Sunday, September 28, 2014

TAZAMA FILAMU YA YESU KWA LUGHA YA KINYAKYUSA.....!!!


 

Fanya siku yako kuwa nzuri kwa kutazama filamu ya Yesu kwa lugha ya kinyakyusa. Share na wenzio waione. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POLISI MORO WAFICHUA SIRI YA KUINYAMAZISHA SIMBA SC


s13

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
NAHODHA wa Polisi Morogoro Nicholas Kabipe amefichua siri ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara iliopigwa jana uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Simba walikuwa kwa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza kupitia kwa Emmanuel Okwi, lakini Danny David Mrwanda aliisawazishia Polisi katika dakika ya 50 kipindi cha pili.
Kabla ya mechi ya jana, Polisi walifungwa 3-1 na Azam fc katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa wikiendi ya septamba 20 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya Simba, Kabipe alisema: “Kwa matokeo haya sisi tumefurahi kwasababu tulipoteza mchezo wa kwanza. Kuna makosa yalikuwa yanatugharimu na Azam wakatufunga magoli matatu.
“Tumerekebisha hayo makosa na tumeweza kupata sare. Wakati wa mapumziko tukiwa nyuma kwa goli moja kwa bila, mwalimu alituelekeza kuwa Simba wana kasi sana sehemu ya kiungo”.
“Kwahiyo akasema tunatakiwa tuwe wengi katikati ili tusiwape nafasi ya kucheza, tuwe tunaenda kukaba watu watatu na tulifanya hivyo, ikawezekana na tukaweza kupata sare hiyo”. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 28, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ARSENAL YAPONEA CHUPUCHUPU EMIRATES….OXLADE-CHAMBERLAIN AOKOA JAHAZI

1411841753978_wps_25_Arsenals_English_striker_
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain (kushoto) alifunga goli la kusawazisha dhidi ya Tottenham
MASHABIKI wa Emirates walishangilia kwa matarajio ya kushinda mechi ya watani wa jadi wa kaskazini mwa London baina ya Arsenal na Tottenham, lakini wametoka sare ya 1-1.
Arsenal walitawala mchezo na kushambuli zaidi, lakini hawakuweza kupata magoli.
Tottenham walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 56 kupitia kwa Nacer Chadli, lakini Alex Oxlade-Chamberlain aliisawazishia Arsenal mnamo dakika ya 74.
Arsenal's Alex Oxlade-Chamberlain celebrates scoring the equaliser against Tottenham at the Emirates
Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia goli lake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAANDAMANO YA KUMPINGA KABILA YAFANYIKA

Rais Joseph Kabila
Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila.
Wafuasi wa upinzani wanataka rais Kabila kuondoka madarakani wakati muhula wake wa pili wa uongozi utakapomilika mnamo mwaka 2016.
Kuna shaka kuwa huenda katiba ikabatilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu.
Maandamano kwenye mji mkuu Kinshasa yaliripotiwa kuwa ya amani lakini polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo.
Rais Joseph Kabila alichukua mamlaka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa babake Laurent Kabila. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...