo ya kura za urais mjini Nairobi kuwasilisha fumo zao
za matokeo.Maafisa wa uchaguzi wametoa wito wa utulivu na amani kwa wakenya wakati tume ikiendelea kutatua tatizo la kura.
Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,ambaye anatakikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, miaka mitano iliyopita, angalia yuko mbele katika matokeo ya uchaguzi wa urais.
Kufikia sasa asilimia 42 ya kura za urais nchini Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa rasmi kwa tume ya uchaguzi IEBC kupitia mitambo ya electroniki.
Hata hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha kura kutokana na hitilafu ya mitambo.
Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia uongozi huku kura za urais zikiwa bado zinahesabiwa.
Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007/2008 kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenyatta aliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya matokeo ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake waziri mkuu Raila Odinga katika siku ya pili ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi ya masaa 36 baada ya shughili ya upigaji kura kukamilika.
Hadi sasa Uhuru ana kura milioni mbili nukta nane wakati Raila Odinga akiwa na kura milioni mbilii nukta mbili
Raila Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka 2007 wakati matokeo yalizua ghasia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja huku maelfu wakiachwa bila makao
Wakati mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura kwa amani siku ya Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura ndio itakuwa ishara ya uthabiti wa nchi hiyo.
Ni asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa huku kukiwa na vituo zaidi ya elfu thelathini ambako kura zilipigiwa.
Ni zaidi ya kura milioni tano zilizohesabiwa kutoka kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.