Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imetoa vibali vya ajira 10,184 kwa mamlaka za serikali za mitaa, sekretarieti za mikoa, wakala za serikali na taasisi na mashirika ya umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, amesema hayo leo katika kikao na watumishi wa umma wa Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
“Mgawo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki
Ameongeza kuwa taratibu za kukamilisha mgao wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kuziwezesha wizara na taasisi nyingine zilizokamilisha uhakiki wa watumishi wa umma hivi karibuni kuajiri watumishi wapya kuziba nafasi za wazi zilizojitokeza.