Thursday, October 17, 2013

REFA ALIYEPIGWA NA YANGA MWAKA JANA KUCHEZESHA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI TAIFA

01_d16d6.jpg
Na Princess Asia, Dar es Salaam
REFA aliyewahi kupigwa na wachezaji wa Yanga SC Machi mwaka jana timu hiyo ikifungwa 3-1 na Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Israel Nkongo Mujuni ndiye atakayepuliza filimbi katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya watani wa jadi, Jumapili.
Nkongo alipigwa na wachezaji wa Yanga baada ya kumtoa kwa kadi nyekundu beki Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa tayari amempa kadi nyekundu kiungo Haruna Niyonzima pia.
Stefano Mwasyika aliyehamia Ruvu Shooting alimtupia ngumi ya 'kibondia' Nkongo na Nadir Haroub 'Canavaro' alionekana kuhusika katika vurugu hizo wote wakafungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mashabiki wa Yanga SC walifanya vurugu kubwa na kuvunja viti Uwanja wa Taifa siku hiyo.

Yamepita hayo na Nkongo amepewa tena mechi ya Yanga. Marefa wote wanne walioteuliwa kuchezesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Simba na Yanga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wanatambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
Mbali na Nkongo atakayepuliza filimbi, wengine ni Hamisi Chang'walu atakayeshika kibendera upande wa jukwaa kuu na Ferdinand Chacha atakayeshika kibendera upande wa pili, wakati mezani atakaa Orden Mbaga.

MUSEVENI ATAKA WAPINZANI WAMUOMBE RADHI

col-kizza-besigye_3dbc4.jpgyuweri_71085.jpg

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewataka viongozi wawili waandamizi wa upinzani nchini Uganda kuacha mapambao ya kisiasa wasiyoweza kushinda na badala yake wajiunge na chama tawala cha National Resistance Movement-NRM.
 Bwana Museveni alimshutumu mpinzani wake Kizza Besigye na meya wa Kampala, Erias Lukwago kwa kupinga program za maendeleo za serikali na kutangaza uongo. Alitaka aombwe msamaha na wapinzani hao wawili.
Lakini wote Besigye na Lukwago walipuuza wito wa Museveni wakiuita mchezo wa kisiasa wa kutaka kupata uungaji mkono wa chama tawala katika mji mkuu ambako wapiga kura mara nyingi hawakiungi mkono chama tawala.
Rais Museveni na chama chake tawala cha NRM wamekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Lakini Lukwago anasema matamshi ya karibuni ya Museveni ni matokeo ya kile anachosema kinaonekana ni mgawanyiko katika chama tawala.
Lukwago alisema maafisa wa utawala mara kwa mara wanakataa kufanya kazi na wapinzani kuhusu wasi wasi wa umma shutuma ambazo wawakilishi wa chama tawala wanazikanusha hazina ukweli. Wanaushutumu upinzani kwa kuzorotesha juhudi za serikali za kuendeleza sheria na kanuni na kuhakikisha amani na uthabiti nchini humo. Kitu ambacho Lukwago hakubaliani nacho. Chanzo: voaswahili

Wednesday, October 16, 2013

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA AWASILI CHINA NA KUPOKEA TAARIFA, ASIKITISHWA NA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA



IMG_0072
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
*Asikitishwa na idadi kubwa ya wasafirishaji wa dawa za kulevya

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili Beijing, China saa 10 leo jioni (Jumatano, Oktoba 16, 2013) na kuanza vikao ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi yake ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Beijing, Waziri Mkuu alielekea kwenye nyumba ya wageni ya Serikali ya Diaoyatui ambako alipokea taarifa fupi kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini China.
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Balozi wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali (Mst.), Abdulrahman Shimbo alisema sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi kati ya Tanzania na China iko chini ya mwamvuli wa FOCAC (Forum on Africa China Cooperation) ambayo inagawanyika katika maeneo sita.
 Alyataja maeneo hayo kuwa ni misaada (grants), mikopo ya masharti nafuu (preferential loans), mikopo ya kibiashara (preferential buyers credit), uwekezaji, ushirikiano maalum na ushirkianao wa kihistoria.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ASISITIZA AMANI BARAZA LA IDD ZANZIBAR

DSC_0112
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiomba Dua pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.kulia kwake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis na kushoto yake ni Katibu mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdalla Twalib,Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanizbar Maalim Seif Sharif Hamadi na wamwisho ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmod Mussa Wadi. DSC_0230
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba katika baraza la Idi -El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja DSC_0206
Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI ALI-HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MUME AMKATA MKEWE MGUU HUKO TARIME MKOANI MARA

Na Waitara Meng’anyi, Tarime


 Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake  aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

ANGALIA VIDEO YA RAIS KIKWETE ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA


JAMBO TZ INAWATAKIA EID MUBARAK NYOTE!


KUMBE SHOW ZA MAJUU SIO KAMA ZA BONGO! - OMMY DIMPOZ


Ommy alikuwa akiongea na kipindi cha Ampilifaya jana baada ya kurejea kutoka nchini Marekani alikokuwa kwenye ziara ya wiki tatu.

“Naweza kusema hapa nyumbani tunalipwa hela nyingi kuliko tunavyopata nje kwa msanii yeyote kwa asilimia kubwa. Inategemea pia unaenda kufanya tamasha sehemu gani. Kwahiyo asilimia kubwa hela unatengeneza zaidi nyumbani,”alisema Ommy.

Alisema hiyo ni kwasababu show za Tanzania huhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko inavyokuwa nchi za nje ambako ni watu wachache sana huingia japo kiingilio ni kikubwa na wengi wanaohudhuria ni watu waliotoka Afrika Mashariki zaidi.
Katika hatua nyingine, leo Ommy Dimpoz kupitia Instagram, ameandika maneno ya shukrani kwa wote walioifanikisha show yake.

“AssaLaam ALeykum Ndugu zangu, Eid MubaraQ Ndugu, jamaa, Marafiki, and all my Fans all over the world…Namshukuru Mungu Alhamdulilah nimerudi nyumbani Salama Kuendelea na Majukumu mengine baada ya Tour ya Takriban Mwezi Mmoja…Ningependa kuchukua Nafasi hii kuwashukuru @Dmkglobal promotion na J&P kwa kufanikisha tour yangu ambayo imeweza kuwa na Mafanikio makubwa Na kufanikisha baadhi ya malengo ambayo mengine sikuyatarajia.Pia ningependa kuwashukuru watu wote ambao walionyesha support kipindi chote cha tour yangu hususan Watanzania wenzangu na Watu wa Africa Mashariki na Kati ambao walionyesha Ushirikiano na support ya kutosha tangia mwanzo mpaka mwisho wa tour yangu…Nachoweza kuwaahidi ni kuwa mengi mazuri Yanakuja na Naimani sitawaangusha.Nawatakia mapumziko na sherehe njema za sikukuu ya Idd…. Mimi na team nzima ya pozkwapoz tutakuwa DARLIVE tukitoa Huduma Karibuni sana.LOVE U ALL.” na Vijimambo Blog

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA EID EL HAJ MSIKITI WA ANWAAR MSASANI, DAR ES SALAAM

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 16, 2013

DSC 0137 46fbc
DSC 0138 47cac

Tuesday, October 15, 2013

WAPINZANI KUTINGA IKULU LEO ... MKUTANO MUHIMU WA JK, MBOWE, MBATIA NA PROFESA LIPUMBA LEO UTOE MAJIBU HAYA

Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchni kutoka kushoto: James Mbatia (NCCR Mageuzi), Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF).
Viongozi wa vyama vikuu vya upinzani vyenye wabunge bungeni wanatarajia kukutana leo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, jijini Dar es Salaam kuzungumzia utata wa baadhi ya masuala yaliyojitokeza katika mchakato unaoendelea wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kama wengi tunavyotegemea, mazungumzo hayo kwa vyovyote ni ya masuala nyeti ambayo yamesababisha mvutano na kuibua hisia kali miongoni mwa makundi ya kijamii, pengine kwa kutambua fika kwamba kupuuza madai ya wapinzani ingekuwa sawa na kumwaga petroli katika nyumba inayoungua, busara za rais wetu zimemfanya awaite viongozi wa kisiasa kuteta nao Ikulu.
Wakati viongozi hao, Freeman Mbowe wa Chadema, James Mbatia wa NCCR Mageuzi na Profesa Ibrahimu Lipumba wanakutana na kiongozi wa nchi leo, pengine akiwa hajasaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambao ulipelekwa mezani kwake baada ya kupitishwa bungeni na wabunge wa CCM wiki chache zilizopita, watampa mwanga kilichowafanya waugomee bungeni, maana katika hotuba yake alisema ameambiwa hiki na kile sasa atasikia laivu kutoka kwao.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE, OKTOBA 15, 2013

DSC 0064 8df93
DSC 0065 72acc

KESI YA BABU SEYA NA PAPII KOCHA KUUNGURUMA OKTOBA 30

sEYA11_4aa61.jpg
MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe.
Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. 

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza.

KIKWETE: TUMESHINDA MAADUI ZETU

Picha_na_8_7b2d0.jpg
Rais Jakaya Kikwete amesema maadui wote ambao walitaka kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kwa lengo la kuvuruga amani ya nchi wamedhibitiwa .
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali yake itaendelea kulinda amani ya nchi na maadui wote wanaohusika na kutaka kuvuruga nchi watachukuliwa hatua kali za kisheria. "Kulikuwapo na upepo mbaya, lakini kwa sasa Tanzania ni shwari na tumemshinda adui," alisema Rais Kikwete jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere yaliyoandamana na sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru, mkoani Iringa.
Alisema katika siku za hivi karibuni, maadui wasioitakia mema Tanzania walikuwa na mkakati wa kuvuruga amani ya nchi, lakini Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola vimewadhibiti na nchi iko salama.
Rais Kikwete alisema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa amani kwa sababu inajua wazi kwamba nchi ikiingia kwenye mgawanyiko, mshikamano utavurugika na shughuli za maendeleo zitasimama.

RAILA ODINGA AELEZA NYERERE ALIVYOMSAIDIA KUSOMA NJE

odinga_79ebe.jpg
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameeleza kuwa bila ya Pasipoti ya Tanzania aliyopewa kwa msaada na Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kwenda Ujerumani kusoma baada ya Idara ya Uhamiaji ya Kenya kumnyima hati hiyo ya kusafiria.
Odinga ambaye hivi sasa ni kiongozi mkuu wa Muungano wa Cord ameeleza hayo katika kitabu chake kiitwacho The Flame of Freedom, ambamo ameelezea historia yake na familia yake katika mambo mbalimbali.
Idara ya Uhamiaji ya Kenya ilimnyima Odinga hati hiyo kutokana na Serikali ya kikoloni kuzuia hati ya baba yake, mzee Jaramogi Odinga kwa sababu alitembelea nchi za Urusi na China zilizokuwa maasimu wakubwa wa nchi za Magharibi.

Hata hivyo, Mzee Jaramongi aliamua kusafiria hati ya kimataifa alizopewa na Kwame Nkurumah wa Ghana, pamoja na Gamel Abdel Nasser wa Misri.
Odinga alihitaji hati hiyo kwa kuwa baba yake alitaka amalizie masomo yake nchini Ujerumani baada ya kukatishwa masomo akiwa kidato cha pili mwaka 1962 katika Shule ya Maranda.
Katika kitabu hicho, Odinga alisema hakushangaa kunyimwa hati hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...