Friday, June 07, 2013

HUYU NDIYE DADA WA KIZUNGU ANAYEDAIWA KUWA NDIO SHEMEJI WETU KWA NGWEA

Mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa demu wa Ngwea aitwaye Misheily akilia kwa uchungu wakati wa kuaga.
Na Gladness Mallya
MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa demu wa Ngwea aitwaye Misheily.Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo ambaye huenda walikuwa na malengo mazuri ya baadaye.

...akiwa na simanzi nzito.
Aidha, kilio alichokuwa akiporomosha binti huyo kiliwafanya watu waliokuwa karibu naye kumsikitikia na kuzidishiwa majonzi kwani ilifika wakati akaishiwa nguvu.
...Akitolewa eneo hilo kwa kusaidiwa na mtu wake wa karibu.
Paparazi wetu alijaribu kumfuata na kumuomba kuzungumzia juu ya kifo cha Ngwea lakini alikataa na kusema asingeweza kufanya hivyo kufuatia majonzi aliyokuwanayo huku akionekana kutoamini kama jamaa yake huyo ametutoka .
 
na global publisher

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...