Tuesday, April 30, 2013

Shambulio lafanyika mjini Rome wakati serikali mpya ikiapishwa.


Serikali mpya nchini Italia imeapishwa na kumaliza hali ya iliyodumu kwa miezi kadhaa ya wasiwasi wa kisiasa, kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Februari mwaka huu, ambao ulishindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja.
Hata hivyo hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilifunikwa na tukio la ufyatuaji risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo maafisa wawili wa polisi walishambuliwa.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona mwanaume mwenye silaha akifyatua risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu katikati ya mji wa Rome, wakati baraza jipya la mawaziri likiendelea kuapishwa, umbali wa kilomita moja kutoka hapo, katika ikulu ya rais.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...