Rais
mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa
na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa
linalokabili nchi.
Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo
mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya
dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.
"Kwa ushirikiano
na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira
ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi
zaidi kukabiliana nao."
Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha
msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa
nchi hiyo kuwa wavumilivu.
"Tumebaini matatizo makubwa matatu.
Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja
analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa
uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe.
Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba
ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika
kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada
ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka
kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."
Anasema rais huyo
mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.