Wednesday, August 07, 2013

SELLY AMUOMBA MSAMAHA MPENZI WAKE KWA KUFANYA MAPENZI NA NANDO NDANI YA BIG BROTHER


Hatimaye mshiriki wa Ghana katika reality show ya Big Brother ‘The Chase’ Selorm Galley maarufu kama Selly aliyetoka wiki moja iliyopita, amemuomba msamaha boy friend wake (wa Ghana) kwa yale aliyoyafanya mbele ya Camera za nyumba ya Big Brother.

Kupitia kipindi cha live ‘Celebrity Show’ cha ETV ya Ghana Selly ambaye pia ni muigizaji alianza kwa kumshukuru mpenzi wake Praye Tietia, na kutokana na kwamba kuna uwezekano yaliyomkwaza mpenzi wake ni mengi, Selly alimuomba msamaha kwa yale yote yaliyojiri mjengoni (ikiwemo kufanya mapenzi na Nando) alipokuwa anaiwakilisha nchi yake kuzifukuzia $300,000.

Selly mwenye miak 25 alisema “I am very thankful for the opportunity given me. I want to thank my boyfriend, Praye Tietia and also use this opportunity to say I am very sorry (for all that happened)”, na akasisitiza “I am very sorry”.

Selly amekuwa akiandamwa na maneno mengi toka camera za Big Brother zimnase akifanya mapenzi na aliyekuwa mwandani wake katika The chase Nando, kitendo kilichowaudhi zaidi mashabiki wa nchini kwake Ghana ambao wamekuwa wakimuandama kupitia mitandao ya kijamii.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...