Sunday, September 15, 2013

IRENE UWOYA: "ERICK SHIGONGO AMEAMUA KUNICHAFUA MAGAZETINI KWAKUWA NINA KESI NAE MAHAKAMANI..."

 
Irene Uwoya amejibu mapigo ya kudaiwa kuiba simu aina ya iphone 5 toleo jipya la  mwaka  huu ambapo habari hiyo iliripotiwa jana  katika gazeti la Risasi na kutawala mitandao mingi  ya  kijamii. 

Katika  utetezi  wake  alioutoa  kupitia  ukurasa  wake  instagram, Irene  Uwoya amesema kuwa chanzo cha kuandikwa hivyo ni kuvunjwa nguvu katika harakati zake za kesi aliyomfungulia Shigongo

HII  NDO  KAULI  YAKE  :

 "Mi ni mti wenye matunda milele siogopi kupigwa mawe…
"Shigongo kaamua kunichafua coz nina kesi nae mahakamani…anadhani nitaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho wa siku sheria itafuata mkondo wake….

"Mi na yake mengi nayajua ila ngoja ninyamaze nisimwagiwe tindikali"

DIWANI WA CHADEMA KATA YA KIWIRA ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUFANYA NGONO NA MWANAFUNZI.

 
MNAMO TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS  HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBUMBE  KATA YA   KIWIRA – TUKUYU  WILAYA YA   RUNGWE MKOA WA MBEYA,  RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKE SUZANA W/O FRANK, MIAKA 38, KYUSA,  MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU  WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA  KUTATANISHA KWA MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA  SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA  USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.

§  MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA  SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA  KUONA MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA  KUPOTELEWA  NA MTOTO.  HATA HIVYO MAJIRA YA  SAA 09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA  MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA   ALIKUWA NA MHE  DIWANI WA KATA YA  KIWIRA [CHADEMA]  LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA  MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA  KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA  SIMU YA  KIGANJANI.

§  MTUHUMIWA AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .

§  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA  KUFANYA MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI KWA  AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA  BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI  MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO NA TAIFA KWA UJUMLA..

 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 15, 2013

DSC 0042 2292f
DSC 0043 f0163

PADRI ALITISHIWA KIFO MIEZI MITATU KABLA

padri_pix_d2d78.jpg
Padri Joseph Magamba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali akisaidiwa kushuka kwenye ndege na Padri Thomas Assenga(kushoto) wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Zanzibar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana kuelekea katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.Picha na Fidelis Felix
Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang'amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.
Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.


Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

WAFANYAKAZI HARAMU WAMEAJIRIWA KWENYE NAFASI NYETI JNIA

julias_airport_489c3.jpg
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wamedai kuwepo kwa wafanyakazi ambao ni wahamiaji haramu katika uwanja huo, ambao wamekuwa wakipewa nafasi nyeti katika mamlaka hiyo.
Aidha, wameeleza kuwa wahamiaji hao haramu pia wamekuwa wakipatiwa vitambulisho nyeti kama watanzania halisi.
Wafanyakazi walimueleza Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana alipofanya ziara uwanjani hapo na kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) katika uwanja huo.
Mfanyakazi Dominic Bomani alisema licha ya juhudi za serikali kuwaondoa nchini wahamiaji haramu, kiwanja hicho cha ndege kimekuwa chimbuko la wahamiaji hao ambao wamekuwa wakipewa nafasi nyeti.
Aliomba serikali kusaidia katika kuwabaini na kuwaondoa wahamiaji hao ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi hizo ziweze kushikiliwa na watanzania ambao wako wenye sifa stahili.

HII NDIO JEULI YA PESA YA JAGUAR, ANUNUA RANGE ROVER MBILI MPYAAAA KWA PAMOJA



Saturday, September 14, 2013

IRENE UWOYA ATIWA MBARONI KWA WIZI WA SIMU ( AINA YA iPhone 5)

MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
 
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
 
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.

Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.

MULUGO AMEAHIDI KITITA CHA SH. MILIONI MBILI IWAPO TIMU YA MBEYA CITY ITAISHINDA TIMU YA YANGA LEO JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe mkoani Mbeya ameahidi kitita cha sh. milioni mbili iwapo timu ya Mbeya City itaishinda timu ya Yanga ya Jijini Dar es salaam.


Waziri Mulugo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya amesema atahakikisha kuwa kila timu itakayotia mguu mbeya inaondoka na kipigo cha magoli

WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA CHANJO INAYOANGAMIZA UGONGWA WA UKIMWI

Washington. Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu.

Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.

Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 14, 2013

DSC 0020 3186e
DSC 0021 4ba64

SAMAKI HATARI WAINGIZWA NCHINI....!!!

samaki_df55c.jpg
Afya za Watanzania ziko shakani kutokana na kuwapo kwa biashara ya kuingiza samaki kutoka nje ya nchi, wanaodaiwa kuharibika na kuuzwa katika la Soko la Feri jijini Dar es Salaam.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa samaki hao huletwa nchini kutafutiwa soko baada ya kukaa kwenye majokofu kwa muda mrefu huko wanakotoka, kiasi cha kuelekea kuharibika.
Ili wasiharibike, samaki hao aina ya Marckerel hukaangwa hadi wakauke. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanunuzi wake wakuu ni wafanyabiashara wa chakula wakiwamo wamiliki wa migahawa na Mama Lishe wanaofanya shughuli zao katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma.
Samaki hao wanauzwa kwa bei ya chini ambayo ni Sh38,000 kwa boksi lenye uzito wa kilo 15, ikilinganishwa na wanaovuliwa hapa nchini ambao bei yake ni Sh60,000, kwa uzito huohuo.
Inaelezwa kuwa samaki hao baadhi yake ni waleambao wamekwisha muda wake wa kutumika katika nchi hizo, hivyo kuingizwa nchini kutafutiwa soko.
Gazeti hili lilifika katika soko hilo kwa siku mbili na kushuhudia samaki hao wakiuzwa kwa wingi, huku wauzaji wakihimizwa wateja wao kuwahi kuwakaanga au kuwaweka kwenye jokofu.

YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA 15.5m

nsajigwa faa6e
Yanga imepewa siku 14 kuanzia (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.

Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba. Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh. milioni 6.5. Chanzo: shaffihdauda

MUME AMSAMEHE MKEWE ALIYEPANGA KUMUUA....!!!


mke_3e033.jpg
Mwanamke mmoja mfanyabiashara mjini Nairobi, Kenya, ambaye alikiri kosa la kupanga njama ya kumuua mumewe, ameachiliwa na mahakama
Bi Faith Wairimu Maina, aliachiliwa huru baada ya mumewe kuitaka mahakama kufuta kesi yake kwani amemsamehe.
Bi Faith alikiri kuwa aliwakodi mamluki kumuangamiza mumewe. "Nataka kumsamehe kwa sababu ya watoto na familia yetu," mumewe Faith aliambia mahakama.

Mwanamke huyo alikiri makosa ya kupanga njama ya kutaka kumuua mumewe baada ya kukamatwa ingawa baadaye alibadili msimamo wake na kukanusha madai hayo na alitarajiwa kushtakiwa.

Polisi walitibua njama ya mwanamke huyo baada ya majasusi waliokuwa wanajidai kuwa mamluki kupokea malipo ya shilingi 40,000 kuitekeleza njama hiyo.

PADRI AMWAGIWA TINDIKALI ZANZABAR

padri_2e446.png
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.


Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.  Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

MAMA MANGWEA AJITOSA KUMTETEA MWANA FA.

Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la ahadi aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
Tarehe 31 ya mwaka huu ilikuwa ni tarehe ya onesho la The Finest ambalo MwanaFA alikuwa akitimiza miaka 13 ya muziki wake, akawa na lengo pia na kuugeuza muziki wa Hip Hop uwe na sura ya kistaarabu na kibiashara pia ili kuuongezea aina ya mashabiki.
Siku moja kabla ya onesho, msiba wa Albert Mangwea ukatokea, na hapo ikamlazimu mwanamuziki huyo kuahirisha onesho lake, na kulisogeza wiki mbili mbele huku akiahidi asilimia 15 ya faida atakayopata, angeipeleka kwa familia ya Albert Mangwea.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...