Zanzibar.
Mahakama Kuu ya Zanzibar, imekataa kumwachia kwa dhamana, mshtakiwa
Omar Mussa Makame, anayekabiliwa na shtaka la kumuua Padri Evarist Mushi
wa Kanisa Katoliki.Hatua hiyo ilifanywa
jana na Jaji Mkuza Issac Sepetu, baada ya upande wa utetezi katika kesi
hiyo ,kuiomba mahakama imwachie kwa dhamana mshtakiwa hadi hadi hapo
upande wa mashtaka, utakapokamilisha upelelezi.Alisema mahakama itaendelea na kesi isiyokuwa na dhamana na ambayo upelelezi wake unaweza kuchukua hadi miezi tisa.
Jaji huyo alisema mahakama haifanyi kazi zake kwa kuzingatia taarifa za watu au magazeti yaliyoko nje yake.“Mahakama
hii haichukui vielelezo vya barua za nje ya chombo hiki. Mtu anayeweza
kusema kila kitu ni mkurugenzi wa mashtaka, yeye ndiye mwenye dhamana ya
kuondoa kesi mahakamani,” alisema Jaji Sepetu.
Baada
ya msimamo huo, wakili Abdallah Juma anayemtetea mshtakiwa, aliiomba
mahakama iuamuru upande wa mashtaka ,kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.
Alisema ni vyema upande huo ukatoa muda maalum wa kukamilisha upelelezi huo.
Jaji aliipanga kesi hiyo kutajwa tena Julai 2 mwaka huu.
Omar ambaye ni mkazi wa Mwanakwerekwe, Mjini Magharibi, anadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padri Mushi Februari 17 mwaka huu.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment