Serikali
ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na
kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Akihutubia kikao cha
dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed
al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi
lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Waziri
huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje
wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa
kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment