Meya wa Manispaa ya Tabora, Gullam Hussein Dewji akizungumza na
waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana, baada
ya kutoka kwenye Baraza ka Maadili ya Viongozi, alikoitwa kuhojiwa
kuhusu tuhuma za kujilimbikizia mali na matumizi mabaya ya madaraka.
Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam
Hussein Dewji ameshushiwa tuhuma nzito za kuidanganya Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushindwa kutangaza mali anazozimikiki
zikiwamo pikipiki 422, licha ya kutakiwa kufanya hivyo kisheria.
Sheria Namba 5 ya mwaka 2001 ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, inamtaka kila kiongozi kujaza fomu za kutangaza mali
zake na madeni na kuziwasilisha kwenye Sekretarieti hiyo kila mwisho wa
mwaka.
Meya huyo alisomewa mashtaka yake jana na
Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude
Cyriacus mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma,
Jaji Mstaafu Hamisi Msumi.
Mwanasheria huyo alisema kuwa meya huyo
anatuhumiwa kutotamka baadhi ya mali anazozimiliki na kuzitaja mali hizo
kuwa ni pikipiki 422, magari matatu, viwanja vitano na nyumba moja.
Cyriacus alisema kwamba meya huyo alishindwa kutangaza mali zake katika kipidi cha miaka minne, kuanzia mwaka 2010 hadi 2013. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz