Friday, April 25, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.

SIKU 67 ZA MIPASHO, MATUSI, BUNGE MAALUM LA KATIBA

bunge 4c2f3
Na Hudugu Ng'amilo.
Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta "Mzee wa Kasi na Viwango" linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.
Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

OBAMA AWASILI KOREA KUSINI

Rais Obama akifanya mashauriano na Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye (kushoto) na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.
Rais Obama amewasili Korea Kusini huku hofu ikizagaa kwamba Korea Kaskazini huenda inajiandaa kufanya jaribio la nne ya zana zake za nukyla.
Inatarajiwa kwamba shughuli mpya katika kinu cha nuklya mjini Pyongyang zitatawala mazungumzo kati ya bwana Obama na rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.
Viongozi hao wawili wanarajiwa kuangazia zaidi jukumu la Uchina katika kuithibiti Korea Kaskazini, jambo ambalo Bwana Obama ametaja kuwa lenye umuhimu mkubwa.
Rais wa Marekani Barack Obama amewasili Korea Kusini katika sehemu yake ya pili ya ziara katika Bara la Asia. Anatarajiwa kukutana na Rais Park baadaye leo na kuwatembelea wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo.
Ziara yake inafanywa wakati ambapo kuna hofu kuwa Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio la nne la Kinukilia.
Korea Kaskazini inatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao wawili na tayari kuna ripoti kuwa maandalizi ya kufanya jaribio la Kinukilia yanayoendelea kufanywa Korea Kaskazini yatahakikisha kuwa taifa hilo jirani linapewa kipao mbele katika mashauriano.
Picha zilizochukuliwa na mitambo ya Sattelite zinaonyesha kuwa kuna masanduku mengi yanayohamishwa hapa na pale katika eneo linalotarajiwa kufanyiwa zoezi hilo Korea Kaskazini. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

KERRY ASHUTUMU URUSI KWA GHASIA UKRAINE

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John Kerry akizungumza na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amelaumu Urusi kwa kuchochea mapigano Mashariki mwa Ukraine.
John Kerry alisema ujasusi wa Marekani una hakika kuwa Urusi imetoa silaha na wapiganaji na pia inaendelea kugharamia na kusimamia wapiganaji wa nchini Ukraine kushiriki ghasia hizo.
Katika lugha ya hasira, Bwana Kerry, alishambulia Urusi akisema kuwa taifa hilo limeshindwa kuchukua hatua madhubuti za kujaribu kutuliza uhasama ulioko nchini Ukraine kama ilivyokubaliwa mjini Geneva juma lililopita.
Bwana Kerry alisema kuwa Urusi inasimamia ghasia zinazoendeshwa na watu wanaotaka kujitenga kutoka kwa Ukraine Mashariki mwa taifa hilo na kujaribu kusababisha ghasia ili kuhujumu uchaguzi unaotazamiwa kufanywa mwezi ujao.
Kwa hasira, Bwana Kerry alilaumu Urusi kwa ghasia zote zinazoendelea Ukraine wakati huu. Ingawa hakutangaza vikwazo inavyoweza kuongezewa Urusi Bwana Kerry alisema mwanya wa kuimarisha amani katika Ukraine unaendelea kuziba. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...