Friday, March 13, 2015

CHAMBERLAIN KUKAA NJE MWEZI MMOJA

 Alex Oxlade-Chamberlain hatokuwepo kwa mwezi mmoja
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlainhatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kulingana na kocha huyo,Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal kuimarisha matokeo yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya tatu .
Alex Oxlade-Chamberlain alichangia pakubwa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester united katika FA
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidi ya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi tarehe 4.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

FORLAN ATUNDIKA DARUGA KIMATAIFA

IMG_20150312_202943
Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Manchester United, Atletico Madrid, Intermilan Diego Forlan jana ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Uruguay baada ya kuichezea timu hiyo tangu mwaka 2002.
Forlan,35, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Cerezo Osaka ya nchini Japan amekuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Uruguay na mwaka 2010 aliiwezesha timu hiyo kushinda nafasi ya 3 kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika huko nchini Afrika kusini huku yeye akibeba tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo baada kuonesha kiwango bora.
“Ninawashukuru kwa wote walionipa ushirikiano tangu naanza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002, ninaamini timu itaendelea kufanya vizuri na nimechukua uamuzi huu ili kutoa kwa nafasi kwa wachezaji wengine ambao ninatumaini wataisadia timu hii” alisema Forlan.
Mchezaji huyo aliyepata sifa nyingi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya adhabu mpaka anatangaza kustaafu tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uruguay michezo 112 na kufunga magoli 36. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, March 12, 2015

KONTENA LALALIA BASI, LAUA WATU 42, LAJERUHI 23

Basi la Majinja likiwa limeangukiwa na kontena na kusababisha vifo katika eneo la Changalawe mafinga.

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 23 kujeruhiwa baada ya lori la mizigo kugongana na basi na kontena lililokuwa limebebwa kuangukia gari hilo la abiria, katika ajali ya aina yake iliyotokea eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa.
Watu 37 waliokuwa kwenye basi hilo la kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam, walifariki papo hapo na wengine watano kufariki wakiwa Hospitali ya Mafinga. Dereva wa basi na wa lori hilo la kampuni ya Cipex, pia wamefariki.
Shuhuda mmoja wa ajali hiyo, Nyasio Pascal, aliyekuwa akiendesha basi la Saibaba, alisema aliliona lori hilo likijaribu kukwepa mashimo kwenye barabara hiyo ambayo ni nyembamba, na mara likaanza kuyumba kulia na kushoto baada ya kukanyaga shimo na ndipo lilipolifuata basi na kugongana nalo.
Alisema kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo, liliangukia juu ya basi na kulikandamiza, jambo ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi na pia kuzuia watu waliokuwa karibu na ajali kuokoa watu waliojeruhiwa hadi tingatinga lilipowasili. Hata hivyo, alisema mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja, alinusurika kwenye ajali hiyo bila ya kudhurika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

NENO KUTOKA YEREMIA 32:27 LILILOPO KWENYE KAMPUNI YA MAJINJA SPECIAL

Yeremia 32 : 27
"Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?"

ZITTO KABWE KUIBUKIA KIGOMA KESHO

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe  

Siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kesho atatua jimboni kwake kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Uamuzi wa kumfukuza Zitto (pichani) ulifikiwa juzi ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya Wadhamini na katibu mkuu wa Chadema, iliyokuwa imeshikilia uanachama wake.
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ndiye alitangaza kutimuliwa kwa Zitto akisema ni kutokana na kufungua kesi mahakamani, kinyume na Katiba ya Chadema kipengele cha 8 (a) (x). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO MARCHI 12, 2015


..
. 


. 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CHEYO AKARIBISHA 'WAGENI' KUWANIA URAIS UDP

Mwenyekiti wa UDp, John Cheyo. 

Mbunge wa Bariadi  Mashariki na Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo  amesema wanakaribisha wanachama wa chama chochote cha siasa nchini kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, kiongozi huyo alisema chama hicho bado hakijateua mgombea  urais hivyo milango iko wazi kwa wanasiasa ambao wako tayari kujiunga na chama hicho kwa lengo la kuwania urais.
“Hiki chama ni cha watanzania wote hivyo tunatoa rai kwa mtu yeyote  aliye tayari kuwa mwanachama wetu milango ya kuwania urais kupitia chama hiki ipo wazi’’ alisema Cheyo
Alisema  yeye bado hajaamua kuwania nafasi hiyo kwa sasa muda ukifika atasema lakini kwa sasa ni mapema kutoa tamko kwamba atawania wadhifa huo.
Aliongeza kwamba  anasikitishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwahamasisha watu wasipigie kura Katiba inayopendekezwa, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyima haki wananchi.
‘’Raia wote wana haki ya kupiga kura sasa ikiwa Ukawa wanatembea kila kona ya nchi kuwahamasisha wananchi kuacha kuipigia kura katiba hiyo ni kosa,’’ alisema Cheyo
Pia Kiongozi huyo wa UDP alisema tume ya uchaguzi ndio yenye majibu ya mashine zinazotumika kuandikisha wapiga kura  kwenye daftari la kudumu, (BVR) kwamba zinafaa au hazifai.
Alisema anashangazwa sana na baadhi ya watu hususan wanasiasa na wasomi wanaojitokeza na kusema mchakato wa kuandikisha wapiga kura usimamishwe kwa sababu zao mbalimbali . Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...