Polisi
mkoa wa Dodoma nchini Tanzania wanawashikilia wahamiaji haram 64 raia
wa Ethiopia, huku mmoja wao akipatikana akiwa amekufa.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Dodoma amenukuliwa akisema wanamshikilia dereva wa gari
lililokuwa limewabeba watu hao ambao inaaminika walikuwa njiani kuelekea
kusini mwa Afrika.
Hii si mara ya kwanza kwa wahamiaji wa aina hiyo kukamatwa katika mazingira hayo.
Mwaka
2012 watu 42 kutoka Eritrea walikutwa wamekufa katika lori mkoa wa
Dodoma kwa kile kinachosemekana ni kukosa hewa kutokana na kufichwa
ndani ya lori hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.