Monday, May 20, 2013

YANGA: MRISHO NGASSA ATAMBULISHWA RASMI KUREJEA YANGA HII LEO



Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.


Mrisho Ngassa ambaye anarudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo kwa kutimkia kwa Matajiri wa Bongo, Azam FC na baade mwaka jana kuzwa Simba kwa Mkopo baada ya kutokea sintofahamu za kimaadili ndani ya Klabu yake hiyo.

Ngassa alienda kuichezea Simba msimu uliopita baada ya Klabu yake ya Azam kuchukizwa na kitendo chake cha kuibusu jezi ya Yanga wakati timu hizo zikicheza.

Ngassa anakuwa ni mchezaji wa kwanza kuatangazwa na klabu hiyo kumsajili muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.

Mrisho Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo, makao ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...