Saturday, August 03, 2013

KESI YA JENGO LA GHOROFA JIRANI NA IKULU LAZIDI KUWANASA WATU WENGI


UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya jengo refu la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu bila kufuata utaratibu unatarajia kuita mashahidi 13 na vielelezo 20 kuthibitisha mashtaka dhidi ya vigogo walioruhusu ujenzi huo.

Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.

Alikuwa akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi fimbo.

Swai alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 7 mwaka kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga.



Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.

Akisoma maelezo hayo, Swai alidai Kimweri alikuwa na wadhifa huo TBA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010 na Maliyaga aliajiriwa mwaka 2002 akiwa msanifu mkuu.

Swai alidai kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na TBA, ambako hadi mwaka 2006 kilikuwa hakijaendelezwa.

TBA, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma iliwaalika wanaotaka kuwekeza kuwasilisha andiko la awali kwa ajili ya uendelezaji.

Kesi hiyo itasikilizwa Agosti 7 mwaka huu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...