Monday, October 06, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS KENYATTA TAYARI KWENDA ICC

Rais Kenyatta anasema anajiamini na kwamba anajua hana hatia katika tuhuma zinazomkabili
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.
Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.
Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.
Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.
Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.
Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.
Takriban wabunge miamoja wanajiandaa kuambatana na Kenyatta Hague katika ishara yao ya kumuunga mkono. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JESHI LA SOMALIA NA AU WADHIBITI BARAWE

Wanajeshi wa Somalia
Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na vikosi vya Muungano wa Afrika kwa sasa wamechukua udhibiti wa mji wa Barawe ambayo ni ngome ya mwisho ya wanamgambo wa al-Shabab.
Wanajeshi hao waliingia mji wa Barawe ulio kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumatatu baada ya kuuzingira tangu siku ya Jumapili.
Sauti za risasi zilisikika mapema Jumatau wakati wanajeshi walikuwa wakiingia mji huo. Ripoti zinasema kuwa kwa sasa mji huo umetulia na magari ya kijeshi kwa sasa yanapiga doria.
Mji wa Barawe haujakuwa chini ya serikali kwa miaka 23 na umekuwa chini ya udhibiti wa al Shabab kwa miaka sita iliyopita.
Gavana na maafisa wa kijeshi waliwahutubia wenyeji leo ambapo walitoa wito wa kuwepo kwa utulivu wakisema kuwa nyakati za al-Shabab zimekwisha.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay alipongeza jeshi hilo la pamoja na kusema kuwa sasa Somalia ina mazuri siku za usoni.
Kutwaliwa kwa mji huo ni pigo kwa kundi la al-Shabab lililo na uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.
Al Shabab wamekuwa wakiutumia mji huo kupitisha silaha na chakula na pia kama kituo cha biashara ya makaa.
Muungano wa Afrika pia unasema kuwa al-Shabab waliutumia mji wa Barawe kupanga mashambulizi yao dhidi ya mji mkuu Mogadishu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

JULES BIANCHI APATA AJALI

Jules Bianchi
Katika Mashindano ya mbio za magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules Bianchi, yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika mashindano ya Japan Grand Prix. Madaktari wa upasuaji wanaendelea kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu wakati alipofikishwa hospitalini hapo.Bianchi alipoteza uelekeo wa gari lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa.Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton alitangazwa mshindi katika mashindano hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA INAVYOSHINDA BILA WASHAMBULIAJI KUFUNGA MABAO

IMG_2927
Yanga SC ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro baada ya kulala kwa mabao 2-0, lakini timu hiyo imemudu kupandisha kiwango chake cha kujituma, umakini na nidhamu na kufunga mabao manne katika michezo miwili iliyopita ukiwemo ushindi wa siku ya Jumapili dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ilipata ushindi wake wa kwanza msimu huu katika ligi kuu baada ya kuichapa, Tanzania Prisons ya Mbeya kwa mabao 2-1 wiki moja iliyopita, na jana wakaifunga JKT Ruvu inayofundishwa na mchezaji/kocha wao wa zamani Fred Minziro kwa ushindi kama.
Michezo yote hiyo ilifanyika katika uwanja wa Taifa hivyo kufanya mabingwa hao wa zamani kusogea hadi katika nafasi ya Tatu nyuma ya Azam FC kwa tofauti ya pointi moja, na pointi Tatu nyuma ya vinara Mtibwa ambao walishinda kwa mara ya Tatu msimu huu katika uwanja wa nyumbani. Mtibwa imekusanya pointi tisa baada ya kuzishinda Yanga, Ndanda FC na JKT Mgambo.JAJA
Hakuna mshambulizi aliyefunga bao hadi sasa katika dakika 270 katika kikosi hicho cha mkufunzi, Mbrazil, Marcio Maximo. Baada ya viungo, Andre Coutinho na Saimon Msuva kufunga katika ushindi dhidi ya Prisons, mlinzi Kelvin Yondan alifunga moja ya mabao mazuri hadi sasa katika ligi kuu wakati alipomnyang’anya mpira mshambulizi, Iddi Mbaga na kuanzisha ‘ move’ aliyopanda nayo hadi alipokutana na pasi ya mwisho kutoka kwa Haruna Niyonzima. Kelvin alipiga kiufundi mpira akiwa ndani ya eneo la hatari na kuupeleka pembeni kabisa ya ‘ angle’ na kumuacha golikipa, Jackson Chove akishindwa la kufanya. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YANGA MDOGO MDOGO, MTIBWA KILELENI

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la pili walilopata katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 2-1.

Yanga imeendelea kutoa dozi Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa 2-1 JKT Ruvu katika mechi iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa huku Mtibwa Sugar ikiichapa Mgambo Shooting 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Hii ni mechi ya pili kwa Yanga kushinda katika Ligi Kuu kwani iliichapa Tanzania Prisons 2-1, lakini katika mechi yake ya ufunguzi wa msimu huu ilichapwa 2-0 na Mtibwa hivyo kuanza safari yake ya kusogea katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kwa mwendo mdogo mdogo.
Katika mechi ya jana, hadi mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa kwa shuti kali na beki Kelvin Yondani dakika ya 35 akiunganisha pasi safi ya Haruna Niyonzima.
Bao la pili la Yanga lilifungwa na Niyonzima kwa mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni dakika ya 73 huku bao la JKT Ruvu likifungwa dakika ya 90 kwa shuti kali na Jabir Aziz akiwa nje ya 18. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, October 04, 2014

MIAKA 15 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWL. J. K. NYERERE

Mwalimu J. K. Nyerere na aliyekuwa Rais wa Msumbiji marehemu Samora Machel.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WABUNGE KUANDAMANA NA KENYATTA ICC


Rais Uhuru Kenyatta akiwasili katika mahakama ya kimataifa ya ICC

Idadi kubwa ya wabunge nchini Kenya wanajiandaa kuandamana na Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC,Uholanzi ambako anatarajiwa kuhudhuria kikao maalum kuhusiana na kesi inayomkabili katika mahakama hiyo.
Kenyatta ametakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo tarehe nane mwezi huu huku kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda akilalamika kuwa Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo kuhusiana na ushahidi dhidi ya Kenyatta.
Mapema wiki hii, mahakama hiyo ya ICC ilitupilia mbali ombi la Rais Kenyatta, la kutaka kikao hicho cha Octoba 8 kuhairishwa au aruhusiwe kutumia video. Majaji wa Mahakama hiyo walimuagiza Uhuru kufika binafsi mbele yao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TOFAUTI YA DINI YAVUNJA NDOA INDIA

Ndoa ya kihindi
Maafisa wa polisi katikati mwa India wamefutilia mbali harusi kati ya mwanamume mkristo na mwanamke wa kihindu baada ya shinikizo kutoka kwa makundi ya kihindu yenye mrengo wa kulia.
Wanandoa hao wawili kutoka Madhya Pradesh walitoroshana na kuoana katika sherehe ya kihindu bila ruhusa ya familia ya msichana.
Baada ya makundi hayo ya Kihindu kupinga hatua hiyo na kutishia kushambulia majengo ya serikali,maafisa wa polisi katika eneo hilo waliwasaka wapenzi hao na kuwalazimisha kuachana.
Waandishi wanasema kuwa hatua hiyo ya makundi ya kihindu imekuwa ya kawaida katika jimbo hilo katika siku za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MESSI AKUTWA NA KESI YA KUKWEPA KULIPA KODI

messi
Nyota wa Barcelona Lionel Messi anakabiliwa na kesi ya kukwepa kodi,majaji nchini Hispania wamethibitisha tuhuma hizo.
Ikumbukwe Messi alikuwa akikabiliwa na tuhuma za ukwepaji kulipa kodi kwa muda sasa.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, October 03, 2014

KURA MBILI ZAPITISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

http://jambotz8.blogspot.com/

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Deo Sanga akisakata muziki katikati ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura zilizopigwa kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba inayopendekezwa mjini Dodoma jana.


Dodoma/Dar. Licha ya upinzani kutoka makundi kadhaa ya wananchi, Bunge la Katiba jana lilihitimisha kazi yake kwa kupitisha Katiba inayopendekezwa baada ya kupata theluthi mbili za wajumbe wa kila upande wa Muungano.

Matokeo hayo yaliyohitimisha mchakato huo, yalifanikishwa kwa tofauti ya kura mbili za wajumbe katika baadhi ya ibara na nyingine kwa kura moja tu, ikimaanisha kuwa iwapo kura hizo mbili zingekosekana hadithi ingekuwa tofauti.

 Kutangazwa kwa matokeo hayo kuliwafanya wajumbe walioshiriki mchakato hadi hatua ya mwisho baada ya wenzao wa kundi la Ukawa kususia, kulipuka kwa furaha, nyimbo, tambo, vijembe na vigelegele huku wakijimwaga ukumbini kusakata dansi.

Akitangaza matokeo hayo, Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashililah alisema hali ya upigaji kura ilikuwa ni nzuri na kila kura za kila upande zilitosheleza na kutoa uhalali wa Katiba inayopendekezwa kupelekwa kwa wananchi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PINDA: "KATIBA IPATIKANE KABLA YA RAIS MPYA"


Bunge Maalumu la Katiba, kabla ya kuahirishwa kwake 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema atafurahi kuona mchakato mzima wa Katiba ukikamilika kabla rais mpya hajapatikana katika Uchaguzi Mkuu ujao, pendekezo ambalo ni kinyume na makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuwa upigaji wa kura ya maoni ufanyike baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Akizungumza Bungeni baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta kutoa shukrani, Pinda alipendekeza kura ya maoni ipigwe sambamba na Rais ili kiongozi ajaye afanye kazi ya kutekeleza matakwa ya Katiba hiyo.

Alisema rais ajaye anaweza kuwa na ajenda zake, hivyo ni muhimu kumaliza kazi yote na kumkabidhi Katiba ambayo imekamilika ili aitekeleze.

“Nampongeza sana mwenyekiti kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana kwa wakati na kwa kuzingatia maoni ya wananchi,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alichojifunza

Pinda alieleza kuwa katika mchakato huo wa Mabadiliko ya Katiba, amejifunza mambo makuu manne, kubwa likiwa ni kutii sauti ya wengi, kwani ni sauti ya Mungu. Alisema wingi wao bungeni ni kiashiria cha uwepo wa sauti ya Mungu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

http://jambotz8.blogspot.com/
Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita.
Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini.
Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa.
Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za kufyatua risasi.
Ndugu ya waliouawa wanaosaidiwa na polisi waliingia mlango kwa mlango katika eneo la Iguala wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao na kutafuta eneo ambalo miili ya ndugu zao ilipofichwa. Serikali ya jimbo hilo imetoa dola 75,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kueleza wanafunzi hao walipo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI WA HONG KONG KUKUTANA NA SERAKALI

http://jambotz8.blogspot.com/
 
Viongozi wa wanafunzi huko Hong Kong wamekubali kukutana na upande wa serikali kujadili malalamiko yao siku tano baada ya maandamano makubwa ya kupigania demokrasia.
Hiyo inafuatia mwaliko kutoka kwa mkuu wa utawala wa Hong Kong CY Leung. Alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao waliotishia kuvamia majengo ya serikali iwapo mkuu huyo hatajiuzulu.
Muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao umemalizika salama.
Bwana Leung amesema atabakia madarakani na kuwaonya waandamanaji kuwa watapata matatizo iwapo watavamia majengo ya serikali.
Kumekuwa na makabiliano makali katika eneo la majengo ya serikali ambapo waandamanaji wamekuwa wakiendelea kudai uchaguzi wa haki mwaka 2017. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...