WAREMBO
14 kutoka vitongoji vitano vya wilaya za Siha na Hai, Kilimanjaro,
akiwemo mdogo wake Wema Sepetu, wamejitokeza kushiriki shindano la
kumsaka mrembo wa Hai, ‘Redds Miss Hai 2013.
Shindano
hilo linalotarajiwa kulindima Hoteli ya Snow View Bomang’ombe Hai,
Ijumaa.Akizungumza mjini hapa jana, muandaaji wa mashindano hayo,
Grace
Mmari,
kupitia kampuni ya ulinzi ya FEM ya jijini Arusha, alisema maandalizi
ya mashindano hayo yamekamilika na tayari warembo hao wako kambini kwa
wiki mbili sasa katika hoteli ya Sinza B.
Alisema
warembo hao wamepatikana kutoka vitongoji vya Kwa Sadala, Bomang’ombe,
Sanya Juu, Machame na KIA, ambao wana vigezo vyote huku akitamba mwaka
huu, Mrembo wa Tanzania atatoka wilaya ya Hai.
“Warembo
wangu ni wazuri, warefu, wanajiamini na wana uwezo wa kuwakilisha
vyema wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro na hata taifa, kwa kuwa tunao
kina Wolper wengine hapa na kina Sepetu wapo pia,“ alisema.
Alisema
miongoni mwa warembo waliojitokeza kushiriki shindano hilo ni pamoja
na mdogo wa mrembo wa zamani wa Miss Tanzania (2006), Wema Sepetu, Weru
Sepetu, ambaye alidai kuwa huenda akafuata nyayo za dada yake.
Aliwataja
warembo watakaoshiriki shindano hilo kuwa ni Sharon Abdalah, Zena
Ally, Ivony Steven, na Winny Shayo wanaotoka Machame na Sanya Juu.
Wengine ni Julieth Kimaro, Rehema John, Mary Chemponda, Catherine Leonard na Modesta Joseph.
Mmari
alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Rich Mavoko pamoja na Jambo Squad, ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga.
Kwa
upande wake, mwalimu wa warembo hao, Evameri Gamba, alisema warembo
wanaendelea na mazoezi ya mwisho pamoja na kushiriki shughuli
mbalimbali za kijamii, ikiwemo uoteshaji wa miti na kutembelea wagonjwa
katika hospitali ya wilaya ya Hai.
Shindano hilo linafanyika kwa mara ya pili sasa, huku wadhamini wakiwa
ni TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, Fem Security, Bonite
Bottlers, Snow View Hotel, Panone pamoja migodi ya madini ya Anglo
America Mining na Manga Germ.
No comments:
Post a Comment