Friday, January 08, 2016

SAMATTA, AUBAMEYANG WATISHA TUZO ZA AFRIKA

Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika. Huku tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borusia Dotmund nchini Ujerumani.

Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.

Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon



Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Cote d’Ivorem


Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo.

Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo

Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon

Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia

Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...