Sunday, June 01, 2014

'JK VUA KOTI LA CCM, VAA LA UARAIS'




Mwenyekiti wa Kongamano la Katiba, Dk Ayub Rioba akizungumza na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mdahalo ulioandaliwa na Muungano wa Asasi za Kiraia (Azaki) uliofanyika Dar es Salaaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa utetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa na Awadhi Ally Saidi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya kukusanya maoni. Picha na Venance Nestory      

Dar es Salaam/Mwanza. Rais Jakaya Kikwete ameshauriwa kunusuru mchakato wa kupata Katiba Mpya ili usisimame kwa kuvua koti la Uenyekiti wa CCM na kubaki na Urais ili awaeleze wananchi nini cha kufanya kupata Katiba Mpya.
Ushauri huo umetolewa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na wasomi walioshiriki katika mdahalo wa Katiba uliofanyika jijini Dar es Salaam na Mwanza jana. Walisema kuwa Rais ana wajibu kuunusuru mchakato huo kwa kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga kwa hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge Maalumu la Katiba iliyoonekana kuelemea upande wa chama chake CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete amekuwa kigeugeu juu ya Muundo wa Serikali za Muungano kama zilizopendekezwa kwenye Rasimu ya Kwanza na ya Pili ya Katiba.
Alisema kuwa Rais Kikwete alionyesha wazi kukubaliana na Muundo wa Serikali tatu, kwani kabla Rasimu ya Pili ya Katiba haijapelekwa kwenye Bunge Malaumu la Katiba ili kujadiliwa, alisaini kuonyesha kuwa amekubaliana na yaliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Akihutubia kwenye Kongamano la Wazi na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine
cha Mwanza (Saut) Dk Slaa alisema:
“Rais Jakaya Kikwete amekuwa kigeugeu, kwani yeye ndiye aliyesaini Rasimu ya Pli ya Katiba ili ikajadiliwe kwenye Bunge Maalumu la Katiba.” Aliongeza: “Kwa kuwa ndiye mtu wa mwisho kuruhusu rasimu hiyo ijadiliwe kwenye Bunge Malaamu la Katiba ni wazi alikubaliana na kilichopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyopendekeza Muundo wa Serikali Tatu, hivyo inashangaza kuona leo anageuka na kutaka Serikali mbili.”
Dk Slaa ambaye pia ni kiongozi katika Umoja wa Katiba ya Wananchi Nje ya Bunge (Ukawa), alisema kuwa katika mikoa 17 waliyozunguka na kufanya mikutano na wananchi, wamebaini kuwa Rasimu ya Katiba ya Pili wananchi hawaifahamu na kwamba hiyo ni njia ya CCM kuchakachua maoni yao yaliyomo kwenye rasimu hiyo, wakati wa kupiga kura za maoni.
Alisema wanatambua ujanja unaofanywa na CCM kutaka kupitisha mambo wanayoyataka wao, lakini wao watendelea kuwaelimisha wananchi ili watambue kwamba maoni yao ndiyo nguzo ya kuwapa Katiba bora na siyo vinginevyo.
“Tumefanya mikutoano mikoa 17, lakini kote tulipopita wananchi wametuambia hawaifahamu Rasimu ya Pili ya Katiba kutokana na janja ya CCM kuficha rasimu ya hiyo ili wananchi wasiifahamu. Kutokana na hilo  ni wazi kwamba wanataka kuchakachua maoni ya wananchi kwenye kura za maoni,”alisema Dk Slaa.
Akinukuu maneno kutoka katika hotuba ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 Dk Slaa alisema: “Watu wapumbavu ni wale wanaoamini kwamba Katiba haibadiliki.”
Alisema lazima Katiba ibadilike na kwamba wananchi ndiyo wenye Katiba, hivyo siyo busara kutaka kuchakachua maoni yao na kuweka maoni ya chama au mtu binafsi.

“Watu wanamini kuwa Katiba haiwezi kubadilika, mimi naona ni upumbavu, kwani hata Mwalimu Nyerera aliwahi kusema hivyo kwenye hotuba yake ya mwaka 1995,” alisema Dk Slaa.


Tundu Lissu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema kuwa kuna mambo mema ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifanya na mengine ambayo siyo mema, hivyo Watanzania na wasomi wanapaswa  kuyachuja na kuyakataa mabaya na kuchukua mema.
Alisema katika mambo mabaya ambayo Mwalimu Nyerere aliacha ni pamoja na kuwarithisha Watanzania hofu, jambo alilosema hadi sasa limewatawala.
“Nyie kama wasomi wa Saut naomba niwaambie kwamba katika mambo mabaya ambayo Mwalimu Nyerere aliwarithisha Watanzania ni hofu, jambo ambalo hadi leo linaawatawala kwani Watanzania wengi wanaogopa kusema kwa kuhofu kufukuzwa kazi au vyuo, “alisema Lissu na kuongeza:
“Mmoja ya mfumo mbaya ambao Mwalimu Nyerere aliuanzisha baada ya kupata uhuru mwaka 1962 ni kuwaweka watu kizuizini. Hii ilikuwa inatokea kwamba unakamatwa na watu usiowajua na unawekwa kizuizini, ”alisema.
Kutoka Dar es Salaam, Muungano wa Asasi za Kiraia (AZAKI), umemtaka Rais Jakaya Kikwete kunusuru mchakato wa kupata Katiba Mpya usisimame ukieleza kuwa yeye ndiye aliyeuvuruga.
Akizungumza katika mkutano wa AZAKI, jijini humo aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, alisema kuwa mchakato mzima ulikwenda vizuri, lakini baada ya Kikwete kulihutubia Bunge Maalumu la Katiba, mwelekeo wa Bunge hilo ulibadilika.
Alisema kuwa Rais Kikwete alikwenda kulihutubia Bunge kama kiongozi wa CCM, badala ya kiongozi wa nchi, ambapo aliweka msimamo wa chama chake wa kutaka Muundo wa Serikali mbili. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
“Rais apate ujasiri akiwa kama kiongozi wa nchi na siyo kama kiongozi wa CCM, awahutubie wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na kuwataka wajadili Katiba ya wananchi na siyo ya chama wala yake binafsi,” alisema Baregu.
Aliongeza kuwa kama Rais hatalinusuru Bunge hilo na kila mtu akafanya anavyotaka au kwa masilahi ya chama chake kama ambavyo ameonyesha mfano, demokrasia nchini haitawezekana.
Baregu aliwataka wajumbe watumie miezi miwili iliyobaki kujipanga upya iwapo wana nia ya dhati ya kuendelea na mchakato huo, ili ipatikane Katiba bora ya wananchi akionya kwamba, tofauti na hapo Watanzania hawatakubali.

Kauli ya Baregu pia iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Sheria Zanzibar, Awadhi Ally Saidi ambaye ni pia ni miongoni mwa waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, aliyesema kuwa inafaa Rais awahutubie wajumbe na kuwakumbusha kuwa jukumu lao ni kujadili Rasimu ya Katiba ya kuipitisha na siyo kuondoa vipengele.
“Ndiyo maana walipewa siku 70 kujadili Rasimu ya Katiba, lakini walitumia siku 21 kutunga kanuni ambazo zilitungwa na Baraza la Wawakilishi likishirikiana na Bunge la Muungano,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...