Sunday, July 02, 2017

TRUMP: TUMECHOKA KUIVUMILIA KOREA KASKAZINI

Rais wa Marekani, Donald Trump amesisitiza kwamba muda wa kimkakati wa uvumilivu kwa Korea Kaskazini umekwisha.

Katika hotuba ya pamoja juzi, akiwa na mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae katika bustani ya Rose kwenye Ikulu ya White house, Trump aliahidi ‘kuchukua hatua madhubuti’ dhidi ya programu ya nyuklia na makombora ya Korea Kusini akisema vitisho vyake vinafaa kupatiwa majibu ya kijasiri.

“Hizi si zama za kuvuta subira juu ya Serikali ya Korea Kusini ambayo imeshindwa kutekeleza wajibu wake,” alisema Trump.

“Imechukua miaka mingi na imeshindikana, na kwa kweli hakuna kuvuta subira hivi sasa.” Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.

Kadhalika, Rais wa Korea Kusini amesema kwamba Taifa lake litaweka marekebisho ya kiusalama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.

Kiongozi huyo ameshauri kuwa ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.

Trump na Moon walitofautiana jinsi wanavyotakiwa kuweka shinikizo juu ya Korea Kaskazini ili iweze kuacha kabisa programu yake ya nyuklia.

Pia walikosoa baadhi ya maeneo ya ushirikiano wa nchi zao katika ulinzi. Hata hivyo, ilikuwa wazi kwamba nchi hizo mbili siku ya Ijumaa zilionyesha mshikamano na msimamo wa pamoja.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...