Thursday, April 02, 2015

BUHARI AAHIDI KUTOKOMEZA BOKO HARAM NIGERIA

Muhammadu Buhari, Rais mteule wa Nigeria
Rais mteule wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amezitaja vurugu zinazosababishwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwa ni tatizo kubwa linalokabili nchi.

Katika mahojiano maalumu na BBC, kiongozi huyo mstaafu wa jeshi amesema anatarajia kulishinda kundi hilo baada ya dhamira mpya kutoka jeshini na msaada wa nchi jirani.

 "Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."

Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.

"Tumebaini matatizo makubwa matatu. Ambayo ni kukosekana kwa usalama nchini, tatizo ambalo kila mmoja analifahamu na lingine ni ukosefu wa ajira, hii ina maana uharibifu wa uchumi ikiwa ni kutokana na vitendo vya rushwa na rushwa yenyewe. 

Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria, wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi, miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii."

 Anasema rais huyo mteule wa Nigeria. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, March 27, 2015

GWAJIMA ASAKWA NA POLISI KWA KUMKASHIFU KARDINALI PENGO

GWAJIMA
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Hatua hiyo ya polisi imekuja baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko, ambapo inadaiwa Mchungaji Gwajima alitoa lugha ya kashfa dhidi ya Kardinali Pengo ambaye alipinga tamko lililotolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) la kuipigia kura ya Hapana Katiba Inayopendekezwa.


Taarifa iliyotolewa jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kamishna Suleiman Kova, imemtaka Mchungaji Gwajima kujisalimisha haraka katika Kituo cha Polisi cha Kati kwenye Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

JK ATEUA WABUNGE WAPYA

rais-kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amewateua Dk. Grace Puja na Innocent Sebba kuwa wabunge wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, ilisema uteuzi huo unatokana na mamlaka aliyopewa rais na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e).


Alisema ibara hiyo, inampa mamlaka rais ya kuteua wabunge wasiozidi 10 na kwamba uteuzi wa wabunge hao ulianza Machi 20, mwaka huu. Kibanga alisema kuteuliwa kwao kumekamilisha idadi ya wabunge ambao rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kikatiba.


Alisema awali Rais Kikwete aliwateua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Asha Rose Migiro (Waziri wa Katiba na Sheria), Saada Salum Mkuya (Waziri wa Fedha) na Janeth Mbene (Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara).


Wengine walioteuliwa awali ni Profesa Sospeter Muhongo, Shamsi Vuai Nahodha, Zakhia Meghji na Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 27, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KILIMANJARO KINARA WA POMBE YA VIROBA


Mji wa Moshi, Tanzania

 Utafiti mpya umebaini kuwa wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa unywaji wa pombe  hasa ya  viroba,  ikiwa ni mara nne zaidi ya wakazi wanaokunywa pombe katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Katika utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiri wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kupitia mradi wa Strive ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanaokunywa pombe ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24.

Utafiti huo wa NIMR ulilenga kujua ukubwa wa Matumizi ya Pombe kwa vijana  katika mikoa ya  Kilimanjaro, Mwanza, Geita na Kahama umebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza  kwa unywaji wa pombe kwa vijana wenye umri kutokana na utamaduni uliopo mkoa huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIL WAYNE AMTANGAZA CHRISTINA MILIAN KUWA MPENZI WAKE MPYA

lil-wayne na mpenzi wake christina-milian
BOSI wa kundi la Young Money, Lil Wayne, amemuweka wazi mpenzi wake mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo analoliongoza.
Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter, aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”
Wayne ni baba wa watoto watano, na sasa yeye, mpenzi wake huyo na mtoto wake wa kwanza, Regina aliyezaa na mama mwingine wanafanya kazi pamoja katika kundi hilo.

Thursday, March 26, 2015

LOWASSA AKUBALI YAISHE URAIS CCM

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa
Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa

SIKU moja baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kumuonya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, kwa tuhuma za kukiuka Katiba na kuanza kampeni za Urais kabla ya muda, kiongozi huyo ameibuka na kudai kuwa hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais.
Pia Lowassa ametumia nafasi hiyo na kuwaomba wale wote ambao bado wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza hadi pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.
Akizungumza na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya waliokwenda pia kumshawishi agombee nafasi hiyo, mjini Dodoma jana, alisema si vyema kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama wao kwenye vyombo vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Alisema watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa na kwamba walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa mkoani Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.
Alisema katika siku hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania wawashawishi viongozi wanaoona wanafaa ili wajitokeze kugombea nafasi hiyo ya Urais. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MACHI 26, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
..


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'VIJANA WENGI HAWANA NGUVU ZA KIUME'

Dk. mwele 
Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),imesema vijana wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea, wanaongoza kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela alisema kwa sasa tatizo hilo ni kubwa ambalo linawakumba vijana wengi hususan barani Afrika.
Alisema hali hiyo,imesababisha vijana hao kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya Mundex, AAili waweze kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Vijana wengi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo limewafanya kutafuta dawa za kuongeza nguvu ili waweze kuzitumia na kupunguza ukubwa wa tatizo.
“Tangu tugundue dawa hii, idadi kubwa ya wanaokuja kununua ni vijana hasa wenye umri wa miaka 30, hali ambayo inaonesha wazi kuwa tatizo hili linakua kwa kasi,” alisema Dk Mwele.
Alisema kipindi kilichopita, matatizo hayo yalikuwa yanawapata wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea, lakini sasa hivi ni tofauti kabisa ambapo vijana wenye umri huo ndiyo wenye matatizo hayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ASKARI WAWILI MBARONI KWA FEDHA BANDIA


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo akionyesha sare za jeshi la wananchi zilizokamatwa kutoka kwa askari polisi baada ya kupekuliwa nyumbani kwake. 

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa wa Old Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.

Alisema askari hao walifika kwenye kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki aina ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo katika simu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...