Tuesday, July 04, 2017

TIMU YA SINGIDA UNITED YAONESHA JEURI YA PESA, YANUNUA BASI LA MILLION 350/-

Baada ya kupata udhamini mnono kutoka katika kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa hatimaye klabu ya Singida United inazidi kutanua misuli yake katika ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kutambulisha usafiri wao utakao tumika katika kusafirishia wachezaji.
 Akizungumza na waandishi wa habari jana katibu Mwenezi wa klabu hiyo Festo Sanga amethibitisha Singida United kununua Basi jipya lenye gharama ya shilling milioni 350.

“Hili ni Basi aina ya Dragon ambalo limenunuliwa kwa fedha za klabu na linamilikiwa na Singida United hiyo ni moja ya jambo kubwa ambalo tunajivunia, kwa zipo timu ambazo mpaka sasa hazina usafiri lakini sisis kwa muda mfupi tunamiliki usafariki kama huu.
“Jambo la pili ni kuhusu maendeleo ya klabu , Singida United inatarajia kuanza kambi siku ya leo mkoani Mwanza na wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi hata mmoja na tuna wachezaji 23 mpaka sasa. Kati ya wachezaji has wachezaji kumi na moja ni wale waliopandisha timu na wachezaji sita ni wakimataifa.
“Uwanja wa Singida United unaendelea na ujenzi wake na tayari zimeshapandwa nyasi nyingine na zimeshaanza kuota kwa upande wa vyumba na majukwaa tayari na ujenzi umesimamiwa na Mkurugenzi wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa na matarajio yetu michezo yetu ya nyumbani tutatumia uwanja wetu wa nyumbani” amesema kiongozi wa Singida United, Festo Sanga.

Kiongozi huyo amewataka wadau wa mchezo wa soka nchini kutambua klabu hiyo haifungamani na upande wowote kati ya timu kubwa nchini za Simba na Yanga kama inavyovumishwa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...